Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

Bado natafuta mantiki ya kujenga hili Daraja la Kigongo - Busisi kwa Tshs. Bilioni 700

G Sam,

Tuna mkuu wa ajabu Sana,unaweza pata picha alipokuwa sengerema ilibidi atoe amri ya kujenga kibarabara ambacho watu Wana shida nacho kuliko hilo daraja,hii ni matumizi mabaya ya pesa na madaraka.

Hata stiglaz ni sawa tu na huu mradi maana utazalusha umeme ambao utakuwa hautumiki kwa vile so far tuna surplus,unaniuliza kwani wangejenga bwawa la mgwt 400 pesa inayobaki ikafanya mengine kungetokea shida gani? Akili za maccm ni tatizo kubwa Sana kwenye nchi hii.

Hayo mahilioni unazungumzia km 750 za lami
 
Good!alafu kiendeshwe na nani?

CEO mwenye uwezo tena kwa kuweka PR yake na apewe kiwango cha mafanikio. Sio kiwanda akabidhiwe mtoto wa kiongozi wa serikali, au mwanaccm anayejipendekeza kwa rais.
 
Mkuu unaandika kwa kudanganya ili kujustify uongo wako.

Labda hauishi maeneo haya ndio maana unaona halina umuhimu.

Kwanza Ferry zimeshazidiwa kuna wakati gari na watu wanasubiria hadi masaa 4 kutokana na foleni iliopo.

Daraja halitakuwa na tozo kama unavyodai.

Daraja hili halipitishi hiace pekee, mabasi na magari ya mizigo ni mengi sana yanzpita hapa.
 
Dawa hapa ni Lissu ili Tiwe na majimbo kila mtu ale usawawakamba hizi hela zinakopwa halafu wakati wa kulipa tunalipa wote nchi nzima
Kama wewe ni mtu uliyezaliwa na kukua sehemu moja mpaka leo, hii comment yako nitaielewa.
 
Mkuu halijengwi Kananga Bali busisi ferry
Ndio lakini sasa gari hazitakuwa zinasubiri kivuko hapa samanga, watakuwa wanaenda kupitia usagara,wanavuka daraja wapo sengerema ndani ya nusu saa, badala ya kumaliza masaa mawili wanangoja ferry ije.
 
G Sam,

Mkuu hata wewe ungepewa kusimamia wala usingelalamika hata kidogo maana mpk mradi unaisha ungekuwa na ghorofa mbili Dar, Dom 1 na Mwz 3.
 
Ubongo wako ushughulishe kidogo hivi wewe na akili zako hujui humuimu wa daraja linalounganisha mkoa mmoja na mkoa mwingine,kwanini lakini chadema mnakuwa nyumbu hivyo ,kabla ya swali lako ungejiuliza umuhimu wa madaraja yafuatayo:nyerere la kigamboni,kikwete la malagarasi,mkapa la rufiji,wami la mto wami na maeneo hayo yote yalikuwa na vivuko kabla ya ujenzi wa madaraja hayo.
Hawa watu wanaotangaza kuwa na bima ya afya huku wanapinga ujenzi wa hospitali na vituo vya afya ni shida sana.
 
Kuna siku nilikua naenda Bukoba, tulikaa masaa 3 kusubiri kivuko, unadhani hiyo ni Sawa!
 
Dawa hapa ni Lissu ili Tiwe na majimbo kila mtu ale usawawakamba hizi hela zinakopwa halafu wakati wa kulipa tunalipa wote nchi nzima
Hii nchi bila kuwa na sera ya majimbo tutaendelea kufanywa wote wajinga,wataoona vipaombele kwao ni ndege na madaraja wafanye maeneo yao, haingii akilini vitu vya msingi kwa ustawi wa watu havifanywi afu mtu anatumia vibaya madaraka kwa matumizi yasiyo na msingi. Lisu alisema katiba inamfanya mtu aitwae rais kuwa alpha na omega ndio Kama hivi sasa.
 
Lissu alipita hapo kigongo ferry akaubeza huo mradi lakini mhe Magufuli aliusifia na kueleza umuhimu wake. Ngoja tuone tar 28 wananchi watatuambia.

Mimi ninavyofahamu hilo eneo kwa siku linapitisha magari na watu wengi sana. Kuvuka kwa kivuko inakula kama dk 30 mpaka 45.
Mkuu watu wengine huwa hawajui wanachokisema, wanaandiika tu, Hapo Busisi watu ni wengi Sana wanaovuka kwa siku, ukifika hapo unaweza kusubiri kivuko kwa zaidi ya dakika 20, kikifika unatumia zaidi ya dakika 35 kuvuka ng'ambo, mtu bado haoni umuhimu wa Hilo daraja.

Mtu anakwambia eti wananchi wa eneo Hilo wana kipato Cha chini et daraja litakuwa mzigo kwao, Unashindwa kuelewa kwamba hilo daraja litakuwa kiunganishi kizuri Kati ya Tanzania na nchi jirani za ukanda huo, na kwamba litaingeza faida za kibiashara.
 
Hili daraja ni muhimu sana kuna network kubwa ya magari, ni muhimu kuliko hata chato airport.
 
Faida zitaonekana mbeleni
Wewe watu Wana suffer unazungumzia habari ya mbeleni, natamani maviongozi yote ya ccm yangefia jela tu huko,ndio maana huwa Kuna wanauchumi kufanya cost benefit analysis, kipi kifanyike sasa na kipi mda wa Kati na kipi Cha baadae ,vyote vinafanywa kwa principal za uchumi sio kwa utaratibu wa ndoto za usiku za mtu mmja.
 
ILA UMESUBIRI MANTIKI YA KUONA MAMIA YA WATANZANIA WANAOISHI MWANZA NA GEITA WAMEZAMA NA KUTEGETEA NA VIVUKO VYA BUSISI NA KAMANGA NA KIGONGO.

HIVI CHADEMA KITU GANI KIMEWAVURUGA??
Kama mnanunuaga vivuko chakavu, vya zamani kwanini msizame?
 
Wajengee hospitality pale walipo, wawe stabilized then ndio wapelekwe bugando. Kusafirisha wagonjwa mahututi ni ushamba. Lisu alipelekwa ubelgiji, je kuna daraja kati ya tz na ubelgiji
[emoji15][emoji15] we jamaa, hicho ulichoandika hapo [emoji867]ndicho ambacho ubongo wako unafikiria[emoji848]?
 
G Sam,

HILO DARAJA LITAUNGANISHA RELI YETU NA NCHI ZA JIRANI RWANDA, BURUNDI NA KONGO DRC.

BADALA YA MALORI YA MIZIGO TOKA NCHI HIZO KUSAFIRI KILOMITA 1200 MPAKA DSM. ZITACHUKULIA MIZIGO YAO TOKA BANDARI KAVU YA FELA SGR.

KITENDO AMBACHO KITAONGEZA MAPATO NA PIA KUWAPUNGUZIA GHARAMA NCHI HIZO.

WEWE MLETA MADA MFU ENDELEA KUFIKIRI KI FARAGHA FARAGHA, WENZIO WANASONGA MBELE.
 
Hata angefanya hivyo, wapo watu wangepinga na kusema Ni maendeleo ya vitu, huenda hata wewe ungekuwa ni mmoja wao.
Haiwezekani kila mtu akawa anajipangia Cha kufanya ndio maana Kuna vipaombele vya kitaifa vinavyoratibiwa na wataalamu wa uchumi baada ya kufanyia utafiti mahitaji ya msingi ya wananchi. Kujenga viwanja ni upuuzi Kama huu tu wa madaraja.

Serikali umejenga vituo vya afya Kama 500 hivi umesikia nani anapinga? Sera ya afya ni kituo cha afya kila kata lakini Kuna zaidi ya kata 2000 hazina vituo vya afya hapo bado zahanati kila Kijiji nk

Hiyo pesa ingetisha vituo vya afya 120 kwa Bei ya serikali ya mln 500,huoni tungeendelea kupunguza tatizo?
 
ILA UMESUBIRI MANTIKI YA KUONA MAMIA YA WATANZANIA WANAOISHI MWANZA NA GEITA WAMEZAMA NA KUTEGETEA NA VIVUKO VYA BUSISI NA KAMANGA NA KIGONGO.

HIVI CHADEMA KITU GANI KIMEWAVURUGA??
Mkuu hakuna namna, tuwavumilie tu hawa [emoji2][emoji2], kuna hoja wanaanzisha mpaka unakosa hata jibu la kuwapa.
 
Back
Top Bottom