Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Wewe kamanda mwenzangu huoni umuhimu wa hili daraja? Ulishakuta foleni ya magari kama feri imeharibika? Kamanda unatia aibu sana. Unakiabisha chama chetu.
 
Umeni pre empty. Kuna wakati unaweza kukaa hapo kivukoni zaidi ya saa 6 unasubiri kuvuka. Wagonjwa kutoka Chato, Biharamulo, Geita, nk wanakimbizwa na Ambulance kwenda Bugando referal hospital .Ningemuelewa kama labda angesema wangeongeza ukubwa wa gati na kuongeza idada ya vivuko kutoka viwili vya sasa hadi kumi.
 
G Sam,

Kwa hiyo wewe hupendi hilo daraja kujengwa au hiyo hela iliyotumika? Ungejua muda unaotumika kusubiri hizo pantoni usingesema hayo hasa siku ukute ipo moja. Mtu unaandika tuu sisi tunaopita ndio tunajua tabu ya hapo. Nyie kila kitu kupinga tuu sijui mkoje.
 
Ni kutupa fedha za maskini baharini. Bilioni 700 tungejenga barabara kilometer 700 kanda ya ziwa ingeunganishwa wilaya zote kwa barabara safi ya lami.
Matatizo ya shule ndogo kichwani; Uelewa mdogo! Hizo barabara zina umuhimu wa kiuchumi? Mbona muli support bandari ya Bagamoyo.
 

Sawa kwa huu utetezi wako, hebu tuambie hayo madaraja yalikuwa ya bei gani hizo sehemu ulizotaja? Tufanye hivi, ingetolewa 20-50b ikajegwa hospitali, 100b kivuko, kisha 50b vikajengwa viwanda kadhaa. Halafu 350b+ ikaelekezwa sehemu nyingine huoni ingekuwa jambo la maana, zaidi ya hilo pambo kwa sehemu yenye tija ndogo?
 
Matatizo ya shule ndogo kichwani; Uelewa mdogo! Hizo barabara zina umuhimu wa kiuchumi? Mbona muli support bandari ya Bagamoyo.

Uza ubongo huo dogo, bandari ya bagamoyo ilikuwa inajengwa na fedha za ndani? Watu mlioajiriwa huwa mna akili fupi sana.
 

Hilo eneo lote ni wagonjwa wafupi mpaka daraja la 70b lijengwe kwa ajili ya wagonjwa? Si wangejenga hospitali ya 100b, kisha hizo 600b wakajenga viwanda maeneo hayo watu wapate ajira?
 
Wewe naona huna unachjua katika nchi yoyote.
Hilo eneo lote ni wagonjwa wafupi mpaka daraja la 70b lijengwe kwa ajili ya wagonjwa? Si wangejenga hospitali ya 100b, kisha hizo 600b wakajenga viwanda maeneo hayo watu wapate ajira?
Wewe unayo hoja hebu tuambie kingejengwa kiwanda cha kutengeneza nini.
 
Wewe hoja unayo sema umeshindwa kuielezea napenda watu kama wewe,lakini daraja hilo likijengwa wenye magari watalipia hivyo yatakuwa ni Yale Yale japo ushauri wako ungechanganua kwa sababu kiwanda ni kweli kinazalisha ajila lakini uendeshaji wa kiwanda ni jambo lingine kabisa ndio maana kuna watu wanafanya kazi serikalini anaweza kopa zaidi ya m10 lakini akianzishia biashara inamshinda na hela imeenda, anaona bora akope akajenge nyumba ambayo haifilisiki wala haina hali mbaya,

akini kiwanda vina changamoto nyingi masoko,uendeshaji, migomo, hasara vipuli na mambo mengi ambayo ni ngumu kuyaelezea lakini daraja unalijenga Leo miaka 100 linaendelea kuwepo na kufaidisha umma mambo mengine ni kuchagua tu ndio maana China ilijenga ukuta mkubwa miaka mingi iliyopita lakini mpaka Leo unaingiza pesa,wamejenga mabwawa ya umeme makubwa kuliko yoyote duniani MG100000 kwa pesa nyingi ambazo zingeanzisha viwanda kila kona ya China pia wamejenga daraja la vioo kwa ajili ya utalii nalo limetumia pesa nyingi,

amejenga treni ya chini ya ardhi na juu yote hayo ni mapesa ambayo wangewekeza kwenye viwanda wangekuwa na viwanda kila uchochoro jambo LA muhimu ni kuona miundombinu wezeshi kwa miaka 100 ijayo viwanda tuwaachie sekta binafsi ambao wanamudu kutokana na uchungu wa uwekezaji.
 
Mkuu halijengwi Kananga Bali busisi ferry
 
Ni dakika 10 hadi 15. Labda sema logistics za kusubiri ferry na kuabiri hizo ferry. Ukitafakari kwa kina, daraja hilo lina umuhimu.
 
Kama ishu ni hospital fikiria hiyo hela zingejengwa hospital ngapi za maana katika hilo eneo na maeneo mengine?
 
Unaweza ukawa uko sahihi kwa upande wako lakini kwa wengine sio sahihi: (1)fly over ni kilio cha muda mrefu kwa watu wa dar ilifika mahali MTU analazimika kuacha gari nyumbani anaenda kwa boda, (2)kuamia Dodoma kiserikali kuna maana sana kuliko unavyodhania wewe na pia kuna faida ya wakazi wa Dodoma kuongeza thamani ya ardhi yao na kupata mzunguko wa fedha,kukuza mji,kuongeza mapato ya almashauri sasa hapo hakuna faida. (3),bwawa la umeme mbona jambo hili liko wazi, (4)reli inapunguza gharama ya usafirishaji ukinunua ciment iliyosafiri kwa treni ni tofauti na iliyosafirishw kwenye roli omba mungu miladi ihishe utaona faida take.
 
Hili ndilo tatizo la ukomo wa mipaka kwenye uelewa, hivi ulishawahi kuvukia kamanga ama busisi? Ukaona kadhia yake? Chadema ya mwaka imefifia hadi kwa wapiga kura wao.
 
Wewe naona huna unachjua katika nchi yoyote

Wewe unayo hoja hebu tuambie kingejengwa kiwanda cha kutengeneza nini.

Vifaa mbalimbali vya plastiki kama mabeseni, ndoo, pipes za maji safi na majitaka. Pia viwanda vya maziwa na ngozi kwani huko kanda ya ziwa ni sehemu ya wafugaji. Unataka nikuongezee matumizi sahihi mengine ya 700b?
 
Vifaa mbalimbali vya plastiki kama mabeseni, ndoo, pipes za maji safi na majitaka. Pia viwanda vya maziwa na ngozi kwani huko kanda ya ziwa ni sehemu ya wafugaji. Unataka nikuongezee matumizi sahihi mengine ya 700b?
Good!alafu kiendeshwe na nani?
 

Ukianzisha kiwanda usimpe mwanaccm kukiendesha, unampa CEO mwenye uwezo hata kutoka nje ya nchi, kama wafanyavyo akina Bakhressa, Mo nk. Fuatilia vizuri viwanda vyote enzi za Nyerere viliuliwa na kamati za chama zilizokuwa ndani ya viwanda. Sio uumpe CEO, halafu umuelekeze kupika data, na kushinda kwenye mbio za mwenge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…