TANZIA Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine J Mushi, afariki dunia kwa ajali ya Gari

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Balozi_Celestine_Mushy_360_453shar-50brig-20_c1_c_t.jpg

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Joseph Mushy, amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati akiendesha gari aina ya crown lenye namba za usajili T175 DMF kuelekea Moshi, Kilimanjaro.

===

Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki ajalini​

Alhamisi, Desemba 15, 2022
balozi-pic.jpg

Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy

Muktasari:​

Balozi huyo amefariki juzi Jumanne alipokuwa akisafiri kwa kuendesha gari mwenyewe kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Tanga. Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa hapa.

Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Desemba 15, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo ambaye alikuwa peke yake alikuwa akiendesha mwenyewe gari akotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.

"Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua," amesema Mchembe.

Alipoulizwa kuhusu kifo cha balozi huyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amesema wizara yake haijapata taarifa rasmi, wakipata watathibitisha hilo.

"Hatujapata taarifa hizo, tuta-comfirm (tutathibitisha), tutakwambia," amesema Balozi Sokoine.

Chanzo: Mwananchi
20221216_064718.jpg
 
RIP Mheshimiwa balozi. Barabara zetu na uchovu zinamaliza sana waTanzania

Toka maktaba :

Vienna, Austria
Published: May 9, 2022; 22:36

H.E. Mr. Celestine Joseph Mushy presenting his credentials (© www.bundespraesident.at / Peter Lechner and Daniel Trippolt /HBF)
Bundespräsident Alexander Van der Bellen empfing heute, am 5. Mai 2022, folgende neue Botschafterin und neue Botschafter in der Präsidentschaftskanzlei und nahm ihre Beglaubigungsschreiben entgegen

H.E. Mr. Celestine Joseph Mushy presenting his credentials to H.E Alexander Van der Bellen the Federal President of Austria (© www.bundespraesident.at / Peter Lechner and Daniel Trippolt /HBF)

Mr. Celestine Joseph Mushy - Ambassador of Tanzania (© www.bundespraesident.at / Peter Lechner and Daniel Trippolt /HBF)Mr. Celestine Joseph Mushy - Ambassador of Tanzania (© www.bundespraesident.at / Peter Lechner and Daniel Trippolt /HBF)

Ambassador of the United Republic of Tanzania to Austria H.E. Mr. Celestine Joseph Mushy

During his career, Mr. Mushy served as the Assistant Administrative Secretary, Mtwara Regional Commissioner's Office and as the Second Secretary in the Permanent Mission of Tanzania to the United Nations in New York.

When Celestine Joseph Mushy, Ambassador of Tanzania to Austria presented copies of Certificates of Identity to Hon. Ambassador Peter Launsky-Tieffenthal, Permanent Secretary, Austrian Ministry of Foreign Affairs, the Secretary-General presented the Ambassador with a gift of cashew nuts that are grown and processed in Tanzania by an Austrian company known as Biotan Group Ltd with a factory located in Mbagala. The company produces and processes organic cashew nuts
Source : Meet the New Ambassadors of Brazil, Germany, Tanzania and Rwanda to Austria
1671108410080.png
 
#Breaking Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Joseph Mushy, amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati akiendesha gari aina ya crown lenye namba za usajili T175 DMF kuelekea Moshi, Kilimanjaro.
Mungu amueke mahara pema poponi,.........ila balozi wetu kuendesha crown sloon sijui ndo economy yetu ndo ilivyo au ubahili?
 
Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Joseph Mushy, amefariki dunia kwa ajali ya gari eneo la Mkata, wilayani Handeni mkoani Tanga.
Ajali hiyo imetokea jana usiku wakati akiendesha gari aina ya crown lenye namba za usajili T175 DMF kuelekea Moshi, Kilimanjaro.

===

Balozi wa Tanzania nchini Austria afariki ajalini​

Alhamisi, Desemba 15, 2022
balozi-pic.jpg
Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy

Muktasari:​

Balozi huyo amefariki juzi Jumanne alipokuwa akisafiri kwa kuendesha gari mwenyewe kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Kilimanjaro.

Tanga. Balozi wa Tanzania nchini Austria, Celestine Mushy amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni mkoa wa hapa.
Mushy aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Balozi wa Tanzania nchini Austria Januari mwaka huu na Mei 5, 2022 akawasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Austria, Alexander Van der Bellen.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Desemba 15, 2022, Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe amesema kuwa balozi huyo ambaye alikuwa peke yake alikuwa akiendesha mwenyewe gari akotokea Dar es Salaam kuelekea Moshi mkoani Kilimanjaro.

Mchembe amesema kuwa ajali hiyo imetokea juzi Jumanne usiku ambapo mwili wa balozi huyo umekutwa ukiwa umeungua.
"Mwili wa balozi tuliuchukua eneo la ajali usiku na tumeuleta Hospitali yetu ya Wilaya. Ndugu zake wapo njiani wakitokea Mbezi Dar es Salaam wanakuja kuuchukua," amesema Mchembe.

Alipoulizwa kuhusu kifo cha balozi huyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amesema wizara yake haijapata taarifa rasmi, wakipata watathibitisha hilo.

"Hatujapata taarifa hizo, tuta-comfirm (tutathibitisha), tutakwambia," amesema Balozi Sokoine.

Chanzo: Mwananchi
RIP balozi, ila wachagga tarehe hizi siyo nzuri kwenda kuhiji.
 
RIP Balozi Mushi, nimeamini wanaopendwa na wengi hufa wangali vijana!.
Huyu ni Balozi mshikaji wangu wa 4 kuchomoka pale foreign!, alianza Balozi Cisco, akaja Balozi Akili, akaja Balozi Edwin Rutageruka!, sasa Balozi Celestine Mushi!.

Ila pia wajameni kama hali ya uchumi inaruhusu, kwa upande wa gari ndogo, saloon cars, kwa long trips, nashauri nunua chuma cha Mjerumani, na sio haya mabati ya makaratasi ya Japan!.
RIP Balozi Mushi!.

P
 
RIP Balozi Mushi, nimeamini wanaopendwa na wengi hufa wangali vijana!.
Huyu ni Balozi mshikaji wa 3 kuchomoka pale foreign!, alianza mshikaji Balozi Cisco, Mshikaji Balozi Akili, kufunga kufungua mshikaji Balozi Edwin Rutageruka!, sasa mshikaji Balozi Celestine Mushi!.

Wajameni kama hali ya uchumi inaruhusu, kwa gari ndogo, saloon cars, nunua chuma cha Mjerumani, na sio makatasi ya Japan!.
RIP Balozi Mushi!.
nunua chuma cha Mjerumani, na sio makatasi ya Japan!.
Hiyo nimeipenda japo imewekwa msibani..☝️.
Apumzike kwa amani.
 
RIP Balozi Mushi, nimeamini wanaopendwa na wengi hufa wangali vijana!.
Huyu ni Balozi mshikaji wa 3 kuchomoka pale foreign!, alianza mshikaji Balozi Cisco, Mshikaji Balozi Akili, kufunga kufungua mshikaji Balozi Edwin Rutageruka!, sasa mshikaji Balozi Celestine Mushi!.

Wajameni kama hali ya uchumi inaruhusu, kwa gari ndogo, saloon cars, nunua chuma cha Mjerumani, na sio makatasi ya Japan!.
RIP Balozi Mushi!.
Inasemekana huyu bwana kapiga tukio huko kwenye kituo chake..vipi tuunganishe nukta?
 
Mungu amueke mahara pema poponi,.........ila balozi wetu kuendesha crown sloon sijui ndo economy yetu ndo ilivyo au ubahili?
Banaa wewe Crown sio za kinyonge achana na hizi Crown za 16 million, kuna Crown zinafika hadi 80 million na kuendelea.. Crown usiposhtuka na barabara zetu mbona hatari, huenda alijisahau akafikiri yupo Austria 😑😑
 
Back
Top Bottom