BAKWATA wana ushwawishi na nguvu kubwa kuliko TEC katika siasa za nchi

Sasa haya yote yana mchango gani kama hawawezi kuwa na karata/ turufu / leverage yoyote katika kufanya mambo wanayopigia kelele yabadilike ?
Wana tofauti gani na taasisi za Askofu Gwajima au Mwamakula ??
 
TEC sio BAKWATA elewa hilo
Hao hao tech wamepotea, bado wapo katika ujahili

Bakwata kama wanatumika kisiasa, na hawapo kwa ajili ya waislamu basi watakua na majibu mbele ya Mwenyezi Mungu.


ayat 64 from Surah Al-Ankabut

﴿وَمَا هَٰذِهِ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا لَهْوٌ وَلَعِبٌ ۚ وَإِنَّ الدَّارَ الْآخِرَةَ لَهِيَ الْحَيَوَانُ ۚ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴾
[ العنكبوت: 64]

Na haya maisha ya dunia si chochote ila ni pumbao na mchezo. Na nyumba ya Akhera ndiyo maisha khasa; laiti wangeli kuwa wanajua!
 
BAKWATA ni CCM B hasa aliyeko on throne akiwa wa upande wao, yaani kama hivi Sa100 basi hawa jamaa wanajifungamaisha na utawala kwa asilimia zote, ila akiwepo wa upande mwingine hawa jamaa wanakuwa vuguvugu, ndumilakuwili wanashindwa washike au waachie.
 
Bakwata ni serikali...tatizo waislamu ni vipofu ndiyo maana mnalia kuwa kanisa katoliki linakula pesa za serikali ila nafumbia macho bakwata ambayo ipo serikalini kabisa ni sehemu ya serikali ! Wanalindwa na serikali na kulipwa pesa za serikali kwa namna mbali mbali ...hivyo kuifananisha TEC NA BAKWATA NI KOSA LA KIMANTIKI
 
Sasa haya yote yana mchango gani kama hawawezi kuwa na karata/ turufu / leverage yoyote katika kufanya mambo wanayopigia kelele yabadilike ?
Wana tofauti gani na taasisi za Askofu Gwajima au Mwamakula ??
Tanzania sio state ya kidini, hii sio Zambia kwa hiyo ni lazma kanisa likitaka kupiga step lazma liangalie mbele.

Haya matamko tu yalionekana kama yanachochewe na udini. What if wakienda front, si itamaanisha serikali ipo chini ya kanisa.

Hii italeta nini katika jamii ambazo zinaamini Tanzania ina mfumo kristu?

Huoni hatari ya kanisa kwenda direct kwenye siasa na uongozi.

Wanachokifanya ndicho wanachopaswa kufanya. Kinachobaki ni kwa watanzania wenyewe. Kama wanaona kila kitu na kukaa kimya

Hata Kanisa likifanya kitu, impact yake itakuwaje consistent kama siku zote watanzania watabaki kama makondoo
 
Mbona BAKWATA wako front kabisa wanasimama na CCM na haionekani ni mfumo Islamu au serikali iko chini ya Uislamu ?

TEC wangejitokeza waseme hawaungi mkono uchaguzi na kuwasihi waumini wake wasishiriki huo uchaguzi kwa sababu ni sham ingekuaje ni mfumo Kristo au Serikali kuwa chini ya Kanisa? Mbona BAKWATA walitoka wazi hadharani wakaweka msimamo wao na kuhimiza waumini wao kushiriki uchaguzi??
 
Bakwata na TEC ni wapumbavu Tu hao
 
Hebu tueleze, KKKT nao wako upande gani?
 
Sema wana ushawishi na kutumika kwa Siasa za ccm na sio siasa za nchi.

Hilo liko wazi, ndio mana wao kila kitu hewala hewala kwa ccm.

Awamu hii hata waislam wengi sana wameidharau sana bakwata.
Hili nalo ni oni kutoka BAKWATA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…