Balozi Batilda Buriani: Mtoto aliyeandika Barua ya kuacha Shule, ana akili sana

... halafu ndio kada isiyothaminiwa sana! Dah! Dogo anamhakikishia Mwalimu Mkuu kwamba HATANII! Ha ha ha!
Ni kada isiyothaminiwa na Nani ?

Ulitamani ipewe thamani kama kada ipi?
 
Mi ni mwalimu by profession. Moja ya dalili ya intelligent person ni poor hand writing.
Huo ni mtazamo hasi. Hakuna uhusiano wa intelligency na mwandiko, pamoja na hiyo profession yako usiseme uongo, tumesoma na tumeona wengi tu wenye miandiko mizuri na hamna kitu na wenye mibaya na wako vizuri.
 
Mnalishwa maneno na watu wanao pigia debe miradi yao na nyie mbaingia kuchwa kuchwa , kwani kabla ya hizo taulo za kike walio soma walisomaje? Kifup sijawahi kusikia bint kaacha shule kwa sababu ya kukosa taulo za kike zaid ya kusikilizia uzushi wa wapigania kombe kwa malengo yao .
 
Mwache asome atakuwa mvuvi wa watu
Hao waliosoma sana wanakitu gani maishani mwao,ni heri kujifunza fursa mapema ukaizoea,wewe huoni wahindi wanavyofanya kwa watoto wao,ama wewe ulishawahi kuona wapi ajira ikatoka serikalini katika kugombea ukaona mtoto wa kihindi akipanga foleni kwenye kufanya usaili
 
Bright with poor handwritting
Nampongeza sana dogo kwa maamuzi yake, amejitambua na kuweza kuchukua hatua ya kile alichokiamini.

Ila kuhusu uandishi fasaha ndio janga sana kwa kizazi hiki, sijui tatizo liko wapi...

Ukiangalia mwandiko wa mtu aliyeishia darasa la 4 la mkoloni ni mazuri sana, achilia mpangilio wa barua(ama ya kikazi au kirafiki, ambapo muundo wa uandishi hifundishwa tangu shule ya msingi) mwandiko umenyooka na mzuri sana.
 
Unadhani wahindi hawasomi au kwa vile huwaoni kwenye shule zenu za kata,wana shule zao,almuntazil,aga khan,shaaban robert,kisutu,upanga na vyuo wanasomea canada ,uk,usa.jidanganye
 
Nimedharau shughuri gani? Mbona kama unanibandikia matendo na maneno?
Uvuvi. Uvuvi siyo kitu kinafanywa na kila mtu tu. Ina ufundi wake ambao ni lazima ufundishwe kama zilivyo fani nyingine zote
 

Mara ya kwanza nilipoona hiyo barua, nilijiuliza sana kuhusu uandishi hasa suala la kupangilia, hili sio tatizo la dogo huyu tu, madogo wengi sana kizazi hiki wanakwama kupangilia miandiko.

Mimi nilipokuwa la nne nilikuwa naandika na kupangilia vizuri sana(ningekuwa karibu na madaftari yangu ya la nne ningetupia picha ya mwandiko wangu).

Mbali na hivyo nasimama na maamuzi ya dogo, amejitambua sana
 
Kwenye mambo kama haya kisaikolojia busara inahitajika zaidi kuliko viboko na lawana, safi sana...
 
Kabisa....hajui hata format ya Barua ,SoMo alilofundishwa darasa la nne!
Mm ninchoamini huyu kijana ni Jasiri!
 
Ni kama huyu kijana alieomba kazi NASA



NASA walimjibu vizuri tu na kumpa nafasi ya kutembelea vituo vya NASA kwa vile waliona ana akili sana



 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…