Ingekuwa nchi za Kiafrika sidhani kama meneja wa kampuni angejibu, yaani hata kusoma angegombana na katibu muhtasi wake, kwa nini kamletea uchafu.Ni kama huyu kijana alieomba kazi NASA
View attachment 2133496
NASA walimjibu vizuri tu na kumpa nafasi ya kutembelea vitu vya NASA kwa vile walipona ana akili sana
View attachment 2133497
For sure, nilimfuatilia akihojiwa na media duuuuuu anaongea na kujenga hoja as if kamaliza chuo cha kumbukumbu ya mwl NyerereDogo inaonekana anajua mambo mengi sana, yaani yuko smart sema mwandiko ndiyo unaweza mpiga mweleka japo siyo kesi
Mtu hana uhakika na mlo hata mmoja lazima aandike barua kama hiyo... halafu ndio kada isiyothaminiwa sana! Dah! Dogo anamhakikishia Mwalimu Mkuu kwamba HATANII! Ha ha ha!
Ni kweli huyu mtoto ana akili sana.Hata alivyojieleza unaona kabisa he is bright. Nadhani atolewe aende boarding ataafanya maajabu"MTOTO ALIYEANDIKA BARUA YA KUACHA SHULE ANA AKILI SANA" RC TABORA
"Niliongea na mkuu wa mkoa wa Mtwara baada ya kuona barua ya mtoto aliyetaka kuacha shule, nikamwambia huyu mtoto ana akili sana kwasababu haiwezekani mwanafunzi mtoro aandike barua kama hiyo, nikamwambia mkuu wa mkoa wa Mtwara mtafute huyu mtoto na kweli amemtafuta na kutatua changamoto zake na sasa amerudi shule mwenyewe, kwahiyo walimu wasaidieni watoto kuwajenga kisaikolojia"-Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Batilda Buriani katika kongamano la walimu na uchumi.
Taufiki Salumu mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Msimbati Mkoani Mtwara ambaye aliandika barua ya kuacha shule kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo amesema lengo kubwa la kutaka kuacha shule ni hali ngumu ya maisha ambayo imemlazimu yeye kuchukua maamuzi hayo.
Chanzo cha habari ni CGFM Tabora
Pia, soma:
1). Mtwara: Mwanafunzi wa kidato cha 1 aandika barua kwa Mwalimu Mkuu akisema Shule imemshinda
View attachment 2132031View attachment 2132032View attachment 2132033
.... by looking handwriting... a k a kwa kuangalia mwandiko.Mental slavery....who said brightness are maesured by looking handwriting
Kwako elimu ni kukaa juu ya madawati na kuandika kwenye daftari na kujua kuandika vizuri na kujua kingereza?Naona Watu wanapoteza pointi ya msingi ya hili suala.
Ni bora kukaa kimya na kutafakari badala ya kila Mtu kukimbilia kutoa hitimisho kwa hisia binafsi.
Huenda kila mmoja akawa na tafsiri yake ya kumtambua Mtu 'smart' lakini vipi kama tutadhani smart ni yule anayefikiri shule/elimu ndio inaweza kumkomboa yeye na wanaomzunguka?.
Nimeiona na kuisoma hiyo barua na sioni dalili yoyote ya kuonesha kama yupo smart (kupitia hiyo barua)...labda kama kuna taarifa nyingine nyuma ya pazia ambazo bado hatujazijua ambazo labda Mh anazifahamu...kinyume cha hapo tusimpumbaze yeye na wanaomzunguka.
Labda tuone u smart wake kwa namna alivyoamua kuvunja ukimya na kutoa la moyoni ambapo sasa sisi wengine tukae chini na kutafuta kuna nini kinaendelea?..kwa Kijana wa kidato cha kwanza (kama inavyosemekana ) kuandika hivyo basi ni dalili tosha kuwa Walimu hawakufanikiwa kumfundisha..au la labda ni mtoro kupita kiasi mpaka anashindwa kujifunza.
Na je hatudhani pia kuwa Wazazi wake nao ni tatizo?. huenda wao hawajasoma na hivyo hawaoni umuhimu wa Mwana wao kusoma.
Na kwa upande mwingine kama Mtoto anaona masomo yanamchanganya na kumpotezea muda hii ndio iwe chachu ya kuona umuhimu wa kuwa na elimu mbadala badala ya kulazimishana na mifumo ya elimu tuliyorithi kwa Wakoloni.
Vipi kama huyu sasa akaanza kuandaliwa kwa kupewa elimu ya uvuvi ya nadharia na vitendo?..ni kama ni sahihi nilivyosikia kuwa anatamani akafanye uvuvi.
Kwa karne hii hili si jambo la kushadadia bali ni kurudi nyuma na kujiuliza iweje 2022 Jamii bado haioni umuhimu wa elimu?.
Usichokijua ni hiki mdogo wangu mwenye muandiko mbaya huwa ana mambo mengi kichwani kwake kwa hiyo yy suala la kuandika huwa halizingatii mfano na mwenye muandiko mzuri huwa hana mambo mengi kwahiy muda anaotumia kuandika akili yake humakinika kwenye kuandikaBright with poor handwritting
We Mzee wa Kichaka Cha karanga ,acha kuchokoza Alumin 😂😂For sure, nilimfuatilia akihojiwa na media duuuuuu anaongea na kujenga hoja as if kamaliza chuo cha kumbukumbu ya mwl Nyerere
Private...hivi Kabende unatumia jina gani kule Jukwaa la Mapenzi na Mahusiano!For sure, nilimfuatilia akihojiwa na media duuuuuu anaongea na kujenga hoja as if kamaliza chuo cha kumbukumbu ya mwl Nyerere
Umewahi kuona miandiko ya madaktari? Au ya the called "genius"? Hawana muda wa kuremba.Bright with poor handwritting
Siyo kweli my bro ni Dr muandiko wake ni Kama pc imeandaka kwa mfumo wa times new romanUmewahi kuona miandiko ya madaktari? Au ya the called "genius"? Hawana muda wa kuremba.
Mtafute mkuu wa mkoa atakupatia namba
Hii ni uongo mkubwa huu.Mi ni mwalimu by profession. Moja ya dalili ya intelligent person ni poor hand writing.
Kabende Msakila - huwa napitia bila commentsPrivate...hivi Kabende unatumia jina gani kule Jukwaa la Mapenzi na Mahusiano!
Hilo tatizo limemalizwa kisiasa... Lakini dogo ukimuangalia kwenye hiyo picha unaona kabisa hajarudi shule!Kwahiyo RC wa Mtwara bila kuambiwa na RC Batilda asingechukua hatua yoyote!
Nchi ngumu sana.
..sidhani kama Dr.Batilda alikuwa na nakala ya barua ya mtoto aliyeacha shule kabla hajatoa kauli kuhusu mtoto huyo.
..Form 1 lakini anaandika kwa kiwango cha chini sana.
..huyo mwanafunzi tatizo lake sio muandiko tu, bali hata kupangilia maneno, na kuandika kwa ufasaha, hawezi.
..huyo dogo uwezo wake wa kuandika unalingana na mtoto wa darasa la 2 wakati mimi niko shuleni.
..pia dogo alitakiwa aandike barua yake kwa KIINGEREZA kwasababu hiyo ndio lugha ya mawasiliano ktk shule za SEKONDARI.
..simlaumu dogo bali nailaumu serikali kwa kushindwa kuboresha mazingira ya utoaji elimu haswa kwa maeneo ya vijijini.
Cc Nguruvi3, MALCOM LUMUMBA