BANK-M mikononi mwa Firoz Bayi, Kutakatisha Pesa za wa siasa

Mifano Mingine ya Maandamano Yaliyoleta Mabadiliko ya Serikali
    • Mapinduzi ya Misri (2011): Maandamano makubwa katika Uwanja wa Tahrir yalimng'oa madarakani Rais Hosni Mubarak aliyekaa madarakani kwa miongo mingine mitatu.
    • Mapinduzi ya Sudan (2019): Maandamano ya mitaani yaliyoongozwa na wananchi na vijana yalimwondoa madarakani Rais Omar al-Bashir aliyekuwa anatawala kwa muda mrefu.
    • Mapinduzi ya Romania (1989): Maandamano na ghasia zilizofuata zilimwangusha kiongozi wa kikomunisti Nicolae Ceaușescu.
Sababu za Kufaulu kwa Maandamano Haya
    • Ushiriki mpana: Idadi kubwa ya wananchi kutoka matabaka mbalimbali walijitokeza mitaani kwa pamoja.
 
Maandamano ya Sudan siyo mfano mzuri wa kuutumia. Wamemtoa Omar Bashir, then nini kinaendelea?
 
Ningelikuwa mimi, ningelikuwa na akiba ya maneno.
 
Da Mange Kasema.
 
Sababu kubwa ni MIND-SET kabla ya huko kushiriki.. huwezi fananisha akili za watu kwenye hizo nchi na ng`ombe zilizojaa Malawi..
Kujielewa wewe binafsi kunaanza halafu ndo uyajue mazingira yaliyokuzunguka,,,

Mfano hao Sudan ambao walianza purukushani za mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tokea 1955 huwezi wafananisha na walioishi kama mifugo kwa miaka 60 chini ya akili za mtu mmoja.
 
Wahuni wote wanarudishwa. Hii benki kipindi cha msoga ilikuwa imebandika bango kubwa sana just before salendar bridge ikijivunia kuwa na "assets" za matrilioni ya shilingi. Kumbe ilikuwa kichaka cha kutakatisha pesa.
 
October 29 watu hawakuandamana? Idadi ya watu waliotoka kupinga ilikua kubwa .
Nepal na sehemu nyingine baada ya wananchi kutoka tuliona vyombo vya ulinzi na usalama vilitoa sapoti .
Nembu nionyeshe sapoti haa ndogo tu iliyotolewa na Hawa wa kwetu waliopo kwenye mfumo.
Captain tesha alitoka hadharani kupinga na akasema hadharani jk akamatwe , mpaka Leo hatujui yuko wapi na hakupewa sapoti yoyote Ile !

Hawa kina brittanica na kundi lake they have nothing to offer zaidi ya umbea , zero plan miaka na miaka ni umbea tu " mara kwenye kikao nchimbi kawakazia macho" hii inasaidia Nini zaidi ya umbea tu
 
Wameuliwa watu zaidi ya 2000 still unasema mindset ya watu wa Malawi ! Hawa wananchi wa Malawi hawana bunduki wala mabomu silaha pekee waliyonayo ni support kutoka kwa watu waliopo kwenye madaraka ambao wanaojinasibisha kwamba wanachukia kinachoendelea na wananchi walikua wataipata support wakitoka na wakatoka cha ajabu kulikua na zero support!

Mpaka Leo hakuna kilichofanyika pamoja na maafa yote yaliyotokea !
Unamlaumu mwanachi wa kawaida mama ntilie au bodaboda ambae hana mamlaka ama nguvu yoyote zaidi sana ameshuhudia wenzake wakifa kama kuku na hakuna Cha ajabu kilichotokea.
 
Kwani hizo bunduki huko Sudan na Egypt hazipo?
 
Kwani hizo bunduki huko Sudan na Egypt hazipo?
Swali lako linalenga Nini??
Sudan baada ya protest tuliona support kutoka jeshini na al Bashir akatolewa.
Huku kwetu protest ilikuepo then kulikua na support yoyote kutoka military au sehemu yoyote?
Wananchi hawawezi kuseize power on their own Bila ya support kutoka kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Huku kwetu ndo kwanza muuaji akaenda kuapishwa huko huko palipoitajika support.
 
JK aliwahi kusema najaribu kunukuu...ni kheri chadema washinde uraisi si TAL kuwa bungeni.
 
Sudan support ya jeshi ilikuja baada ya wananchi kuonyesha consistency kwenye jambo lao, hawakutoa support kirahisi tu ndugu.

Halafu hiyo Sudan unayoiongelea wananchi wake utafananisha kweli na wamalawi? halafu jiulize nchi gani ya kusini mwa Jangwa la Sahara ambao waliwahi kufanya hilo? kwasababu waarabu na wasudan(a.k.a waarabu weusi) huwezi fananisha na wamalawi..

halafu kila nchi ina njia zake ambazo serikali na taasisi zake zinaendeshwa .. kwamba unataka jeshi la malawi kuja na kitu fulani hivi unachofikiri?... si rahisi ,,, kuna theory za kwenye makaratasi na real life practice..
 
Huko Egypt na Sudan kulikua na military intervention ( military support) baada ya wananchi kujitokeza .

Consistency gani unaitaka hapa ya wananchi?? Almost watu 2000 wamekufa halafu unajificha kwenye kichaka Cha consistency! Sudan hata watu 900 hawakufika lakini military iliingilia kati huko Egypt penyewe idadi ya watu waliokufa hailingani na yaliyotokea nchini .

Njia za serikali inavyoendeshwa hapa kwetu ni failed methods, ndio nataka jeshi na TISS kuja na njia nayofikiri ,kushinda kuja nazo inaonyesha tayari ni ma failure wote waliopo huko that's why wanakuja na hichi anachokileta britanicaa Kila siku na Kila mwaka " gossip" umbea usiokuwa na tija kwa taifa.

Tesha hakupewa support na hatujui alipo mpaka sasa, Lissu hana support mpaka sasa , gwajima hakupewa support na watu wengine wengi kina polepole kina mzee msuya . Hawa wote wameonyesha ujasiri wa kutoka na kuongea wazi but sadly wamebaki lonely with zero support.

Kwa hayo yote tunaweza kusema sasa JK ,Rostam na Hawa puppets wengine they own TPDF and TISS !
Vyombo vya ulinzi na usalama ni Mali ya mtu mmoja au tuseme ccm mtandao.
 
Wahuni wote wanarudishwa. Hii benki kipindi cha msoga ilikuwa imebandika bango kubwa sana just before salendar bridge ikijivunia kuwa na "assets" za matrilioni ya shilingi. Kumbe ilikuwa kichaka cha kutakatisha pesa.
Hivi sio mnachanganya M bank (iliyohusishwa na marehemu Mkono)na i&M bank?
Au mimi nimechelewa kuifahamu hii ya sasa!
 

ndiyo Sudan hawakufa 2000 sawa ila walitoka wangapi barabarani? malawi walitoka wangapi? yaani watu wa kuhesabika ambao hata nia wala lengo halieleweki jeshi lije litoe msaada?

weka pembani hisia halafu angalia mambo kwenye uhalisia wake, acha kuishi kwenye kusadikika,, kwamba unataka kukataa taasisi hazipo chini ya muundo fulani.. hata ukiziita "failed methods" ndo hizo zinaongoza nchi.. na kama unachunguza vyema utaona huu ndo mtindo wa uongozi kwenye nchi nyingi duniani kwa sasa, kwahiyo siyo kitu rahisi kushindani nayo,,,
 
29/10 idadi haikuwa kubwa. Tungetoka wengi wa kutosha sasa hivi CCM na Samia ingekuwa historia, Bahati mbaya sana kuna watu wenye mawazo mgando kama wewe ambao walidhani wanajeshi ndiyo watapindua nchi. Nepal walitoka vijana wengi tena haikuwa siku moja! Ukitegeana kutoka hakuna wa kukuletea mabadiliko na wewe umekalisha makebo kama unavyobwabwaja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…