Bangi: Kwanini wengine wanaifurahia, lakini wengine hupata madhara makubwa?

Bangi: Kwanini wengine wanaifurahia, lakini wengine hupata madhara makubwa?

Issue kubwa hapo ni tolerance, watu wanatofautiana kuna wengine wanapiga fresh na haiwapeleki puta lakini wengine wakiigusa tu basi ni balaa kubwa , mfano pia pombe wapo wenye uwezo wa kunywa pombe nyingi bila shida yeyote na mambo yake mengine yakaenda vizuri lakini wengine wakigusa kidogo tu basi hata kuamka hawawezi na shughuli zao zinaenda mrama
 
Akili hauna.,ndo maana nikakupa taadhari
Tahadhari,
Pia andika ndio na sio ndo,

Sasa wewe hata kuandika lugha yako tu kwa ufasaha hujui,

Unaweza kukuta huko kwenye familia yenu,wewe ndio unaonekana una akili,ndio akili yako ikakuongopea kua una akili mpaka nje ya familia yako!
 
Dogolasi wangu ye ganja kwake km sigara tu 24/7.
Bia 2 ukimpa anaweza kufa.
 
Bangi ilikua mwanzo wa matatizo mwanzoni wakati tunaanza kuvuta niliona nilichelewa wp lkn siku zinavyozid kwenda ndyo nazid kuharibikiwa bangi ilinifanya niwe naitegemea hasa usiku nilikua sipati usingizi mpaka nivute bangi na nikiamka usiku wa manane nilikuwa siwezi kulala mpaka nivute tena bangi iliniletea anxiety ikifika jioni nawaza kama nipo sehemu ambayo siwezi kuvuta basi hiyo siku nitakaa macho hadi asubuh bila kupata usingizi nilikua nakaa hata siku mbili bila kupata usingizi kama sijavuta ilinitesa sana nashukuru niliacha 2023 kuvuta bangi ile hali ya kukosa usingizi ikanifanya nihamie kwenye tungi sasa nimeacha vyote bangi sivuti,pombe sinywi,sigara sivuti,punyeto sipigi naomba ile hali isinirudie tena yalikua mateso
 
Bangi ni kama pombe tuu, ukiona huiwezi acha. Tukiwa shule form three ujana ujana wa kujaribubkila kitu, kuberi, pombe, fegi, ugoro, kuna siku mpuuzi mmoja si akatupeleka shamba la miwa, kumbe katikati wanalima bange.
Tukakuta wajuba wanakoka, ebana si tukajaribu pafu moja moja. 😁

Mimi nilihisi kama kichwa kinapasuka na nina paa mawinguni.
Jamaa yangu mmoja yeye aliqnza kucheka mpaka anagalagala chini, anasema eti tupo uchi. 😁
Mkali mmoja na hesabu ni marehemu wa kuitwa Carlos, yeye alianza kutembea anaruka ka.a anaruka mitaro hivi. Tukamuuloza vipi, akasema kuna mitaro mingi kinoma wazee. Jamaa yangu Henry yeye alitabasamu sana siku hiyo, akawa anasema twendeni tukalime shamba la shule wazee. 😁
Ilibidi wale mabigi, watushike kwanza na kutulazimisha kuingia kwenye maji baridi mtoni na kutupa miwa mingi sana tule. 😁
Baada kama ya lisaa ndio tukawa sawa tena, tukarudi bwenini kimya kimya.

Mi nakumbuka nililala usingizi nilikuja amka mchana kesho yake. Naamka sio njaa ile, sijawahi sikia njaa kama ile tena.
Sijagusa kaya tena maisha yangu yote. 😁

Bangi na Maji ni marafiki wakubwa sana, Bangi stimu yake ni Miwa. Ukiona stimu imepanda sana wee chukua muwa mkubwa anza kula, kadiri unavyoula ndio bangi inakata.
Au kama ni mtoni, we jitupie, ukikaa dakika 15 utaona stimu inakata na unatoka ukiwa poa tuu.
Mvuta bangi yeyote akivuta bangi, lazima akaoge au utafune muwa.
Miwa tena? 🤣🤣🤣
 
Nachojua bangi yenyewe sio hizi takataka za buguruni na keko machungwa haina madhara yoyote zaidi ya kukuweka uwe high .

Nilitumia bangi mara ya kwanza 2002 nikiwa na work mate ,na hakika haikuwa bangi bali haya matakataka ikaniabisha ofisini na kwenye familia yangu .

Nikairudia tena ili nijue kama kweli ilikuwa bangi yenyewe au ni kichwa changu kina matatizo mwaka 2019 pale Harbow south Africa haikunifanya chochote zaidi ya kunipa stimu kali na kujiona mimi ndiye japo sikurudia tena sababu nimebobea kwenye ukemia wa pombe hivyo ilikuwa ni lazima niamua naondoka na kipi ,nikaamua kuondoka na pombe sababu sipendelei sana vitu vya moshi moshi.

Nafinalize kwa kusema bangi yenyewe haina shida na kichwa chochote cha mtu hata kiwe kikubwa au kidogo vipi ila mashudu ya bangi ndiyo yenye matatizo .

Ahsante Seran ila nachojua mvuta bangi na wale wa matakataka ni watu real sana sio wanafiki wala masnitch wamenyooka ,moja ni moja na mbili ni mbili .

Heshima yako ndwete hapo 44 kj
Aww kumbe kuna nyingine si mchezo! Kwakweli wako peace sana hawanaga uchawi!👌🏽
Fanya mpango nionje hiyo ya kusini mkwe😅
 
Issue kubwa hapo ni tolerance, watu wanatofautiana kuna wengine wanapiga fresh na haiwapeleki puta lakini wengine wakiigusa tu basi ni balaa kubwa , mfano pia pombe wapo wenye uwezo wa kunywa pombe nyingi bila shida yeyote na mambo yake mengine yakaenda vizuri lakini wengine wakigusa kidogo tu basi hata kuamka hawawezi na shughuli zao zinaenda mrama
Tolerance? Labda unieleweshe kidogo hapo mkuu! Tolerance ina relate vipi na wengine kugusa tu ulevi shughuli zao zinaenda mrama?
 
Bangi hukuongezea kile ambacho unacho. Haibadili kitu. Kama una uchizi uliopelea bange inakupeleka kwenye uchizi kamili. Kama unaakili nzuri bangi inaziboresha zaidi ya zilipoishia. Onyo usivute bangi kama unaakili %100 maana itaziongeza ziwe 130%
 
Hola! 🙋🏽‍♀️
Ningependa kujua maoni yenu kuhusu bangi(420) pia huitwa weed, marijuana, ganja, n.k..

View attachment 3563320

Kuna watu wanasema wanaitumia kwa kujisikia vizuri, kupunguza stress au hata kama dawa. Pia nimesikia kwamba baadhi ya watu wanaofanya kazi ngumu au zenye msongo mkubwa (kama hospitali au sehemu za hatari hutumia ili kujituliza.. madakataria (theatre,morgue)

View attachment 3563321

Lakini kwa upande mwingine, kuna watu wanaosema bangi inaweza kusababisha uraibu (addiction), kuchanganyikiwa akili, au hata mtu “kuwa kama amerukwa na akili” hasa akitumia kupita kiasi. Wengine pia wanasema katika familia zao ni mwiko mkubwa, na mtu akianza kuitumia anaweza kuharibika kabisa.

View attachment 3563322

Maswali yangu ni:

* Kwa nini watu wengine wanaweza kuitumia bila matatizo makubwa, lakini wengine hupata madhara makubwa?

* Je, ni kweli bangi inaweza kuwa dawa au ni hatari zaidi kuliko faida zake?

* Ni mambo gani yanayofanya mtu awe katika hatari ya uraibu au matatizo ya akili?

Haya ni baadhi ya majinaa tofauti ya bangi yanayotumika:

  • Bangi
  • Weed
  • Marijuana
  • Ganja
  • Herb
  • Grass
  • Pot
  • Dope
  • Mary Jane
  • Joint (wakati imevutwa kama sigara)
  • Spliff
  • Hash / Hashish
  • Skunk
  • Kush
  • Blaze (slang ya kutumia)

View attachment 3563324
 

Attachments

  • 7dacb7a46c8c139ddee3acddcdff0efb.mp4
    3.2 MB
Back
Top Bottom