Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi
Hawawezi kukuelewa Mkuu! Huoni nguvu kubwa ya ushawishi inavyotumika? Hawataki kusikia upinzani kwenye hili, nimeona clip ya Chris Lukosi imewekwa kwenye Account ya Facebook ya Mama yupo Kazini akitetea uwekezaji huo.

Kwa maelezo yake anasema eti Kampuni hiyo imepewa uwekezaji kwenye Bandari za Uingeleza ikiwemo London Gate Way na Southampton, hivi anafahamu Uingeleza wameingia Mkataba gani na Dubai? Suala hapa ni aina ya Mkataba ambao Serikali inaingia na Dubai, hivi Nchi yetu inaingia Mkataba wa hovyo kama huu lakini Kuna Watu wanajitoa ufahamu na kutetea uozo.
 
Ina maana CCM haijampa TOR? Huwezi kumruhusu agent akiwashe wakati huu wa taharuki
Mtakuja kunishukuru,
huu ni wakati wa kumrudisha Agent katika nafasi yake kwa faida ya baadae.
CCM haiufii chochote kuhusu huo mkataba wanauhakika utaenda kama ulivyo pangwa.
Kama walivyo fanya ktk uchaguzi mkuu 2020 na mkatulia kimya.
 
Balozi Dkt. Willibrod Slaa anazungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, leo Juni 13 2023 kuhusu hati ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya Tanzania na DP World.

=======

Dkt. Slaa: Hadi kufikia hatua ya azimio hili kuridhiwa na Bunge, ikumbukwe makubaliano ya awali yalifanyika tarehe 28 February, kampuni ya DP World na bandari waliingia kwenye makubaliano yalitokana na shughuli iliyofanyika Dubai expo 2022, hatujaambiwa ni tathmini gani au utafiti gani ulifanyika

Kwenye expo, kwenye maonesho kama yale ya sabasaba Dar es Salaam watu wanaingia kwenye mkataba mkubwa wa kulifunga Taifa, nadhani mnaelewa hiyo maana yake ni nini!

Hadi wakati huu Taifa na watanzania walikuwa hawajapewa taarifa yoyote ile inayohusu mkataba mkubwa wa aina hiyo.

Naomba kuwakumbusha pia kuwa pamoja na mkataba huu, katika Dubai 2020 Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Rais mwenyewe kulisainiwa mikataba 17, nani kati yenu hadi leo hii anaifahamu mikataba 17 inahusu nini, ni usiri mtupu, ni nchi inaingizwa kwenye giza, Rais wa Nchi amehudhuria lakini mambo hayo yote yako ndani ya giza.

Waliohudhuria maonesho ni viongozi wa Serikali, wamesafiri, wamelala hoteli, wamekula chakula kwa kodi ya watanzania, ni Tanzania pekee ambako Serikali haiwajibiki kwa wananchi wake, jambo ambalo katika hatua hii, jambo ambalo linalazimisha kuwakumbusha uhitaji wa haraka wa katiba mpya na bora.

Hii taarifa tunayozungumzia hatukuipata Serikalini, tumepata taarifa iliyovuja. Ni nchi gani duniani tunasubiri taarifa ivuje tuanze kuizungumzia. Siku siku 30 zilizotajwa kwenye mkataba na Bunge, kwa maneno mengine umeridhiwa ndani ya siku 30 lakini umekuja kuridhiwa baada ya miezi takribani 8, kwa hali hiyo tuna uhakika gani Tanzania ina uwezo wa kutimiza mkataba huu kama mwanzo tayari ni mbaya na hakuna anayeeleza uchelewashaji huo unatokana na nini.

Dkt. ametoa hoja zifuatazo
  1. Dkt. Slaa: Nchi inayojulikana kisheria ni United Arab Emirates, Je Dubai ni Serikali? Dubai ni mji unaojiongoza, sisi ni nchi ya Jamhuri ambayo maamuzi yetu yanafanyika kwa kutumia Bunge. Bunge lilitangaza wanataka maoni ya wananchi tarehe 5 Juni wanaotoka maeneo mbalimbali wawe wamefika bungeni tarehe 6. Kwa saa 24 mtanzania gani anafika Dodoma na kutoa maoni yake. Ni dhahiri kuliwa na hila na Serikali haikuwa na nia ya kushirikisha wananchi wake. Hatukushirikishwa na imepelekwa bungeni na mjadala ulivyokuwa bungeni ulikuwa ni mjadala wa ki-mangimushi
  2. Aidha ikumbukwe Serikali iliyopo ina legitimacy ya wasiwasi kutokana na uchaguzi wa 2019 na 2020. Simung'unyi maneno, uchaguzi wa 2019 na 2020 inaweza kuwa na legitimacy lakini sina hakika kama uchaguzi huo ulikuwa sahihi, najua ulivurugwa kwa makusudi na chama cha mapinduzi na vyombo vyake. Mwenye macho haitaji kuambiwa kuhusu hilo na wananchi wote ni mashahidi.
  3. Kwa mujibu wa kifunge cha nne cha IGA kinatamka wazi rasilimali zote zilizotajwa zinakabidhiwa kwa Serikali ya kigeni. Rasilimali hizo ni bandari zote za nchi nzima(bahari, maziwa, mito, zitakazokuwepo hata kwenye mabwawa) yale yote yaliyokuwepo leo na hata yatakayokuja. Huu ni uuzaji wa nchi, hakuna mwenye Tanzania mwenye akili atakaekubali jambo hilo bila uhakika wa rasilimali zake hizo.
  4. Serikali ya awamu ya nne wakati inataka kutaifisha mashirika muhimu ikiwemo bandari, aliyetupa taarifa alifukuzwa kazi. Alitupa taarifa ya kutokubali kuyataifisha kutokana umuhimu wake kwa usalama wa Taifa.
    Dkt. Slaa ameongelea mfano wa mbia katika kampuni ya mafuta wakati wa vita ya Uganda ambapo Tanzania ilikuwa inamiliki 51% katika kampuni hiyo huku mbia akiwa na 49% lakini aliweka ngumu kwasababu alidai mtu tunayepigana nae ni mbia wake pia hivyo. Slaa amedai kwa siku 5 vifaa havikuweza kuondoka kwasababu ya mafuta wakati nchi inaendelea kupigwa.
  5. Slaa pia ametoa mfano wa 'Entebbe Raid' ambapo amesema ndege ya Air France ilitekwa nyara na wapiganaji wa Palastine wakishinikiza mambo yao ya kisiasa ndani ikiwa na waisraiel ilitua uwanja wa Entebbe. Slaa amedai Waisrael iliwachukua chini ya dakika 90 kuwakomboa watu wao na amedai iliwezekana kwasababu wao ndio waliojenga uwanja na ramani zote walikuwa nazo ikiwepo sehemu ya kuingilia na kutokea.
  6. Slaa amesema sababu hapo juu pia ilisababisha Serikali ya awamu ya tano itumie wajenzi wa ndani kujenga Ikulu lakini sasa bandari zote zinakabidhiwa kwa mgeni.
  7. Dkt. Slaa: Mkataba unaotoa 'exclusive rights' daima uogope, inatoa pia kifungu baadae yatakayojadiliwa kwenye mikataba midogo midogo, unatoa kwanza mali yako, unajuaje wakifika kwenye hiyo mikataba midogo midogo wakikutalia! Una nguvu gani, ulishasain 'exclusive rights'
  8. Utekelezaji wa DP World sio kwamba unaanza Tanzania, katika Afrika peke yake tuna migogoro mingi. Nenda nchi za Ulaya, Brussels ni yaUlaya laikini wako mahakamani, karibu kote kunakogombaniwa ni rushwa, kuna wabungwe walipelekwa, wakalishwa, wakapewa posho ya dola 2000 yote hiyo ni rushwa. Kama ingekuwa nchi nyingine, hizo zinatosha kufuta mkataba huu na kapeleka hata hiyo kampuni mahakamani.
  9. Sijawahi kuona mkataba(IGA) Marekani na Ulaya amabo una lugha kama hii ya kwetu, waathirika tumewaandaaje mfano ujenzi wa reli bandarini mpaka airport. Tumeona barabara ya Kibaha watu walivyolia Kimara. Mikataba hii lazima iwe ya tahadhari sana.
  10. Tunayasema haya kwa nia njema lakini tunashangazwa na kutishwa na propaganda ambayo Serikali inafanya, jambo jema huwa haliendeshwi kwa propaganda, ukiona mtu anafanya propaganda ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye madhehebu ya dini anza kuweka mashaka, kuna maslahi gani nyuma ya makubaliano hayo!







Lakini Padre, Dr. Wilbrod P.Slaa legitimacy yako pia iko na wasiwasi mingi. Pia huu uchambuzi wako wa kawaida sana hauna hisia za uchungu za kizalendo, me nadhani unajaribu ku-lay down trap kwa vyama vya siasa vivutiwe nawe upate nafasi ambayo unaitamani sana ya kugombea Urais2025. But for sure uchambuzi wako wa leo kuhusu Bandari haujabamba hata
 
Anayepinga uwekezaji wa bandari ni adui wa maendeleo. Mmeendesha bandari wenyewe miaka yote bila tija yeyote zaidi ya rushwa na urasimu tu. Maza akimaliza bandari zifuate airports wape wanaojua wanachokifanya na wenye nyezo za kazi.
 
Naam Dr.slaa mzalendo kabisa

Huyu Samia kwa mara ya kwanza nadiriki kusema ni kiongozi asiyefaa hata kidogo

Kwenye picha kubwa ni asilimia mia moja hajali chochote kuhusu Tanganyika mbaya zaidi wale waliomleta kwenye siasa za Tanganyika wanamuunga mkono kwasababu wanafaidika na maamuzi...
Ndiyo maana bandari za Zanzibar hazimo kwenye huu uchafu
 
Naam Dr.slaa mzalendo kabisa

Huyu Samia kwa mara ya kwanza nadiriki kusema ni kiongozi asiyefaa hata kidogo

Kwenye picha kubwa ni asilimia mia moja hajali chochote kuhusu Tanganyika mbaya zaidi wale waliomleta kwenye siasa za Tanganyika wanamuunga ...
Ndiyo maana bandari za Zanzibar hazimo kwenye huu uchafu
 
Acha tupige deal mkuu , msijali kwenye SGR mkataba tutautafsiri hadi kwa kiswahili ili muelewe ila huu tumeshausaini .
Kwanza miaka mia mbele wewe hutakuepo tena !!
Cheers 😂😂
 
Balozi Dkt. Willibrod Slaa anazungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, leo Juni 13 2023 kuhusu hati ya makubaliano yaliyoingiwa kati ya Tanzania na DP World...
Unaongea mambo mengi, mengine hayana muunganiko, unaharaka sana, unakosea hujajipanga, unatuchanganya, unaonekana kama kuna ka-mkono kasiko onekana kanakokusukuma.
 
Anayepinga uwekezaji wa bandari ni adui wa maendeleo. Mmeendesha bandari wenyewe miaka yote bila tija yeyote zaidi ya rushwa na urasimu tu. Maza akimaliza bandari zifuate airports wape wanaojua wanachokifanya na wenye nyezo za kazi.
Tatizo siyo kupinga uwekezaji, kinachopingwa ni aina ya Mkataba ambao Serikali inaingia na Wawekezaji.
 
Dr.Slaa banaaaa [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]


"Opportunist"....

Pamoja na usomi wake...sijui huwa anafanya kusudi kutochagua maneno ya "staha" ya kidiplomasia ilihali yeye ni MSOMI NA BALOZI?!!![emoji15][emoji15]

Japo hawafanani asilimia zote ila Dr.Slaa hana tofauti sana na Mh.Tundu Lissu....wanapenda sana siasa za "TUG OF WAR" na "kuvabana" kila inapotokea "FURSA ADHIMU"......[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Eti anasema mh.Rais alisaini mikataba 17 na iko "SIRINI" ....

Hivi mikataba yote inayosainiwa huwekwa wazi ?!!!

Dr.Slaa atuambie....alipokuwa balozi wa SWEDEN...Serikali ya JMT iliingia mikataba na YERPI MERKEZ kujenga SGR alielezwa?!!!

Tulielezwa wananchi ?!!!

Dr.Slaa atuambie....alipokuwa balozi SWEDEN....Serikali ya JMT iliingia mikataba na ARAB CONTRACTORS kujenga bwawa la ufuaji umeme la Mwalimu Nyerere alielezwa? Tulielezwa ?!!! [emoji15][emoji1787][emoji1787]

Dr.Slaa banaa.....akiwa balozi kimyaaaaa.....huyu kama yule ndugu kamarada "Slowslow" eeeee?!!![emoji1787]

#MamaAnaupigaMwingiMnooo[emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom