Serikali ya awamu ya nne wakati inataka kutaifisha mashirika muhimu ikiwemo bandari, aliyetupa taarifa alifukuzwa kazi. Alitupa taarifa ya kutokubali kuyataifisha kutokana umuhimu wake kwa usalama wa Taifa.
Dkt. Slaa ameongelea mfano wa mbia katika kampuni ya mafuta wakati wa vita ya Uganda ambapo Tanzania ilikuwa inamiliki 51% katika kampuni hiyo huku mbia akiwa na 49% lakini aliweka ngumu kwasababu alidai mtu tunayepigana nae ni mbia wake pia hivyo. Slaa amedai kwa siku 5 vifaa havikuweza kuondoka kwasababu ya mafuta wakati nchi inaendelea kupigwa.