Bandari Salama, bandari ya TPA, itakapopokea meli kubwa ya kihistoria

Bandari Salama, bandari ya TPA, itakapopokea meli kubwa ya kihistoria

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Kishindo kikuu 'Bandari Salama', bandari ya TPA, itakapopokea meli kubwa ya kihistoria. Kaa tayari kujua.

Kuna jamaa kaandika;
"It's our Vessel called Frontier Ace is coming direct from Singapore carrying 4342 units. Accordingly to Vessel Captain tomorrow morning at 0900Lts confirmed will be out Anchorage for waiting berth instruction from Port Control our authority"
 
Frontier Ace, Meli kubwa kabisa ya Magari kuwahi kutia nanga Bandari ya Dar Es Salaam kesho Ijumaa tarehe 8/04/2022 itaandika historia, itakapotia nanga bandarini mapema asbh, moja kwa moja kutoka Japan.

Hii ni kutokana na maboresho makubwa kabisa ya miundombinu yaliyofanywa katika bandari za Tanzania, na hususani Bandari Kuu ya Dar Es Salaam hivyo kuwezesha Meli kubwa kama Frontier Ace kutia nanga kwa Usalama kabisa bila shida yoyote.

Heshima kwa DG Eric Hamissi kwa bidii ya kazi na kufanya kazi bila makeke yoyote.

Hongera sana Mama Samia kwa kuiunga Mkono Menejimenti ya TPA kupitia uwekezaji wa miundombinu na ununuzi wa vifaa hivyo kuwezesha Bandari yetu kuaminiwa na wenye meli wakubwa

Karibu Tanzania FRONTIER ACE
Kazi Iendelee ✌✌

download (1).jpeg
 
Frontier Ace, Meli kubwa kabisa ya Magari kuwahi kutia nanga Bandari ya Dar Es Salaam kesho Ijumaa tarehe 8/04/2022 itaandika historia, itakapotia nanga Bandari ya Dar Es Salaam mapema asbh, moja kwa moja kutoka Japan.

Hii ni kutokana na maboresho makubwa kabisa ya miundombinu yaliyofanywa katika bandari za Tanzania, na hususani Bandari Kuu ya Dar Es Salaam hivyo kuwezesha Meli kubwa kama Frontier Ace kutia nanga kwa Usalama kabisa bila shida yoyote.

Heshima kwa DG Eric Hamissi kwa bidii ya kazi na kufanya kazi bila makeke yoyote.

Hongera sana Mama Samia kwa kuiunga Mkono Menejimenti ya TPA kupitia uwekezaji wa miundombinu na ununuzi wa vifaa hivyo kuwezesha Bandari yetu kuaminiwa

Karibu Tanzania FRONTIER ACE
Kazi Iendelee

View attachment 2179435
Acheni kupamba watu wasiohusika, ukarabati wa pale TPA ulianza muda Sana mwishoni mwa JK na Magu akapokea malengo yakiwa ndio haya ya meli kubwa kutia nanga na kuchochea uchumi na hata wakuu wa bandari by then walipita wengine sio huyu wa Jana eric...au labda kakutuma umfanyie branding?
 
Frontier Ace, Meli kubwa kabisa ya Magari kuwahi kutia nanga Bandari ya Dar Es Salaam kesho Ijumaa tarehe 8/04/2022 itaandika historia, itakapotia nanga Bandari ya Dar Es Salaam mapema asbh, moja kwa moja kutoka Japan.

Hii ni kutokana na maboresho makubwa kabisa ya miundombinu yaliyofanywa katika bandari za Tanzania, na hususani Bandari Kuu ya Dar Es Salaam hivyo kuwezesha Meli kubwa kama Frontier Ace kutia nanga kwa Usalama kabisa bila shida yoyote.

Heshima kwa DG Eric Hamissi kwa bidii ya kazi na kufanya kazi bila makeke yoyote.

Hongera sana Mama Samia kwa kuiunga Mkono Menejimenti ya TPA kupitia uwekezaji wa miundombinu na ununuzi wa vifaa hivyo kuwezesha Bandari yetu kuaminiwa

Karibu Tanzania FRONTIER ACE
Kazi Iendelee

View attachment 2179435
Akili za kilumumba lumumba hizi. Bure kabisa
 
HONGERA CHAWA the great kwa UPUUZI, hivi hujui habari ya vifaa, vitu kupanda bei, UJIO wa meli ya Magari una maana gani? Huku bei ya mafuta pasha kichwa, hongera kwa kuchagua UJINGA....😃😃😬😬😆😆
 
Acha kupotosha kwa muda aliokaa Eric pale TPA kamwe asingeweza kuboresha hiyo miundombinu.

Bali ukweli ni huu maboresho yote unayoyaona hapo TPA ni moja ya maamuzi bora kabisa kufanywa na Hayati Magufuli kwa kutenga fedha za kufanya maboresho ya miundombinu yote ya bandari yetu pendwa ya Dar es Salaam.

Wakati mwingine hata kama tuna chuki na mtu lakini tumpe credit kwa aliyoyafanya.
 
Hayo magari yatagawiwa bure?
Shangaa na wewe bwashe; utafikiri hayo magari yatarudishia nchi ktk uchumi wa kati chini.
Bandari ya DSM imekuwa ikiingiza shehena kadhaa ya mizigo ukiwemo ya magari kupitia Meli hizihizi. Leo hii kuna specialty gani ya hii meli hadi tuharibiane swaumu kiasi hiki?
Uchawa ni mzigo nchi hii.
 
Kutua kwa meli kubwa bibsawa. Ila kunahitajika mambo ya ziada ambayo yangenufaisha nchi yetu kiulaini kabisa bila makeke. Pamoja na sheria kuwepo. Kama ningekuwa nini ningerekebisha baadhi ya mambo yafuatayo.
1. Ningeacha kutoza customs warehouse rent, maana tayari storage inatozwa na tpa.
2. Ningeruhusu wateja wanaokuja kuchukua magari yao na wakanunua mizigo kariakoo waibebe kwa uhuru ili mradi wawe na efd receipts. Kwenye hili uchumi wa maduka yetu ungeongezeka sana.
3. Ningepunguza usumbufu wa askari barabarani kwa kuweka vituo maalumu vya ukaguzi kama vigwaza njiani bila haja ya kusimamishwa kila mahali.
Usumbufu huu ungehusu pia malori yanayobeba mizigo kwenda nje ya nchi.
4. Ningehakikisha pale bandarini kunakuwa na mazingira mazuri ya mawakala wanaotoa mizigo. Mawakala hawana usafiri wa haraka bandarini. Ucheleweshaji wa utayarishaji wa Ankara za kulipia malipo ya bandari.
5. Ningehakikisha malipo yakishafanyika ya bandari basi kutolewe masaa 24 ili kutoa mzigo huo bandarini. Tofauti na sasa ambapo wakala akilipia saa 5 usiku basi ikifika saa 6 usiku inahesabiwa kuwa ni siku nyingine.
6. Ningeruhusu pale mzigo mkubwa unapolipiwa kabla ya siku za storage kuanza basi mzigo huo uendelee kutolewa mpaka uishe bila storage kuliko utaratibu wa sasa ambapo kwa mfano kama kontena 100 zimelipiwa kabla ya storage, wakala akaanza kuingiza magari kupakia, siku ya storage ikifika kontena zilioko bandarini zinahesabiwa storage. Haina tija yoyote.
 
Back
Top Bottom