Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Unamaanisha nini ukisema kuzaa watoto ni baraka?
 
Uongo mtupu, familia kubwa sio lazima iwe kwa kuzaa.
 
coach, maneno ya mwenye kushiba hayo!! mtoto ana raha yake asikwambie mtu; isitoshe kuna wimbi la wazazi wasiotaka au kupenda watoto wao kulelewa na mabibi siku hizi......ungelipata tabu na majuto.
Mtoto ana raha yake sawa mkuu lakini ndio wazaliwe kwa utaratibu maalum
 
Mtoto ana raha yake sawa mkuu lakini ndio wazaliwe kwa utaratibu maalum
Nasubiri jibu
Niambie kutokuwa sahihi kunatokana na Nini? Nipe sababu za kisayansi na kijamii.usione aibu kuzitaja kinagaubaga.
Maybe hata Mimi sizijui ndiyo maana. Nimeshikilia msimamo wangu
 
Vijiji vingi watu wengi bado wana njaa pia, watoto wanaishia kuteseka tu.Na huduma kwa watoto sio chakula tu.
Huku kwetu vijijini tuna uwezo huo, chakula tele mashamba na hata nguvu pendwa uhakika... huko mjini dhiki nyingi chumba kimoja cha kupanga unadhani wote tunaishi hivyo?
 
Kwa hiyo kwa sababu wewe ni muafrika ndio uzae kama sungura? Akili za wapi hizi!
 
Ishu sio kuzaa,ni wachache sana ambao hawawezi kuzaa,tatizo ni kutunza hao watoto.
Haya mambo kama wewe huwezi, Basi nyamaza waachie wanaoona wanaweza....


Tusipangiane namna ya kuzaliana....
 
Acha uoga mkuu...
Sheria yoyota iliyotofauti na nature ni batili!
Kama suala ni nature mbona kaka na dada wa tumbo moja hawaoani kama wafanyavyo wanyama wengine kama ng'ombe na mbuzi?
 
Kama suala ni nature mbona kaka na dada wa tumbo moja hawaoani kama wafanyavyo wanyama wengine kama ng'ombe na mbuzi?
Hapo Kuna sababu za kisayansi ambazo zinajulikana kabisa ( inbreeding effects) ndiyo maana hairuhusiwi

Wewe nipe sababu za kisayansi na kijamii za kupinga hicho unachokipinga
 
Zaeni mkaijaze nchi...
Km unaweza kufikiri kuwa watoto wawili wataweza kufanya uwe na furaha,
Sasa kwann umuogope anaepata furaha yake kwa kuwa na watoto wengi?
Tuwajal watoto.
Tuendelee kuzaana kwa staha
 
Yameshajadiliwa sasa,lamba ndimu au chumvi
Nosense., Haya mambo si ya kujadili na yaonekana wazi ata dini huna, na unafkiri kila kitu ulimwenguni kinaendeshwa ni mawazo binafsi ya mwanadamu, na ndio mana sasa ukijisikia unakuja hapa jf na kuandika tu chochote.
 
Mke wako amekukubalia kukuzalia kama sungura?
Hizi kauli za kikoloni ziacheni huko, mnatawaliwa mpaka mnashindwa kufanya maamuzi yenu binafsi, kwani mke wangu kubeba ujauzito hata kama binti yake yake naye ana ujauzito shida nini?...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…