Bandari ya Bagamoyo: Waziri Mwambe asema Wachina walisema Dar hadi Pangani, na sio Mtwara hadi Tanga

Bandari ya Bagamoyo: Waziri Mwambe asema Wachina walisema Dar hadi Pangani, na sio Mtwara hadi Tanga

Nina hakikisha huo miradi kama ingekuwa marehemu magu katuingiza chaka na wanavyopenda kumkosoa wangeweka hadharani hayo masharti nafuu ila kwa vile jamaa alikuwa sahihi na hiyo point aliyesimamia nina uwakika 90% yuko sahihi

Maana ni very weak wanakosea wala huo sawa dar mpaka pangani pima kijiographia uone hapo utaona bandari ya tanga ndani na ya dar kwani pangani ni pwani si ni tanga iyo

Watu walishachukua advance hapo hamna kitu utawaeleza
 
Hii hoja ina uzito mkubwa katika biashara ya usafirishaji wa mizigo kwa meli kimataifa. Mwenye maamuzi ni mwenye meli wakati mwenye bandari anasubiri kupokea/kupakua tu mizigo.

Tunakubaliana kuwa China inaongoza katika biashara ya mizigo katika ukanda wa Afrika Mashariki, Kusini na Kati. Hivyo, watakapomaliza kujenga bandari ya Bagamoyo upo uwezekano wa mizigo mingi kutoka China kupokelewa hapo Bagamoyo. Bila shaka itakuwa mizigo mingi kwa ajili ya Tanzania na majirani zake kama Congo DRC, Zambia na malawi. Kama hali itakuwa hivyo bandari ya Dar , kwa mfano, itapokea mizigo kutoka wapi kama siyo kufa taratibu. Bagamoyo inaweza kuwa "mtego wa panya" kwa bandari zote za Tanzania zikiwemo bandari za Zanzibar. Hii ni hoja ya kibiashara, ni busara tutafakari kwa kina.
Una akili sana hapo wanaoelekeza meli zote kutoka kwao zifikie hapo huko kwingine empty na ndo zitakuwa taratibu

Watu wamekalia ushabiki tu magu aliona mbali sana
 
Kwanini tusiendeleze huu ndio ujibga wa kitanzania taifa la nje kutuzuia maendeleo yetu
 
Wachina wamejifunza na historia. Walivyowekeza kwenye TAZARA, nchi za Magharibi wakaja wakatia fitna na kufadhili ujenzi wa barabara ya Dar - Tunduma; mwisho wake imeua TAZARA. Wana uhakika gani kuwa baada ya kujenga Bagamoyo port, USA hawatakuja na bandari ya Pangani?

Anyways, sio kazi ya Mchina kulinda maslahi ya Mtanzania. Ni kazi yetu.
Hamna kitu kinaweza ua reli maana reli ni njia rahisi kusafirisha mizigo mingi na mizito.. barabara ni njia ya kusafirisha watu ila reli ni ya mizigo.
 
MaCCM yanapingana yenyewe sasa hivi. Yaani ni unafiki uliokubuhu.
 
Tunapata uchungu sababu sisi si wachina, wachina sio sisi na watatusumbua sana kuwa na hiyo bandari wakiwa mabosi zetu kwa miaka mingi.

Ila Binadamu hatukupaswa kufungwa na suala la kuzaliwa, kupewa kabila sijui utaifa n.k tulipaswa tu tuwe binadamu, tutawale viumbe wengine kwa uhuru amani tukiwa na serikali moja.

Mipaka, utaifa, ukabila ni mambo yetu tuliyojitungia binadamu. Dunia haina mipaka ina nchi kavu na bahari, viumbe hai na visivyo hai. Tungejiacha tu bila kujali huku ni kwa waarabu, kule kwa wazungu.

Siku tukipata ugeni kutoka sayari nyingine tutafunguka sana.

Kwa sasa hawa wachina watatunyoosha.😁😁
 
SERIKALI YAMKANA HAYATI MAGUFULI

Waziri Mwambe amesema haya ''Kuna jambo niliweke sawa ilisemwa kuwa wachina walisema kusiendelezwe bandari yoyote kutoka Mtwara hadi Tanga,sio kweli. Hayo maneno sijui yalitoka wapi, kilichosemwa ni kwamba kuanzia Dar es Salaam hadi Pangani kusiendelezwe bandari''

Nimeona na kusikia maneno ya waziri Mwambe kuhusu ujenzi wa bandari ya bagamoyo na kilichosemwa sio Mtwara hadi Tanga bali ni Dar hadi Pangani.

Kwanza namkumbusha waziri Mwambe kuwa Pangani pia ipo Tanga.

Pia hata kama ni Dar hadi Tanga, pia sio masharti mazuri. Kwanini ndani ya nchi yako upangiwe uendeleze wapi na wapi usiendeleze?

Sababu waliyotoa ni kupata ushindani endapo bandari zitaendelezwa ukanda huo, Ila mbona wao wanakuja kuleta ushindani kwa bandari ya Dar?

Hilo lilikua moja ya sharti, vipi kuhusu mengine mbona waziri umekua kimya?

Na-support ujenzi wa bandari ila tutangulize maslahi ya taifa kwanza na naomba hata hayo masharti ya kutoendeleza Dar hadi Tanga msiyakubali.

Kazi iendelee
Huyo mwambe naye anasema ujinga. Sasa utaweza kukubali bandari ya dar iache kuendelezwa?
 
Kwanza hiyo bandari si lazima kukopa kwa masharti yasiyokua na tija kwa taifa. Tunaweza pia kuijenga wenyewe kwa taratibu.
 
Renovation ya bandari ni expansion. Au unafikiri renovation ya bandari ni kupaka rangi ofisi?

Hapana Renovation ni kufanya modification ya kwenye uchakavu na kurepair! Expansion ni kuongeza capacity eg kama capacity ni ya kupokea meli 10 kwahiyo ukifanya expansion utakuwa na uwezo wa kupokea zaidi ya meli 10 ila ukipaka rangi ukirepair miundombinu capacity inabaki ile ile ya meli 10.
 
Awamu ya nne walishapiga % zao kwahyo ni lazima wapambane mradi ufanyike maana hawawezi kurejesha hizo walizochukua ukizingatia na jiwe la msingi walishaweka kuashiria mradi kuanza
 
Yawezekana kukawa ndiko kwenye mazuzu mengi.
Mazuzu jeshini wapo, sawa na huku uraiani. Usisahau hata hivyo kwamba wataalamu (professionals) wa kila fani wapo pia jeshini.

Magufuli kwa miaka yake michache kajitahidi sana kufanya yaliyoshindikana kwa watangulizi wake. Mzee Mwinyi amewahi kushuhudia hili. Lakini mara nyingi tulimsikia akisema nchi imechezewa sana akishindwa kuwataja au kuwachukulia hatua hao walioichezea nchi.

Jeshi likikamata nchi japo kwa mwaka 1, nina hakika hao wanaosemekana kuichezea nchi wataanikwa hadharani na kuchukuliwa hatua stahiki.

Umewahi kujiuliza, pamoja na kusemwa kuwa baadhi ya pesa ya escrow kusombwa toka benki kwa magari ya Ikulu mpaka leo haijulikani nani alichukua pesa ile?!
 
Eneo la mradi serikali iwajibike kuwafidia wananchi watakaoondolewa halafu limilikshwe kwa mradi.
 
Mazuzu jeshini wapo, sawa na huku uraiani. Usisahau hata hivyo kwamba wataalamu (professionals) wa kila fani wapo pia jeshini.

Magufuli kwa miaka yake michache kajitahidi sana kufanya yaliyoshindikana kwa watangulizi wake. Mzee Mwinyi amewahi kushuhudia hili. Lakini mara nyingi tulimsikia akisema nchi imechezewa sana akishindwa kuwataja au kuwachukulia hatua hao walioichezea nchi.

Jeshi likikamata nchi japo kwa mwaka 1, nina hakika hao wanaosemekana kuichezea nchi wataanikwa hadharani na kuchukuliwa hatua stahiki.

Umewahi kujiuliza, pamoja na kusemwa kuwa baadhi ya pesa ya escrow kusombwa toka benki kwa magari ya Ikulu mpaka leo haijulikani nani alichukua pesa ile?!
Jeshi limejengwa kwa nidhamu ya kuogopa viongozi kuliko walivyo raia.
Mawazo yao ni ya kutumika zaidi bila kujali kwa faida au hasara (wanaweza kutumiwa kuiba kura/uchaguzi na wakafanya kwa nguvu zote. Itategemea wana viongozi wenye common sense na weledi au hapana.
Jamii corrupt huzalisha jeshi la ajabu na lisilotegemewa sana.
Magufuli alikuwa na majeshi aliyoyategemea, kuyapenda na kuyapendelea kwa hali na mali.
Mwenyewe alifumbia macho escrow kama vile wahusika wa kuidhinisha hawakuwa serikalini.
Kivuko chenye utata akakificha jeshini.
Jiulize pia kwa nini?
 
Hii nchi bila jeshi kutunusuru tumekwisha. It's time for the army to intervene.
Jeshi?
Uliwahi kuishi kwenye nchi inayotawaliwa kijeshi?
Hivi jeshi likitawala nchi hii utapata nafasi ya kuja kumkosoa kiongozi hapa?

Magufuli hakuwa mwanajeshi lakini alikuwa na fikra za kuzima mitandao ili asikosolewe.
Hali itakuwaje chini ya jeshi?
 
Hii nchi bila jeshi kutunusuru tumekwisha. It's time for the army to intervene.
Watu wa aina yako hata tairi ya gari liki basti mnalala chini kwa hofu mkihisi majambazi,sasahivi umevimbiwa maharage ya mbeya unaombea jeshi liingilie kati kwenye jambo lakipuuzi!
 
Back
Top Bottom