Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi
Waandishi wa habari washutumiwa kutumika kuchafua wanaosema ukweli pia kufanywa chombo cha propaganda kuandama wanasiasa wanaosema kweli kuhusu mapungufu ya mkataba, mfano Mh. Freeman Aikaeli Mbowe ameshutumiwa sana na baadhi ya vyombo vya habari kipropaganda

1686648206880.png
 
Tegemea kuanzishwa kwa makundi mengi ya ugaidi miaka michache ijayo .silaha za kuipiga Congo zitapitishwa bandari yetu,machafuko ya afrika mashariki na kati yataanzia mikononi mwetu ..USA ndie aliyeratibu hili na yuko nyuma ya hili ..
 
Balozi Dkt. Willibrod Slaa anazungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, leo Juni 13 2023 kuhusu hati ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya Tanzania na DP World.

=======

Dkt. Slaa: Hadi kufikia hatua ya azimio hili kuridhiwa na Bunge, ikumbukwe makubaliano ya awali yalifanyika tarehe 28 February, kampuni ya DP World na bandari waliingia kwenye makubaliano yalitokana na shughuli iliyofanyika Dubai expo 2022, hatujaambiwa ni tathmini gani au utafiti gani ulifanyika

Kwenye expo, kwenye maonesho kama yale ya sabasaba Dar es Salaam watu wanaingia kwenye mkataba mkubwa wa kulifunga Taifa, nadhani mnaelewa hiyo maana yake ni nini!

Hadi wakati huu Taifa na watanzania walikuwa hawajapewa taarifa yoyote ile inayohusu mkataba mkubwa wa aina hiyo.

Naomba kuwakumbusha pia kuwa pamoja na mkataba huu, katika Dubai 2020 Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Rais mwenyewe kulisainiwa mikataba 17, nani kati yenu hadi leo hii anaifahamu mikataba 17 inahusu nini, ni usiri mtupu, ni nchi inaingizwa kwenye giza, Rais wa Nchi amehudhuria lakini mambo hayo yote yako ndani ya giza.

Waliohudhuria maonesho ni viongozi wa Serikali, wamesafiri, wamelala hoteli, wamekula chakula kwa kodi ya watanzania, ni Tanzania pekee ambako Serikali haiwajibiki kwa wananchi wake, jambo ambalo katika hatua hii, jambo ambalo linalazimisha kuwakumbusha uhitaji wa haraka wa katiba mpya na bora.

Hii taarifa tunayozungumzia hatukuipata Serikalini, tumepata taarifa iliyovuja. Ni nchi gani duniani tunasubiri taarifa ivuje tuanze kuizungumzia. Siku siku 30 zilizotajwa kwenye mkataba na Bunge, kwa maneno mengine umeridhiwa ndani ya siku 30 lakini umekuja kuridhiwa baada ya miezi takribani 8, kwa hali hiyo tuna uhakika gani Tanzania ina uwezo wa kutimiza mkataba huu kama mwanzo tayari ni mbaya na hakuna anayeeleza uchelewashaji huo unatokana na nini.

Dkt. ametoa hoja zifuatazo
  1. Dkt. Slaa: Nchi inayojulikana kisheria ni United Arab Emirates, Je Dubai ni Serikali? Dubai ni mji unaojiongoza, sisi ni nchi ya Jamhuri ambayo maamuzi yetu yanafanyika kwa kutumia Bunge. Bunge lilitangaza wanataka maoni ya wananchi tarehe 5 Juni wanaotoka maeneo mbalimbali wawe wamefika bungeni tarehe 6. Kwa saa 24 mtanzania gani anafika Dodoma na kutoa maoni yake. Ni dhahiri kuliwa na hila na Serikali haikuwa na nia ya kushirikisha wananchi wake. Hatukushirikishwa na imepelekwa bungeni na mjadala ulivyokuwa bungeni ulikuwa ni mjadala wa ki-mangimushi
  2. Aidha ikumbukwe Serikali iliyopo ina legitimacy ya wasiwasi kutokana na uchaguzi wa 2019 na 2020. Simung'unyi maneno, uchaguzi wa 2019 na 2020 inaweza kuwa na legitimacy lakini sina hakika kama uchaguzi huo ulikuwa sahihi, najua ulivurugwa kwa makusudi na chama cha mapinduzi na vyombo vyake. Mwenye macho haitaji kuambiwa kuhusu hilo na wananchi wote ni mashahidi.
  3. Kwa mujibu wa kifunge cha nne cha IGA kinatamka wazi rasilimali zote zilizotajwa zinakabidhiwa kwa Serikali ya kigeni. Rasilimali hizo ni bandari zote za nchi nzima(bahari, maziwa, mito, zitakazokuwepo hata kwenye mabwawa) yale yote yaliyokuwepo leo na hata yatakayokuja. Huu ni uuzaji wa nchi, hakuna mwenye Tanzania mwenye akili atakaekubali jambo hilo bila uhakika wa rasilimali zake hizo.
  4. Serikali ya awamu ya nne wakati inataka kutaifisha mashirika muhimu ikiwemo bandari, aliyetupa taarifa alifukuzwa kazi. Alitupa taarifa ya kutokubali kuyataifisha kutokana umuhimu wake kwa usalama wa Taifa. Dk
    Dkt. Slaa ameongelea mfano wa mbia katika kampuni ya mafuta wakati wa vita ya Uganda ambapo Tanzania ilikuwa inamiliki 51% katika kampuni hiyo huku mbia akiwa na 49% lakini aliweka ngumu kwasababu alidai mtu tunayepigana nae ni mbia wake pia hivyo. Slaa amedai kwa siku 5 vifaa havikuweza kuondoka kwasababu ya mafuta wakati nchi inaendelea kupigwa.

Excellent Baba
 
tuwasikie na wale wanaojiita wanasheria uchwara wabishane na Dr Slaa kwa hoja.nchi hii iliishauzwa ndo maana serikali inatumia nguvu kubwa kuharmonize mazingira lkn ukweli unabaki pale pale.ni hatari sana kuwa na wabunge waliochaguliwa kwa hila pale bungeni sababu hata wao hufanya mambo kwa hila.tupige na kupaza sauti hayo makubalinao yawe nullified kama sivyo hao wabunge wote 2025 waisrudi bungeni.
 
Habari

Sina mengi moja kwa moja kwenye point tunaomba sisi kama watanzania kusitishwa haraka Kwa uwekezaji wa BANDARI zetu/yetu Kwa DUBAI

hatuko radhi na uwekezaji wa bandari yetu Kwa yeyote yule kiufupi hakuna MTANZANIA aliyefurahishwa na hilo Kama tunaweza kulipia matengenezo yote ambayo tunayoyataka yawe kwenye bandari yetu pendwa na iwe hivyo lakini kwa swala la wawekezaji hatupo radhi

Wapeni mashamba walime na sio bandari zetu

Asantum
 
Back
Top Bottom