Kimsingi Balile kapaniki na paniki yake ingeleta positive impacts kama waandishi wa habari na wamiliki wa hizi media angalau kwa asilimia 25% wangekuwa huru maana ameipa "air time" hiyo katuni imewafikia wengi; wenye akili kama zake na wenye "akili zao"
Kwa kuipata hiyo air time tu, wangeweza kujitafakari kwa kujiuliza nini mchora katuni alikusudia?
1. Alikusudia kufikisha ujumbe alioutafsiri (uelewa) Balile au Balile yeye kaamua kujipa tafsiri yake na kuiamini?
2. Alimaanisha hizi media zinatumika kusafisha uovu (uchafu) wa watu kwenye jamii? Yaani watu wanafanya uchafu wao bila hofu kwasababu wanajua kuna mahali "kisafishio" kipo na kitawasafishia uchafu wao bila wasiwasi?
3. Je, ni kweli wapo watu wanazitazama media kama "kisafishio" kwao?
4. Je, media kukubali kutumika kama "kisafishio" nani kamdharau mwenzake, media iliyokubali kutumika au aliyeomba kujisafisha?
5. Mchora katuni amelenga kutahadharisha media au amelenga kudhihaki media?
Ukijiuliza maswali kama hayo na mengine mengi unajikuta hauna sababu ya kupaniki kwasababu msanii kaleta sanaa yake na kila mmoja anatafsiri yake na hauna sababu ya kujifanya wewe ndo umeelewa zaidi
Hata hivyo, kupaniki kwake ni kama anataka kuonekana na watu fulani sehemu fulani kwa malengo fulani. Mimi nimemuelewa hivi