Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Unamaanisha nini ukisema kuzaa watoto ni baraka?
Brother hili swala hutakiwi kugeneralize, siyo kila mtu hana uwezo wa kulea watoto zaidi ya watatu hadi Saba. Kinachotakiwa ni mtu kufanya tathmini ya hali yake kiuchumi kabla hajachukua maamuzi ya kuongeza idadi ya watoto na pia kuzingatia ushauri wa Afya kuhusu child spacing.

Kuzaa watoto ni baraka Kama una wezo wa kuwalea na kuwapatia mahitaji yao jinsi inavyotakiwa. Kwa hiyo hakuna limit kwamba mtu anatakiwa aishie kuzaa watoto watatu ndo aonekane kuwa anafuata uzazi wa mpango.
 
Uongo mtupu, familia kubwa sio lazima iwe kwa kuzaa.
sasa ujinga gani, hujui familia kubwa ni faraja.
familia ikiwa ndogo sana misiba ikitokea huwa inachoma sana kwa maana mpo wachache, mkiwa wengi kuna amani na faraja fulani hivi

hivyo tatizo sio big family ni uwezo tu wa kulea, kama mtu ana uwezo azae tu, kama kina kardashian, ni wazungu ila familia ni kuubwa hadi inafurahisha ile ni faraja kubwa sana.
 
coach, maneno ya mwenye kushiba hayo!! mtoto ana raha yake asikwambie mtu; isitoshe kuna wimbi la wazazi wasiotaka au kupenda watoto wao kulelewa na mabibi siku hizi......ungelipata tabu na majuto.
Mtoto ana raha yake sawa mkuu lakini ndio wazaliwe kwa utaratibu maalum
 
Mtoto ana raha yake sawa mkuu lakini ndio wazaliwe kwa utaratibu maalum
Nasubiri jibu
Niambie kutokuwa sahihi kunatokana na Nini? Nipe sababu za kisayansi na kijamii.usione aibu kuzitaja kinagaubaga.
Maybe hata Mimi sizijui ndiyo maana. Nimeshikilia msimamo wangu
 
Vijiji vingi watu wengi bado wana njaa pia, watoto wanaishia kuteseka tu.Na huduma kwa watoto sio chakula tu.
Huku kwetu vijijini tuna uwezo huo, chakula tele mashamba na hata nguvu pendwa uhakika... huko mjini dhiki nyingi chumba kimoja cha kupanga unadhani wote tunaishi hivyo?
 
Kwa hiyo kwa sababu wewe ni muafrika ndio uzae kama sungura? Akili za wapi hizi!
mwafrika mimi hata usiniletee habari hizo:

kama mama bado anayo mayai na yupo katika umri salama wa kuzaa na ninahitaji mtoto; anazalishwa mara moja.

kama mama ana miaka 35 na binti yake wa kwanza na pekee mwenye miaka 18 aliyempata akiwa na miaka 17 naye ni mjamzito.....wala sisiti kumpachika mimba kwa sababu hiyo. utakuwa ni ujinga kuacha kuijaza dunia kwa vijisababu ambavyo ni maoni 'opinion' tu za watu na sio 'fact'.

kwangu kipaumbele ni; je, tunahitaji mtoto? je, ni salama kwa mama kujifungua sasa? basi!

mkuu Jurjana, tujuze suala hili katika msimamo wa kidini tafadhali!!!
 
Ishu sio kuzaa,ni wachache sana ambao hawawezi kuzaa,tatizo ni kutunza hao watoto.
Haya mambo kama wewe huwezi, Basi nyamaza waachie wanaoona wanaweza....


Tusipangiane namna ya kuzaliana....
 
Acha uoga mkuu...
Sheria yoyota iliyotofauti na nature ni batili!
Kama suala ni nature mbona kaka na dada wa tumbo moja hawaoani kama wafanyavyo wanyama wengine kama ng'ombe na mbuzi?
 
Kama suala ni nature mbona kaka na dada wa tumbo moja hawaoani kama wafanyavyo wanyama wengine kama ng'ombe na mbuzi?
Hapo Kuna sababu za kisayansi ambazo zinajulikana kabisa ( inbreeding effects) ndiyo maana hairuhusiwi

Wewe nipe sababu za kisayansi na kijamii za kupinga hicho unachokipinga
 
Zaeni mkaijaze nchi...
Km unaweza kufikiri kuwa watoto wawili wataweza kufanya uwe na furaha,
Sasa kwann umuogope anaepata furaha yake kwa kuwa na watoto wengi?
Tuwajal watoto.
Tuendelee kuzaana kwa staha
 
Yameshajadiliwa sasa,lamba ndimu au chumvi
Nosense., Haya mambo si ya kujadili na yaonekana wazi ata dini huna, na unafkiri kila kitu ulimwenguni kinaendeshwa ni mawazo binafsi ya mwanadamu, na ndio mana sasa ukijisikia unakuja hapa jf na kuandika tu chochote.
 
Mke wako amekukubalia kukuzalia kama sungura?
Hizi kauli za kikoloni ziacheni huko, mnatawaliwa mpaka mnashindwa kufanya maamuzi yenu binafsi, kwani mke wangu kubeba ujauzito hata kama binti yake yake naye ana ujauzito shida nini?...
 
Back
Top Bottom