Bandari ya Bagamoyo: Waziri Mwambe asema Wachina walisema Dar hadi Pangani, na sio Mtwara hadi Tanga

Bandari ya Bagamoyo: Waziri Mwambe asema Wachina walisema Dar hadi Pangani, na sio Mtwara hadi Tanga

Naunga mkono ujenzi wa bandari kubwa Bagamoyo Ila napinga kwa nguvu zote sharti la kuendeleza na kuboresha bandari zetu zote nchini kwaujumla wake.

Huo utakuwa ni ukoloni wa hatari na wa Hali ya ju kabisa .
 
Leo Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Geofrey Idelphonce Mwambe, amefafanua kuhusu uwekezaji wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo,

amefafanua mambo mengi lakini nimepata ukakasi niliposikia hii sehemu ya ufafanuzi wa waziri ambapo namnukuu "Kuna eneo moja niliweke vizuri sana ilizungumzwa kuwa wale wachina wanataka kusiendelezwe bandari yoyote ile kutoka Mtwara mpaka Tanga, sio kweli, sijui hayo maneno yalitokea wapi" Waziri Mwambe. Kama inavyoonekana hapa kwenye video 👇

Lakini hii hapa ni video ya Hayati Rais Magufuli akiongelea mradi huo na kipengele kilichotaka kusiendelezwe bandari yoyote ile kutoka Mtwara mpaka Tanga inamaana Hayati Rais Magufuli alitudanganya ? au Waziri ndio ametudanganya ?
 
Kama Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo hautaathiri Maendeleo ya Bandari za Dar,Tanga na Mtwara sioni ni sababu gani inazuia isijengwe.
Tatizo linaanzia hapa, mtu anapokana msimamo wa serikali kwa lugha nyepesi, watu wanashindwa kuwa na imani na yale tunayoambiwa

SERIKALI YAMKANA HAYATI MAGUFULI

Waziri Mwambe amesema haya ''Kuna jambo niliweke sawa ilisemwa kuwa wachina walisema kusiendelezwe bandari yoyote kutoka Mtwara hadi Tanga,sio kweli. Hayo maneno sijui yalitoka wapi,...
Katika mambo machache ambayo nilimuunga mkono dhalim mwendazake ni kuukataa huu mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo. Naona Msoga Gang wameurudisha tena kwa mbwembwe nyingi.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Sasa hivi wanaenda kwenye majadiliano wakati walishaweka jiwe la Msingi ili kuanza ujenzi.
Sijui wanajadiliana nini ikiwa walitaka kuanza ujenzi
 
Kwa lipi hilo hadi jeshi liingilie kati? Ukishashiba ugali ni rahisi sana kuja kutapika hapa JF, Ni wakati sasa Samia apige pini hii mitandao ya jamii kama mtangulizi wake, watapikaji (bila ushahidi wowote) wamekuwa wengi sana, jobless....
Unaliogopa jeshi kwa sababu unajua watakubinya mbupu wakiamua kuwashughulikia wanasiasa uchwara.

Na itapendeza sana. Nyie vinyago mnaoitafuna nchii bila kuangalia mustakabali wa kizazi cha sasa na cha baadae ni vyema mkabinywa kweli kweli.

Gesi mmeuzia wachina, miradi mikubwa ya umeme mnaihujumu. Madini yote mmeuzia wazungu. HAPANA.

Hapa panahitaji dawa. Haiwezekani hatima ya nchi iangamizwe na kundi la watu wasiozidi hata mia moja.
 
Kikwete alikuwa kirusi kwa nchi hii.

How comes masharti kama hay yapo hapa nchini?

Akija mwigine akasema awekeze kwenye kilimo cha mpunga na hakuna mtu mwingine kulima kwa miaka tisini si tumekwisha?.
We yule Kikwete hata ukimuangalia usoni unaona yuko timamu??

Just look at him in the face and tell me if he is not mentally unfit!

Muone anavyocheka tu vile!
 
Kumbe kusiendelezwe? hapo sawa nilidhani wasifanye kabisa biashara,Kuendeleza means expansion ila renovation lazima iwepo kama nayo wamezuia basi hawatutakii mema.
 
Kwa lipi hilo hadi jeshi liingilie kati? Ukishashiba ugali ni rahisi sana kuja kutapika hapa JF, Ni wakati sasa Samia apige pini hii mitandao ya jamii kama mtangulizi wake, watapikaji (bila ushahidi wowote) wamekuwa wengi sana, jobless....
Ukute unaishi kwa shemeji yako
 
Back
Top Bottom