Chiwaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2009
- 5,726
- 3,778
5G, Chip na 666. Zina mahusiano makubwa sana.Si nia ya uzi huu kuorodhesha visa vya tanzia tangia kuondokewa bila ya kutarajia na mama yetu mpendwa mama mchungaji. Ikumbukwe kuwa majina ambayo yamekuwa yakiripotiwa ikiwamo humu jamvini ni yale yenye kuhusisha majina makubwa makubwa tu.
Hapa ninaangazia matukio ya juzi peke yake kutokea katika maeneo ya vijijini kuonyesha hali iko je:
Juzi katika mazingira tata kama yanazolingana na sababu za tanzia zinazowekwa humu jamvini siku za hivi karibuni, mkuu wa kituo cha polisi Nyakanazi (Biharamulo) naye katangulia mbele za haki.
Mtu mdogo huyo vijijini huko. Kufariki kwake hakukuonekana mahali popote.
Juzi hiyo hiyo maeneo karibu na mizani ya Nyakahura (Biharamulo) amefariki mtu njiani akipelekwa hospitali akiwa na matatizo ya kupumua.
Juzi hiyo hiyo huko Kahama (Shinyanga) ofisa halmashauri wa wilaya alifariki ghafla kwa matatizo kama hayo hayo ya kupumua.
Nani anawajua wadogo hawa huko madongo kuinama kiasi cha kufanya iwe habari ya kuripotiwa popote? Hii ikizingatiwa pia kuwa, hata kwa hao wakubwa juhudi za kudunisha matukio yao zimekuwa kubwa kwa kiasi tunachokiona?
Hebu basi hata tuweke japo sababu za vifo pembeni. Hata kujiuliza tu, hivi hii kasi ya vifo ni sawa sawa pia hamna?
Tumekuwa kama tuliopigwa upofu. Tunetekwa na shetani. Tumekuwa mawakala kamili na waaminifu wa shetani. Hatuoni wala hatusikii hadi pale mmoja mmoja litakapomfika peke yake mlangoni?
Nakumbuka kale kawimbo:
"nyoka huyo, nyoka huyo" (kibwagizo)
"Mwache apite" (kiitikio)
"nyoka huyo, nyoka huyo" (kibwagizo)
"Mwache apite" (kiitikio)
Hadi wote wanaangamia na nyoka wakiwa wakiitik ia acha apite.
Matukio ni mengi sana lakini ajabu ya Mussa pana kaupepo kengine siku za hivi karibuni ka kuona mtu au watu kufa ni jambo la kawaida. Hakuna kujali wala kufuatilia. Eti kuwa hata zamani watu walikuwa wanakufa.
Walikuwa wanakufa hivi?
Dalili kamili za kumtumikia shetani.
Enyi mnaodunisha vifo vya wengine ni vyema mkajitathimni:
"you could be in possession of the devil. Faithful agents of the devil himself".
Badilikeni jamani mnatia kinyaa.
Wanatakakutupeleka kwenye Chip ili maandiko ya 666 yatimie