Bangi: Kwanini wengine wanaifurahia, lakini wengine hupata madhara makubwa?

Bangi: Kwanini wengine wanaifurahia, lakini wengine hupata madhara makubwa?

Kutumia mara kwa mara pombe ni jambo mojawapo la kuongeza tolerance level lakini Kuna watu by nature tolerance level tayari Iko chini, unashangaa mtu kanywa bia mbili tu kashawehuka au kuanza kujisikia vibaya. Mfano pia Wajapan, Wachina na Wakorea hawawezi kunywa pombe kwa kiwango kikubwa sana kwa sababu hulewa mapema sana(Asian flush).
Duhh beer mbili! Na kuna watu wanakata crate😳
 
Nashukuru sina hamu nayo tena na siipend tu inanifanya nakuwa km nimenyeshewa mvua hata sigara nayo ukiivuta mwili unaishiwa nguvu ghafla bora kufanya vaping na pombe
Vaping ni hatari zaidi nasikia! Kukufanya uwe hivyo nahisi ni unaitumia ukiwa katika state ya namna hiyo! Ivute ukiwa na vibe utaona utofauti wake🤔
 
Hola! 🙋🏽‍♀️
Ningependa kujua maoni yenu kuhusu bangi(420) pia huitwa weed, marijuana, ganja, n.k..

View attachment 3563320

Kuna watu wanasema wanaitumia kwa kujisikia vizuri, kupunguza stress au hata kama dawa. Pia nimesikia kwamba baadhi ya watu wanaofanya kazi ngumu au zenye msongo mkubwa (kama hospitali au sehemu za hatari hutumia ili kujituliza.. madakataria (theatre,morgue)

View attachment 3563321

Lakini kwa upande mwingine, kuna watu wanaosema bangi inaweza kusababisha uraibu (addiction), kuchanganyikiwa akili, au hata mtu “kuwa kama amerukwa na akili” hasa akitumia kupita kiasi. Wengine pia wanasema katika familia zao ni mwiko mkubwa, na mtu akianza kuitumia anaweza kuharibika kabisa.

View attachment 3563322

Maswali yangu ni:

* Kwa nini watu wengine wanaweza kuitumia bila matatizo makubwa, lakini wengine hupata madhara makubwa?

* Je, ni kweli bangi inaweza kuwa dawa au ni hatari zaidi kuliko faida zake?

* Ni mambo gani yanayofanya mtu awe katika hatari ya uraibu au matatizo ya akili?

Haya ni baadhi ya majinaa tofauti ya bangi yanayotumika:

  • Bangi
  • Weed
  • Marijuana
  • Ganja
  • Herb
  • Grass
  • Pot
  • Dope
  • Mary Jane
  • Joint (wakati imevutwa kama sigara)
  • Spliff
  • Hash / Hashish
  • Skunk
  • Kush
  • Blaze (slang ya kutumia)

View attachment 3563324
Mkuu wewe upo kwenye kundi lipi la watumiaji kati ya uliyoyataja?
 
Bangi ni kama pombe tuu, ukiona huiwezi acha. Tukiwa shule form three ujana ujana wa kujaribubkila kitu, kuberi, pombe, fegi, ugoro, kuna siku mpuuzi mmoja si akatupeleka shamba la miwa, kumbe katikati wanalima bange.
Tukakuta wajuba wanakoka, ebana si tukajaribu pafu moja moja. 😁

Mimi nilihisi kama kichwa kinapasuka na nina paa mawinguni.
Jamaa yangu mmoja yeye aliqnza kucheka mpaka anagalagala chini, anasema eti tupo uchi. 😁
Mkali mmoja na hesabu ni marehemu wa kuitwa Carlos, yeye alianza kutembea anaruka ka.a anaruka mitaro hivi. Tukamuuloza vipi, akasema kuna mitaro mingi kinoma wazee. Jamaa yangu Henry yeye alitabasamu sana siku hiyo, akawa anasema twendeni tukalime shamba la shule wazee. 😁
Ilibidi wale mabigi, watushike kwanza na kutulazimisha kuingia kwenye maji baridi mtoni na kutupa miwa mingi sana tule. 😁
Baada kama ya lisaa ndio tukawa sawa tena, tukarudi bwenini kimya kimya.

Mi nakumbuka nililala usingizi nilikuja amka mchana kesho yake. Naamka sio njaa ile, sijawahi sikia njaa kama ile tena.
Sijagusa kaya tena maisha yangu yote. 😁

Bangi na Maji ni marafiki wakubwa sana, Bangi stimu yake ni Miwa. Ukiona stimu imepanda sana wee chukua muwa mkubwa anza kula, kadiri unavyoula ndio bangi inakata.
Au kama ni mtoni, we jitupie, ukikaa dakika 15 utaona stimu inakata na unatoka ukiwa poa tuu.
Mvuta bangi yeyote akivuta bangi, lazima akaoge au utafune muwa.
 
Nachojua bangi yenyewe sio hizi takataka za buguruni na keko machungwa haina madhara yoyote zaidi ya kukuweka uwe high .

Nilitumia bangi mara ya kwanza 2002 nikiwa na work mate ,na hakika haikuwa bangi bali haya matakataka ikaniabisha ofisini na kwenye familia yangu .

Nikairudia tena ili nijue kama kweli ilikuwa bangi yenyewe au ni kichwa changu kina matatizo mwaka 2019 pale Harbow south Africa haikunifanya chochote zaidi ya kunipa stimu kali na kujiona mimi ndiye japo sikurudia tena sababu nimebobea kwenye ukemia wa pombe hivyo ilikuwa ni lazima niamua naondoka na kipi ,nikaamua kuondoka na pombe sababu sipendelei sana vitu vya moshi moshi.

Nafinalize kwa kusema bangi yenyewe haina shida na kichwa chochote cha mtu hata kiwe kikubwa au kidogo vipi ila mashudu ya bangi ndiyo yenye matatizo .

Ahsante Seran ila nachojua mvuta bangi na wale wa matakataka ni watu real sana sio wanafiki wala masnitch wamenyooka ,moja ni moja na mbili ni mbili .

Heshima yako ndwete hapo 44 kj
 
Huu uz una harufu ya bangi pepo tokaaa mamame.... Ila bang nzur sana nilishawah kwenda kwenye intavuu moja watu mia mbil nafas 50 nikasema usinitanie nikavuta bang huyo kweny inatavuu fika pale naulizwa unauzoefu wa miaka mingap kwenye kaz, nikamjibu kwahyo asie na uzoefu wakafanye nini? Umesoma mpaka darasa langap nikajibu kwan alieanzisha a e i o u nae alisomea wapi? So sikujibu swal lao hata moja wakabak wananiangalia tu ila end the day nikasikia tu jamaa anajiamin huyu ndio safi nikapata kaz ya kuwa mfanyakaz wa kusimamia wafanyakaz wanaofanya kazi za wafanyakaz
 
Back
Top Bottom