Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 64,960
- 111,265
Kwenye siasa kuwa na msimamo unaoleweka na wa wazi ni jambo muhimu sana la kujenga heshima na kuaminika.
Ukiangalia katika siasa za Tanzania BAKWATA wao wamejifungamanisha wazi kabisa na CCM na serikali yake, hawajifichi na msimamo wao uko wazi kabisa unaeleweka kwa watawala na wafuasi wao, hawaongei kwa mafumbo na vitendawili.
Kwa upande wa TEC wao hawaeleweki wamesimama upande gani. Wanasema wanatetea haki lakini hapo hapo mguu mmoja wako ndani ya CCM na mwingine uko nje. Wanajifanya kama vile hawana "leverage" yoyote kwenye utawala.
Mfano katika uchaguzi wa 2025 BAKWATA wao walisema wazi wanaunga mkono huo uchaguzi na wakawa wanashiriki shughuli mbalimbali za uchaguzi, TEC wao walibaki nyutro wakiwa hawaeleweki wala kuwa na msimamo kama wanaunga mkono au wanaupinga huo uchaguzi!
Haki ina upande.