Uchaguzi 2020 Balozi wa Japan ashangazwa na ubadhilifu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Uchaguzi 2020 Balozi wa Japan ashangazwa na ubadhilifu Uchaguzi Mkuu wa Tanzania

Balozi ana haki ya kuongelea uchaguzi wowote wa kijeshi. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
Kwa hiyo yaliyotokea kwenye Uchaguzi wa Rais wa USA 2020 pia ilikua ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi??
Naomba unijibu hili [emoji1483]swali tafadhali.
 
Kwa taarifa yako tu matamko yao ni soft cash, kunauwezekano mkubwa wa kukosa hard cash mbele ya safari.
Jifunze kujitegemea mtanzania mwenzangu. Misaada tunayoletewa si ya bure. Hivi kwann mnarubuniwa na kitu kinachoitwa “misaada “.
Kumbuka hao wakoloni, mabeberu na makaburu sio baba zako au mama zako wazazi wakupe msaada bila malipo au wao kunufaika. Amka mtanzania mwenzangu.
 
Naomba nitoe lineage ya Ufalme kwa kule Japan wanaita Emperor.Ufalme wa kijapan umeanza miaka mingi na ni wazamani katika dunia nzima kuongozwa na familia moja.

Mfalme wa kwanza aliitwa Jimmu alitawala miaka ya 11th feb 660BC yaani kabla ya YESU hajazaliwa.Turuke siwezi kutaja majina ya wafalme waliofuatia wote nitataja wa hivi karibuni.

Hirohito 1926-1989
Akihito 1989-2019
Naruhito 2019-aliyeko madarakani hadi sasa
Huyu aliyeko madarakani hadi sasa amepokea kutoka kwa baba yake Akihito na ni mfalme wa 126 kuanzia Jimmu kule juu.Baba yake aliamua kumkabidhi mwanae rungu baada ya kuona afya yake Inadorora na inasemekana ni mfalme pekee aliyekabidhi madaraka kwa ridhaa yake mwenyewe kwa miaka mia mbili iliyopita tukio kama hilo ndio lilitokea.

Sasa nisiwachoshe nia yangu hapa ni kumuonyesha balozi kuwa kama anatuchungulia akachungulie kwao Japan kwanza how come wanakabidhiana madaraka kwa familia moja Mfano babu yake Naruhito huyu kiongozi wa sasa yaani Hirohito alikaa madarakani miaka 63 ndio akamkabidhi mwanae Akihito mwaka 189 ambaye ndo baba wa huyu Naruhito wa sasa.

Sisi tuna utaratibu wetu kwa kutumia kura najua watu watasema nchi ya kifalme haina uchaguzi sawa mwenye uchaguzi ni waziri mkuu basi kama ni hivyo basi wasitufundishe sisi demokrasia.

Wakamhoji Malkia Elizabeth kwanza na Naruhito watuanchie ya kwetu na sisi ndio utaratibu wetu watuachie tumechagua wenyewe kwa kupenda.
Nakushukuru sana kwa maelezo yako.
Naomba usichoke kuchangia hoja kwa kutumia mifano hai kama hii.
Jamani, tusichoke kuwaamsha na kuwaelewesha hawa watanzania wenzetu wanaorubuniwa na itikadi na mifumo ya watu wa magharibi.
 
Washikirika wa mataifa makubwa wote wanatoa matamko yanayotia shaka juu mchakato mzima kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020 na matokeo yake.

Hapa ni mtihani mkubwa kwa serikali ya CCM Mpya kuweza kuendelea kupata misaada toka kwa "wadau wa maendeleo" baada ya uchaguzi huu batili wa 2020 ulioupa CCM Mpya miaka mitano mingine.

Yetu macho tutazame kinachoendelea baada ya CCM Mpya kulazimisha kuwepo madarakani kwa njia haramu kupata madaraka ya urais na kulimiliki bunge.
Naomba ukae ukijua hao unaowaita wadau wa maendeleo wanatoa misaada bure. Hao sio baba zako wazazi wala sio wajomba zako. Hivyo basi hao wadau wa maendeleo hawawezi kukupa msaada bure. Hicho kitu hakipo kwenye huu uso wa dunia tunayoishi.
 
Dah kweli hawa jamaa wanataka kutuzoea. Hadi Japan wanatupiga mkwara na macho yao nusu.
Sisi uchaguzi wetu ulikuwa na sintofaham, wao mfalme wao anachaguliwa kwa kura za wananchi gani?
Tena tujiulize hivi huyo Waziri mkuu anayeteuliwa na wananchi kwa kutumia mfumo wa vyama vingi ni nani mwenye nguvu zaidi? Waziri mkuu au Mfalme?
 
Kinachokera zaidi ni walioua watu na kuwadhulmu haki zao wao bado wapo na wanapandishwa vyeo na familia zao zinaishi maisha ya raha mustarehe. Waliopigwa na kudhalilishwa wanawindwa ili hata wasilalamike.

Waliovuruga uchaguzi wala hawajiaikii nafsi zikiwasuta mana mema waliyoahidiwa wanazidi kuyapata wakiwa duniani.

Wenyeviti wa upinzani wajiuzulu mana wameshindwa kujenga vyama vyao kiitikadi.

Lindi kama ingekuwa ndiyo Hai anakotoka Mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani na mbunge mlevi na msanii Mbowe nafikiri uhuni ungekoma kwenye nchi hii .

Halafu Mwanamke kule Nkasi amedhibiti wizi kwenye jimbo lake ,wanaume wapumbavu wanamwambia asiende kuapishwa. Ile ni ajira ndio maana analipwa . Upinzani onyesheni uwezo wa kujipanga na kuwakataa viongozi wasiofaa kama Dikteta Mbowe. Hafai kuongoza tena Chama mana ameshindwa kukijenga jimboni kwake mwenyewe.

Ni mbinafsi mbaya sana. Huwezi kuwa na kofia tatu kubwa kisiasa halafu hujawajenga watu kiitikadi hata wa nyumbani kwako. Hai hakuna hata MTU aliyeandamana kupinga uonevua anaofanyiwa mbunge wao kwa miaka 15 . Bila shaka hakua na faida nao. Ni mbinafsi . MTU mbinafsi hawezi kuwa mpigania haki zaidi ya kupigania uenyekiti wake ili azidi kuudhoofisha upinzani.
 
Huyu Balozi naye, amekaa ofisini akilishwa matango pori naye anakurupuka kupost[emoji848]! Kwani amesikia wapi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]! Wengewe wapiga kura na wasimamizi mbona hatukuziona kizo rafu[emoji848]! Itabidi tumchunguze huyu mjepu!
 
Tell the Ambassador to mind his representation of his country Japan and not to become apolitical analyst and we vehement refuse and denounce any foreign involvement in our democracy and tell the Ambassador that the overwhelming majority is a message to the world at large that Tanzanians can differentiate between a brick and a loaf, the majority is to protect our NATURAL RESOURSES simple!
 
How credible is that "information of widespread irregularities and wrongdoings" is the ambassador talking about? Have that information been verified and substantiated , or he's just talking about hearsay?
 
Hongera bwana balozi. Kwetu Zanzibar tunapigwa usiku kucha hadi hii leo. Viongozi wetu wamepigwa na wengine hatujui waliko. Magu ameleta jeshi kuja kufanya mapinduzi. Hakuna ambae hakushuhudia mapinduzi . Halafu Mwinyi anasema anataka maridhiano. Zanzibar ina katiba ya serikali wa UMOJA wa KITAIFA, sasa kama ni hivo, vita na majeshi dhidi ya wazanzibari ni za nini.

CCM wameua raia 15 na kuna maiti zilizo tupwa baharini, na maiti ziliopo mnazi mmoja. Sasa sisi mumetupiga bure, nchi ni ya vyama vingi. Kura tumewashinda. sasa kama mumeiba sio lazima kuuwa. Sote wazanzibari tuna masikitiko ya kupigwa na majeshi. Hatuna msaada maana ndugu zetu mumetuacha mkono. Mateso haya yana mwisho na mwisho uko karibu. Tumenyamaza lakini ukimya wetu mutsikiya jawabu lake.
 
Kwani wewe kuandamana mpaka uwe na wengine? Kama hawakuja kuandamana jua hawakuungi mkono na wanaunga mkono serikali hii. Pia juwa hao ndiyo waliyompigia kura Magufuli kura, kwani wao wajinga wampigie kura kisha waandamane kumpinga. Ni wenda waxzimu tu watafanya hivyo.
Unajiona smart kumbe ovyo hahaha, haya nenda kwa mama kachukue hela ya bando
 
Kwa hiyo yaliyotokea kwenye uchaguzi wa raisi wa USA 2020 pia ilikua ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi??
Naomba unijibu hili 👆🏾swali tafadhali.

Yametokea nini? Naona umejiunga juzi jumapili hapa jukwaani umekuja na moto kama umefunga turbo.
 
Anaestahili kushinda uraisi ni yule kiongozi makini, anaelinda rasilimali zetu na yule anayewabana wafadhili wanaoikandamiza nchi na kuiba madini yetu, na yule asiyeburuzwa na mabeberu na makaburu.

Anayefaa kushindwa uchaguzi wa raisi ni yule kiongozi mwenye uhusiano wa karibu na wakoloni, anayetumiwa na wakoloni kwa kutetea maslahi ya wakoloni ili wamiliki rasilimali za nchi yetu.
Sasa mbona ameiba kura wakati wananchi wamemkaraa kwa kupitia Kura Kama kweli analindwa rasilimali.
 
Marekani wao popular vote haimpi Urais mtu. Ellectoral College (hawa ni watu objective) as checks measures to balance mihemko. Hao ndio wanakuambia wewe uende na popular vote kumpata Rais.

Na makemeo lukuki 🙂 we have a long way to go.

Nimekuelewa Chief
Sifikirii kama wanakulqzimisha ufuate popular vote kama demokrasia yako ime base kwenye misingi ya Electoral College. Ila kama wewe misingi yango ya demokrasia imebase kwenye popular vote basi wanataka uufuate huo msingi.
 
Haturudi nyuma, hatuna muda wa kuchezea.

Balozi afanye kazi yake, mambo yetu ya ndani hayamhusu, na kama amekwazika afunge virago.
Mbona mkiambiwa ukweli mnapanik sana, jiwe hana uhalali wa kuwa Rais sema ndiyo hivyo tena
 
Wajapani wana hasira na Tanzania sababu tenda za ujenzi wa barabara Magufuli anawapa wachina sio kampuni za Japan
 
Jifunze kujitegemea mtanzania mwenzangu. Misaada tunayoletewa si ya bure. Hivi kwann mnarubuniwa na kitu kinachoitwa “misaada “.
Kumbuka hao wakoloni, mabeberu na makaburu sio baba zako au mama zako wazazi wakupe msaada bila malipo au wao kunufaika. Amka mtanzania mwenzangu.
Sizungumzii nyumbani kwangu ninazungumzia nchi, lugha uliyotumia si ya hoja hii kwani misaada haiamriwi na mtu mmoja. Nchi duni za dunia ya tatu zinakabiliwa na ufisadi uliokithiri na mipango ya mtu mmoja na ni sababu kubwa ya kutegemea mikopo na misaada.
 
How credible is that "information of widespread irregularities and wrongdoings" is the ambassador talking about? Have that information been verified and substantiated , or he's just talking about hearsay?
Itakuwa umefanya mazoezi usiku kucha, hongera.
 
Back
Top Bottom