Bado sijaona mbadala wa Scandinavian katika usafiri wa Mabasi. Nauli ilitofautiana kwa aina ya SCANIA

Mi najua hali ya kawaida safari ya kuanzia km 500+ kuchoka ni Hali ya kawaida bila kujali upo kwenye luxury au mkweche. Sasa wewe umepanda kampuni zote za mabasi hapa Tanzania?
 
Na haitakuja kutokea kamwe, sijapata kuona aina ile ya coordination ya safari nadhani ni ya pili kwa ubora baada ya EAR enzi hizo
 
Mi najua hali ya kawaida safari ya kuanzia km 500+ kuchoka ni Hali ya kawaida bila kujali upo kwenye luxury au mkweche. Sasa wewe umepanda kampuni zote za mabasi hapa Tanzania?
Zile ulizozitaja zoote nimezipanda shabiby ni loyal customer wao wa basi la mwisho kutoka Dar to Dom hivyo najua alipopungukiwa kumfikia scand, Darlux kabla ya hizi zilizomshinda akamuuzia klm alikuwa na zile polo original mbili(2) nazo nilizipanda japo kwa ule upungufu wao wa kuvuja kipindi cha mvua miaka hiyo akiwa na route ya Dar Mwanza. Hao abc ni uchafu usiomfikia hata shabiby
Hivyo ninapokubali ubora wa scand dhidi ya hao uliowataja na wengine ambao umewaruka, sio kwa sababu za kisiasa aka mihemuko ni kwa sababu ya kile alichokuwa anatupatia bila yeye kutuchoka hata tukiwa on board kwa masaa ishirini na zaidi
Sio jambo rahisi kwa hawa wasafirishaji wa leo mteja afanye booking ya mwezi mmoja mbele akubaliwe na siku ya safari akute nafasi ile aliyoomba bila kuletewa sarakasi ila kwa scand ilikuwa inawezekana
 
Kabisa
 
Sio mbaya kushare experience Shabiby kapungukiwa Nini kilinganisha na Scandinavia? Kampuni Gani ulienda kubook mwezi Mmoja kabla wakakataa? Na Kwa Nini walikataa usifanye booking?

Toka kuanzishwa Kwa Scandinavia mpaka Kufa kwake hazikuwahi kupata hitilafu njiani?

Mmeimiss Scandinavia hata Mimi nimeikumbuka
 
Alitengeneza reputation yake nzuri ila msipate upofu Bado Kuna kampuni zinatoa service nzuri za mabasi kushinda hizo gari mseme mmezimiss hizo basi tu.
Kipindi hicho hakukuwa na mabasi mengi yenye ubora hivyo kuyafanya mabasi ya Scandinavian yaonekane kama ni kitu cha ajabu sana. Ni pia huduma za mabasi enzi hizo zilikuwa ni za kuringa na kufokea wateja lakini wao walikuwa wanatoa huduma nzuri. Kwa kifupi ni yalikuwa mabasi ya kawaida sana ila kampuni shindani zilikuwa za hovyo.
 
Hivi mabasi ya Bongo huwa wana wazimu? Hili la kuharakisha abiria kama msukule mimi huwa linaniacha hoi. Kuanzia kupakia, kushusha na kula chakula kila kitu ni amri na haraka kama mko jeshini!
 
Huduma siyo tu kuweka kondakta wa kike bwashee

Hayo mabasi uliyoitaja mpandishe mtoto uone kama hajapitilizwa kituo kwa haraka zao
Si bora hata kondakta wa kiume. Nilipanda gari moja inajitangaza ni luxury, kuna mhudumu wa kike anagawa soda na karanga lakini anatia kichefuchefu kweli kweli. Anazoea watu hovyo, anadhani kila mtu anataka kumtongoza, yaani ni kero kubwa!
 
Sio mbaya kushare experience Shabiby kapungukiwa Nini kilinganisha na Scandinavia? Kampuni Gani ulienda kubook mwezi Mmoja kabla wakakataa? Na Kwa Nini walikataa usifanye booking?

Toka kuanzishwa Kwa Scandinavia mpaka Ku
Nimewahi kata tiketi kwenye shabiby mara mbili hivi. Na nilikuwa napandia bus vituo vitatu mbele toka stand na mara zote nilifika kwenye gari nakuta siti yangu imekaliwa na mtu afu nae ana tiketi kama yangu dadeki,

Hao ABC tulimpakia dogo wamshushe mlandizi tena kwa kuwasisitiza sana na kuwapigia simu mara kwa mara wakiwa njiani, lakini bado walikuja kushtukia wamefika nae mbezi na bahati mbaya dogo alisinzia
 
Hivi mabasi ya Bongo huwa wana wazimu? Hili la kuharakisha abiria kama msukule mimi huwa linaniacha hoi. Kuanzia kupakia, kushusha na kula chakula kila kitu ni amri na haraka kama mko jeshini!
And as usual hatuna uwezo wa kuwaambia, ndio maana Scandinavian Express standards zao hakuna hata kampuni moja iliyofikia even 45%,na tuelewe kuna madereva they're driving fast Sina tatizo na hawa ila wanaoendesha reckless hawa ni cold blooded killers
 
Hivi kampuni ya OTAWA ya pale songea ilishakufaga. nje ya mada.
 
Sio mbaya kushare experience Shabiby kapungukiwa Nini kilinganisha na Scandinavia? Kampuni Gani ulienda kubook mwezi Mmoja kabla wakakataa? Na Kwa Nini walikataa usifanye booking?

Toka kuanzishwa Kwa Scandinavia mpaka Ku
Miongoni mwa kampuni za mwanzo mwanzo kukata tiketi online alikuwa Dar lux, 2019 kwa shauku kubwa kwa ajili ya kupanda zile basi zao za luxury nikajisogeza pale kwenye ofisi yao ya mianzini Arusha, wakashindwa kuweka booking ya wiki mbili mbele sembuse ningewaomba ya mwezi!!!
Hao Shabiby labda mapenzi yako yapo kwao lkn wanamatatizo kuzidi,
 
Zilikuwepo basi zenye choo na viti vya sofa na ac. sema ulikuwa hauendi njia hizo za Mbeya.
 
Zipo basi zenye vyoo na makochi pia ac na chaja za simu pia chai au kahawa ukitaka.
 
Zilikuwepo basi zenye choo na viti vya sofa na ac. sema ulikuwa hauendi njia hizo za Mbeya.
Kulikuwa Na mabasi yanaitwa Royal yalikuwa yaki compete Scandnavian pia yalikuwepo baadhi dar express.

Marcopolo ndio ilikuwa Brand ya mabasi Luxury.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…