Bahati iliyoje Ukraine firm kununua ndizi zote za Tanzania

Soma tu kwenye hiyo source mkuu,

Tuendelee kumwombea Mama Samia

Mambo yatakuwa mazuri kwelikweli
😍😍😍😍
 
Utakuwa unakaa mitaa ya burundi siyo Tanzania bwashee.

Huku tanzania mambo ni bambam. Pesa imejaa mitaani. Sisi watz tunakula bata tu. Sasa hivi ni kazi na bata kwa uhuru. Furaha imerejea.
😍😍😍😍 Sio Mtanzania huyu
 
Kuna kipindi tuliaminishwa kwamba Wachina wanataka kununua mihogo yote Tanzania - hadi wa leo hakuna cha mchina wala muhogo wetu uliyovuka bahari ya hindi.

kwa hiyo watanzania msiwe wepesi wa kushangilia kila jambo.
Wachina wasanii sana wallahi
 
😍😍😍😍 Hatari sana,
 
Wenzio yamewakuta sasa!!
hao wanakuvuta unaenda...ukishaenda unajazwaaa mwisho ndiyo unaliwa!!
Wanajua vema wanawake wanaamini kirahisi.
Mahubiri yakweli hayahitaji mambwembwe meeengi mf. msikilize mwakasege... Nipoint tuu hamna ujanjaujanja
Acha kukufuru roho mtakatifu mkuu,

Achana na mambo ya imani za watu
 
Mimi kinacho nishangaza kuhusu Taifa letu,hivi inakuwaje Kenya imeweza kuteka soko la uuzaji ndizi nchi za nje kwa kuuza ndizi wanazo nunua kwa wingi Tanzania, si ndizi tu hata vitunguu,citrus fruits na parachichi wana nunua Tanzania wanazi- repack na kuviuza Ulaya na Merikani wanaweka nembo za Kenya!!

Yaani Tanzania inageuzwa shamba la bibi, hata Wizara zinazo husika hazina mpago mahususi wa ku-reverse trend hii ya Wafanya biashara wa Kenya kuichukulia Tanzania kama mtambo wa kuwanufaisha wao na Taifa lao - enough is enough kama Tanzania inashindwa kutafuta masoko nje ya nchi basi Wizara husika zifanyiwe marekebisho ya haraka kiutendaji au wahusika watembelee mataifa kama Kenya ,Israel na Afrika Kusini ili wajifunze wenzao walitumia mbinu gani kuteka masoko nchi za nje, kama hamuwezi ya nini kuanzisha Wizara ambazo hazina ubunifu wowote wa kibi hashara - yaani tunabaki tunachekwa tu na majirani zetu kutokana na uzubaifu wetu husio wa kawaida.
 


Mkuu Prof Mkenda na Bashe ni vichwa kwelikweli chini ya Rais Samia Suluhu Hassan,

Hii hatua yakwanza ni nzuri sana,

Ngoja tuone baada ya hili nini kitafuata,

But all in all Rais anafanya kazi nzuri sana
 
good intention can move mountains, sio kama chadema ni vurugu tu, kulumbana wenyewe kwa wenyewe, lazima MWENYEZI MUNGU AWAPIGE CHINI TU KILA SIKU
Unamuhusishaje Mungu na ushetani wenu wa CCM!!?!
 

Ni jambo jema, itawasaidia sana wakulima wengi.

Umekosea, hawajawekeza $29bn in Uganda wanachosema jumla la Soko / biashara yote ya ndizi Uganda ni $29bn.
 

Kenya wametupita sana. Kwa ubunifu, kutafuta masoko kwa bidhaa zao, wakulima, kuchangamkia fursa, wao, kubrand nchi yao, kuweka mazingira rafiki kwa watu wao wawekekezaji na kutoa vibali fasta (export license).

Serikali yao is proactive inajaribu kuboresha na kumsaidia mkulima wao kadri inavyowezekana, hapa bado urasimu, kodi lukuki, mazingira mabovu kwa wakulima.

Unaondoa ruzuku kwenye mbolea maana yake unaongeza gharama kwa wakulima.

Ingekuwa vizuri kuvutia wawekezaji kuanzisha viwanda vya mbolea hapa Tanzania kabla ya kuondoa ruzuku.

Wazungu wengi bado wanajua Kilimanjaro ipo Kenya na Tanzanite zinatoka kenya.

Matunda kibao yanaoza Tanga. Bado tunasafari ndefu kujua vipaumbele vyetu vitakavyowasaidia wengi, kuongeza pato la wananchi, mapato kwa serikali na kupunguza matatizo ya ajira, Umachinga.
 
😍
👍🙏😍👊

SIEMPRE CHIFU HANGAYA ,amen🤲
 
Hivi kweli Ndizi zitapatikana kila mwezi kama mnunuzi anavyotaka?
Kama sio za msimu basi tumeula maana kila mwezi tunatuma tu zinaota zingine kwa mwezi tunatuma tena
 
Mkuu Prof Mkenda na Bashe ni vichwa kwelikweli.
Hawa wako vizuri, ila kasi ni bado ndogo sana ya uwekezaji wa ukweli kwenye kilimo. Futa ushuru kwenye vifaa vya irrigation, tuvutie kampuni kubwa kufungua viwanda vya kutengeneza mbolea, Tractors, mbegu bora kwa gharama nafuu.

Export license zitolewe kwa wakati bila urasimu na rushwa, serikali, balozi,taasisi na wizara husika zifanye kazi pamoja kuondoa changamoto/ vikwazo pamoja na kutafuta masoko makubwa na kushiriki maonyesho mbalimbali (Expo Exhibition) top Supermarkets, top food distributors and buyers na wadau wengine wakubwa around the world kutangaza bidhaa zetu.

Wenzetu wsna export Maua, mbogamboga, Chai, kahawa, matunda kwa wingi.

By the way nimeona juzi Kenya wamewatafutia Nurses na Doctors zaidi ya elfu 20,000 wasio na waliokosa na ajira Kenya, kwenda kufanya kazi UK.

In return UK itailipa serikali ya Kenya kiasi kadhaa na kuwekeza zaidi kwenye vyuo na sekta ya afya kenya. Majirani wamechangamka kuliko sisi.

 
Huu ni ujinga, maswala ya mendeleo tayari mmeisha ingiza siasa! Kwa hiyo Uganda wanaouza ndizi zaidi, M7 atawale milele?
 
Haya ndio mawazo ya kushare sio matusi na kejili,
Nimepata kitu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…