Stupidity,
SGR km 1,000 unajenga wewe?
SG Rufiji unajenga wewe?
Barabara kila kona unajenga wewe,
Mishahara watumishi unalipa wewe?
Ndege unanunua wewe?
Chanjo unaagiza wewe?
Meli unanunua wewe?
Elimu bure unatoa wewe,
Madarasa elfu 15 unajenga wewe?
Vituo vya afya 220 unajenga wewe?
Viwanja vya kimataifa ikiwemo Msalato unajenga wewe,
Bil 500 Za HESLB unatoa wewe?
Ajira elfu 56 unaajiri wewe?
Acha ukichaa tumia akili vizuri
Umepaniki ndugu, pole pole.
Ungependa tuzungumzie miradi ipi labda, ya kipindi cha kwanza cha awamu ya tano au kipindi cha pili cha awamu ya tano?
Hiyo miradi yote uliyoorodhesha, ainisha upi umeanza baada ya March 2021 na ipi ilikuwepo!
Hayo mengine kama kuna hata moja ni tangible mpaka sasa, ukiacha kulipa mishahara, njoo na mifano hai.
Madarasa yanayojengwa, 15,000 yanajengwa wapi? Ujenzi umeanza lini?
Barabara kila kona, ni kona gani hizo? Kuna mikoa ina barabara moja tu ya lami ya maana, Dar peke yake hakuna hizo barabara kila kona.
Mpaka sasa kuna ajira ngapi mpya zimetolewa ukiacha hizo za kuziba mapengo yaliyokuwepo kutokana na kustaafu, vifo, magonjwa, kuacha kazi, kutumbuliwa kwa vyeti feki n.k?
Chanjo mmekopa, ndege zimenunuliwa, tumeziona, HESLB si kweli, kuna madogo wengi hawana mikopo, hizo pesa mmewapa wakina January?
Vituo hivyo vya afya vinajengwa wapi? Ujenzi unaanza lini?
Airports, Meli, Bwawa ni vitu vilivyo kwenye utekelezaji tu, kama mtashindwa kuviendeleza kama mlivyotelekeza Stendi, barabara ya moro na moroco, mje mtupe sababu pia.
Zaidi ya hapo, nilisikia wanasema fikra pevu na ukada ni mbingu na ardhi.