Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
- Thread starter
-
- #41
Hapana, walinunua hawakupewa, na watu wanasema bei waliyonunulia iko juu mno. Kulingana na maelezo yao, vilikuwa kwa ajili ya SGR, lakini inaonekana vimeenda reli ya zamanisasa
Sasa Mkuu haya Mabehewa na Vichwa vya Treni si wamekubali wenyewe kwamba ni Used? ama hivi havikununuliwa walipewa?
Mie nadhani badala ya kuongeza wigo wa kodi kuna watu wameamua kuongeza wigo wa ulajiNa inafanyiwa ukarabati mkubwa
Hapana, walinunua hawakupewa, na watu wanasema bei waliyonunulia iko juu mno. Kulingana na maelezo yao, vilikuwa kwa ajili ya SGR, lakini inaonekana vimeenda reli ya zamani
Hapo Mkuu umetukoroganya kidogo. Ni kwamba SGR itakuwa na uwezo wa kutumia treni za umeme na dizeli, lakini reli ya zamani haiwezi kutumia treni za umemeKwani hiyo SGR ndio itatumia umeme au kuna treni ya umeme itakayotumia reli ya SGR?
The power of FAKE ID..!! Unajiandikia tu huku hujui kuwa unayemjibu ni baba yako au yupo sawa nayeMmezoea cheweing gum nyie, wenzenu wa zamani walizoea matobolwa - waulize watu wa Tabora watakuambia utamu wa matobolwa kulinganisha na hizo cheweing gum zenu!
Hee, haya bwana, samahani, huo ulikuwa utani sio matusiThe power of FAKE ID..!! Unajiandikia tu huku hujui kuwa unayemjibu ni baba yako au yupo sawa naye
Shida kubwa tuliyo nayo hatuna mipango ya muda mrefu inayoeleweka na iliyo wazi mfano reli zitakuwaje miaka 50 ijayo, miji itakuwaje, nk.Kuna kila dalili kwamba SGR itakapokamilika bado tutakuwa na reli ya zamani ikitoa huduma. Hapo mwanzo nilifikiri kwamba reli ya zamani itaendelea kutoa huduma kwa matawi ya Tabora - Mpanda, na labda Dar -es Salaam kwenda Tanga, Moshi na Arusha, ambako sijasikia lolote juu ya kuwepo kwa SGR.
Lakini kila habari zinapotolewa, sisikii hili likiwekwa wazi. Ninasikia tu kuhusu SGR sambamba na reli ya zamani, na manunuzi yakifanywa kwa ajili ya reli zote mbili.
Kwa nini tuendelee kuhudumia na kuwekeza kwenye reli zote mbili? Ni kupanua wigo wa huduma katika bei, kwamba SGR iwe kwa mabwana na reli ya zamani watwana?
Ninachelea kwamba uwepo wa SGR utafanya reli ya zamani iendeshwe kwa hasara iwapo tutaendelea kuitumia. Nilidhani labda SGR ikikamilika reli ya zamani itauzwa kama vyuma chakavu.
Labda ni ule uswahili wetu tu wa kiafrika, tunaendelea kutaka kumiliki vitu vya zamani, tunashindwa kuvitupa hata kama tumenunua kitu kipya mbadala
Lakini reli siku zote ni kitu cha muda mrefu, hatutegemei muundo wa reli utabadilika katika miaka 50 ijayo kwamba wote tuende kwenye bullet trains. Kwa hiyo hakuna baya juu ya hili la SGR kuwa mpango wa muda mrefu, ila ni huu mkoroganyo kidogo wa mabehewa na SGR Vs reli ya zamaniShida kubwa tuliyo nayo hatuna mipango ya muda mrefu inayoeleweka na iliyo wazi mfano reli zitakuwaje miaka 50 ijayo, miji itakuwaje, nk.
Kwa hiyo mambo yanafanyika kuendana na utashi wa kiongozi aliepo. Ndio maana tunashukuru rais kufanya hili na lile - inakuwa kama hisani badala ya jukumu la kutekeleza mipango iliyo wazi na inayoeleweka. Na kwa hili ilani ya chama sioni kama itakupa jibu, haina maelezo yanayoeleweka na mipango ya muda mrefu....
Tukitazama nchi kama Afrika ya kusini, India, na Brazil n.k nao pia walikuwa na na hii hii MGR na hawakuitelekeza waliendelea nayo kwa sababu ilisupport reli mpya zao.Sasa kama reli iliyopo ni nzima inafanya kazi, ni cheaper ku-operate, kwa nini tukaamua kujenga SGR kwa mabilioni ya fedha badala ya kuimarisha hiyo iliyo nzima?
Najua ndivyo wengi wanafikiri, lakini amini nakuambia, usidhani ukiwaleta Chadema au ACT sijui basi hiyo ndio dawa ya maendeleo. Binadamu ni wale wale, wawe CCM, Chadema au ACT hata TLP. Niambie ni nchi gani duniani imepiga hata kubwa ya maendeleo kwa kuwa tu walibadilisha chama tawala. Zambia? Kenya? USA? Uingereza? Brazil? Malawi?Nchi mpaka huu mfumo wa kijani
Ukitoka labda mambo yanaweza kaa
Sawa
Ova
Mkuu, hebu labda utufahamishe nini hasa faida ya kuwa na hizo reli zenye ukubwa tofauti, kama unavyosema India. Inawasaidia nini kuwa na reli SGR 1435 na hiyo ya 1676?Tukitazama nchi kama Afrika ya kusini, India, na Brazil n.k nao pia walikuwa na na hii hii MGR na hawakuitelekeza waliendelea nayo kwa sababu ilisupport reli mpya zao.
India wakaenda mbali zaidi kujenga hadi Broad gauge ambayo ni kubwa zaidi kwa hiyo ya SGR (1435mm) ambayo ni 1676mm, kwahiyo wanayo meter gauge (1000mm), standard gauge (1435mm) pia hiyo Broad gauge (1676mm) na zinapiga kazi.
Inatakiwa uwe mpango wa muda mrefu, ila hawana ndio maana hatuelewi...kwa nini reli ya kaskazini isiendelezwe wakati kuna abiria na mrundikano wa malori ya mizigo namanga? Sasa akiibuka rais flani anaweza kusema napo pajengwe SGR!! Haya yanatakiwa kuwepo kwenye mipango ya muda mrefu inayoeleweka!!!Lakini reli siku zote ni kitu cha muda mrefu, hatutegemei muundo wa reli utabadilika katika miaka 50 ijayo kwamba wote tuende kwenye bullet trains. Kwa hiyo hakuna baya juu ya hili la SGR kuwa mpango wa muda mrefu, ila ni huu mkoroganyo kidogo wa mabehewa na SGR Vs reli ya zamani
Mkuu, jambo jingine nikukumbushe, reli haipaswi kujengwa hata siku moja kwa lengo la kuhudumia abiria. Abiria ni sehemu ndogo sana ya mapato ya reli na inapaswa kuwa huduma tu, ambayo mara nyingi inabidi iwe subsidized na mapato ya huduma ya mizigo. Hatuna uchumi wa kupeleka SGR kaskazini kwa ajili ya abiria kama factor kubwa.Inatakiwa uwe mpango wa muda mrefu, ila hawana ndio maana hatuelewi...kwa nini reli ya kaskazini isiendelezwe wakati kuna abiria na mrundikano wa malori ya mizigo namanga? Sasa akiibuka rais flani anaweza kusema napo pajengwe SGR!! Haya yanatakiwa kuwepo kwenye mipango ya muda mrefu inayoeleweka!!!
Kwa hiyo sgr imeanza na hujaona mabehewa ya zamani!?Hata mie ndivyo nilivyoelewa mwanzoni; SGR ingeanza na mabehewa ya zamani, kulingana na Samia. Lakini sasa naona mabehewa ya zamani ni ya reli ya zamani, kitu ambacho naona ni kama jambo jipya
Something is not adding up na hakuna aliye jasiri kusema ukweli
SGR imeanza? Mie sijui kwa kweli. Ila najua Samia alisema SGR itaanza na mabehewa ya zamani kabla ya mapya kukamilishwa kutengenezwa. kitu ambacho nimesema hapo juu was bad planning. Plan ilitakiwa by the time unamaliza SGR kwa ajili ya kuanza operation order ya kwanza ya mabehewa iwe tayari imekamilishwa. Tunaita synchronization in project implementationKwa hiyo sgr imeanza na hujaona mabehewa ya zamani!?
Hela ya kununua mapya' unayo!?SGR imeanza? Mie sijui kwa kweli. Ila najua Samia alisema SGR itaanza na mabehewa ya zamani kabla ya mapya kukamilishwa kutengenezwa. kitu ambacho nimesema hapo juu was bad planning. Plan ilitakiwa by the time unamaliza SGR kwa ajili ya kuanza operation order ya kwanza ya mabehewa iwe tayari imekamilishwa. Tunaita synchronization in project implementation
Aaah bwana, huko unaenda gizani na unaturudisha nyuma. Tangu mwanzo order ilitolewa kuagiza mabehewa mapya na ya zamani, hilo halina ubishi. Kuna wakati tatizo lilikuwa kuona kwamba design ya mabehewa yaliyosemwa ni mapya ni ya kizamani, na ikafafanuliwa kuwa ni kweli ni ya kizamani kwa sababu sio mapya. Mabehewa mapya mengi yanakuja kama train set, sio behewa moja moja.Hela ya kununua mapya' unayo!?
Wamesema tutaanzia makuukuu,shida nini!?Aaah bwana, huko unaenda gizani na unaturudisha nyuma. Tangu mwanzo order ilitolewa kuagiza mabehewa mapya na ya zamani, hilo halina ubishi. Kuna wakati tatizo lilikuwa kuona kwamba design ya mabehewa yaliyosemwa ni mapya ni ya kizamani, na ikafafanuliwa kuwa ni kweli ni ya kizamani kwa sababu sio mapya. Mabehewa mapya mengi yanakuja kama train set, sio behewa moja moja.