Bapa limepita na mzee wa upako

Mkuu tatizo lako ni kwamba unadhani tupo JF KUJIBISHANA

Ondoa kwanza hiyo mentality kichani mwako ili usiwe unatumia lugha za maudhi as if tuna UGONVI

HOJA ni kwamba Yesu ni Mungu au la
Umetoa mistari ya Bibilia kusapoti madai yako kuwa ni Mungu na ukatoka na nje ya mada ukaanza kuhoji uislam lakini hakuna aliyekuita MPUMBAVU

Mimi nimejenga hoja kwamba Yesu sio Mungu kwasababu kuna mistari mingi zaidi inayosema Mungu hana mshirika na Yesu sio Mungu kuliko mistari ya kuokoteza kusapoti ni Mungu.
Na nikajenga hoja kuhusu ni lini na nani wali develope idea ya Yesu kuwa ni Mungu....... na idea hiyo ni Holy Trinity

Sasa ulitaka nijenge vipi hoja yangu bila kutaja chanzo cha idea ya yesu kubatizwa umungu bila kutaja Holy Trinity?
Mistari yote uliyo quote na utakayo quote ndiyo iliyotumika kutengeneza Trinity.... kuhalalisha Yesu ni Mungu pia...... UPUMBAVU wangu ni nini mkuu?

Kama huwezi kujibu hoja KINZANI au hutaki unaipotezea tu kama hujaiona vile na sio kuanza kuporosha matusi
 
Wewe ndio uliye anza kuninukuu mimi na kunikejeri bila sababu za msingi.
Mi anaye ongea kistaarabu namjibu kistarabu pia.
Sawa tufanye wewe ndio mshindi.
Ila mimi mambo ya holly trinity ndio nayasikia kwako.
Na hayapo kwanye vitabu vya dini nilivyovisoma.
Kama niliongea pumba ungenipotezea tu.
 
Ndio maana nakwambia ondoa mentality ya kubishana au kushindana kutafuta MSHINDI
Mimi sishiriki mjadala KUSHINDA wala sihitaji USHINDI wowote
Na issue hapa sio nani kaanza kum quote nani...... hapa tunajadili kwa hoja kinzania

Nime quote bandiko lako kwasababu sijaliona kama ni PUMBA, na ndio maana nikalisifia lakini nikasema ni la kutungwa tu...... hii sio kejeli Mkuu

Najua unajua dhana ya Mungu katika utatu mtakatifu(Mungu baba, Mwana na Roho Mtakatifu)
Na kama kweli hujui ungeuliza upewe ushahidi....... mjadala ungeendelea kwama amani
 
Unapata wapi ujasiri wa kumuomba msamaha mwanamke?
 
Hivi wewe ukiwa na majina matatu yaani
Joseph Wiliam Kigosi.
Inamaana wewe ni watu watatu ?
Mimi sifahamu mambo ya utatu.
Ninachojua. Huyo Mungu wengine walimwita Baba
Huyo huyo wengine wakamwita wakamwita Roho Mtakatifu
Wengine wakamwita Neno,
Walimwita huyo huyo Mungu mmoja.
Sasa habari za Utatu sijui unazitoa wapi
Kwani ukiwa Baba ya watoto wako
Halafu ukawa Mwalimu shuleni
Pia ukawa Mshauri wa vijana
Hapo utasema wewe ni watu watatu ?
Tatizo tunatofautiana namna ya kuelewa mambo.
Nabii isaya alimwita mtu fulani mmoja majina mengi tu

Soma hapa
Isaya 9:6 Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake,
1.Mshauri wa ajabu,
2.Mungu mwenye nguvu,
3.Baba wa milele,
4.Mfalme wa amani.

Kumbuka Isaya anasema Jina lake na sio Majina yake.
Kwa mtizamo wako huo ni Unne mtakatifu, ni zaidi ya Utatu.

Samahani kwa nilipo kukosea. Ilikuwa mihemko tu.
 
wacha aendelee kupiga hela
 
Hebu tuangalie maandiko yanayo andika habari za majina matatu, kwanza ni pale alipotamka Yesu kukusu kutaja majina matatu wakati wa Ubatizo.

Mathayo 28
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu.

Papili ni waraka wa Yohana.

1 Yohana (1Jo) 5:8
Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja.
.............
Hapa Neno au Mwana inasimama kwenye sifa moja
Kama ilivyo andika Yohana.

Yohana 1:1 Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1:14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu "kama" wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.

Hapa kwa upande wa Baba hakuna shida ni sifa ya uumbaji maana Kibiblia anaye zaa ni Baba na sio mama.
Soma Mathayo 1: 1 na kuendelea.
Mungu sehemu nyingi tu alijiita
Baba.

Roho Mtakatifu.
Maandiko yanasema Mungu ni Roho Takatifu na kwakuwa ndio chanzo cha uhai anaitwa Roho Mtakatifu.
Tuseme Mungu hana mwili wa kibinadamu bali ni Roho.
Hapa hapana shida.
........
Yohana (Joh) 4:24
Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.
..................
Shida inaanzia kwa Mwana au Neno.
Yohana 1:1 hapo juu inasema Neno ni Mungu mwenyewe.

Yohana 1:14
Inasema huyo Neno ambaye ni Mungu
1. Alifanyika mwili (kiasili yeye hana mwili)
2. Alikuja duniani na kuishi na watu (ila kwake ni mbinguni)
2. Alijitambulisha kwa hao watu "kama" Mwana wa Mungu.

Kutokana na Yohana huyo Mwana sio Mwana kweli bali ni Neno ambaye ni Mungu Mwenyewe.

Pia kule Agano la Kale huyo ndio mtoto (mwana)ambaye Nabii Isaya 9:6, alimpa yale majina manne na mojawapo ni jina la
1. Mungu mwenye nguvu
2. Baba wa milele

Hapo ndio dhana ya Yesu ni Mungu au sio Mungu inanza kuchipua.
Maana huyo Mwana alitambulishwa pia na Malaika kuwa Jina lake ni Yesu.

Kwangu mimi neelewa kuwa hayo majina ni sifa au utambulisho tu wa huyo huyo Mungu mmoja.
Mungu sio Binadamu na hana mwili wa kibinadamu.
Kumwita Binadamu kuwa ni Mungu ni kosa.

NB
Hizi habari sio za mimi wala Wakristo.
Hizi habari zimeandikwa na Mitume na Manabii wa kwenye Biblia wa Agano la Kale na Jipya.
Ndio walio andika kuwa Mungu huyo huyo ni
Baba, pia ni
Roho Mtakatifu, na pia ni
Neno au Mwana.
Na kusema hao watatu ni Umoja na sio Utatu, (hapo kwenye waraka wa 1Yohana 5:8)
.......
{Wasomi wa kudadavua mambo ya dini nawaacha hapo muendelee kutafakari}
 
Suala la Yesu alilitolea ufafanuzi, kwa hiyo nawe njoo na fact za kujenga hoja juu ya Uungu wa Yesu tuitathimini.

Kurudia jambo lililokwisha kufafanuliwa bila ya kujenga hoja mbadala ni ukasuku.
 
sema huyu mzee wabongo kuna kipindi wakawa wanasema ameathirika, mara ana kisukari mara pressure ila ukiwa mtu maarufu ni shida sana maneno yote machafu yatakuishia wewe
MIMI namwelewa kinoma huyu Mzee asiemwelewa pigo zake za far right hawezi kumuelewa kamwe kuna topic 1 aliiongelea kuhusu kuneka kwa lugha ndio nilimwelewa zaidi lakini kingine watu wasichomwelewa Mzee huyu ni Chifu Mwantembe Chifu wa Wahehe kwa HIO anaposema Yesu sio Mungu waelewe anaesema hivyo sio Mzee wa Upako bali ni Chifu Mwantembe wajue kutofautisha kati ya Chifu Mwantembe na Mzee wa Upako hao ni watu wawili tofauti ndani ya Mwili wa mtu mmoja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…