Bar zilizofungiwa zatakiwa kulipa Faini Milioni Tano 5M kila moja ili ziruhisiwe kufanya biashara

Waache kupigia kelele waone km hao nemc watawasogelea
 
Mikwara ya nn chief? Si mfuate sheria?
 
Ndio tatizo wa vijijini wakija kuishi mjini, wanaona ni sawa tu makelele ya muziki
Kuna moja olikuwa karibu na nyumbani miaka ile, ikaanza huu upuuzi, tukamwambia tutachoma baa muda si mrefu, siku moja tukaanza kufanya usafi usiku mtaani na kukusanya takataka kibao karibu ya baa yake tukapiga kiberiti, bonge la bonfire, akapewa taarifa kesho yake na muziki ukayayuka mpaka leo
 
Sheria za Tanzania zina tungwa na kina Msukuma .. Ambao hata maana ya sheria hawajui..
 
Acha mikwara boss
 
Kwa hiyo viongozi ndio wana haki ya kuvunja sheria na kufanya usumbufu kwa raia wengine?? Akili za hovyo sana hizi.
 
Sawa ni kweli mkuu hata mi mtaani kwangu ni hivo hivo ila Huwa haidumu dk 20 hizo maneno zote.Sasa mziki Huwa ni kuanzia saa tatu usiku Hadi kunakucha.
 
Kuna viwanda na migodi kibao inachafua mazingira ila wanafungia bar kisa mziki.
Bar zimefungiwa kisa kelele kwa watu wa nje wasiohusika nazo, sio kwa sababu ya muziki.
Viwanda na migodi kufanya uharibifu wa mazingira haihalalishi uchafuzi wa mazingira wa Bar.
 
Hivi utafiti gani huo uliofanyika na kubaini kuwa kupiga mziki kwa sauti kubwa ndio unaovuta wateja? nijuavyo mimi kinyume chake ni sahihi kwa sababu wakati huo muziki unakuwa kama tiba. Unywaji wa pombe na vichangamshi vingine vinapovuka kiwango ndipo watu wanaposhindwa kusikilizana na kudai muziki uongezwe sauti.

Shillingi millioni moja kwa wasumbufu hawa wenye kiburi na dharau kwa wengine wasiopenda makeleie, naona ni ndogo sana. Hiki kinaweza kuwa chanzo kizuri cha mapato ya serikali, Million ishirini ingewafaa sana, waliofungiwa na masharti ya kupata leseni yawe magumu zaidi kwa wote wanaotumia vyombo vya muziki kwenye biashara zao mfano, Makanisa, misikiti, baa, kumbi za harusi, boda boda na magari ya matangazo na promosheni.

1. Ningeshauri NEMC mamlaka yake na utendaji vihamishiwe kwenye ngazi ya Serikali za mitaa, wawe na ofisi zao kwenye halmashauri za miji vijiji na katani.
2. Vibali vitolewe kwa atakayekidhi masharti mapya magumu yanayozuia uzalishaji wa kelele zilizopitiliza hasa kwenye makazi wa watu.
3. Ujenzi wa kumbi za starehe, baa, misikiti makanisa wamiliki wapewe elimu juu ya athali za kelele mtaani, ikibidi walazimishwe kufunga vidhibiti sauti kama hawawezi kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha sauti kinacho kubalika.
4. Kwa kuwa Tatizo la kelele mitaani ni kubwa na wazalishaji wa kelele wanajua hawawezi kuadhibiwa kwa kisingizio cha kulipa kodi au kuajiri wafanyakazi, nashauri vibali vya biashara zote zinazohusiana na uchafuzi wa mazingira, vitolewe kila baada ya miezi sita hadi mwaka na viwango vyake viwe juu zaidi, kitu kama laki tano hadi million moja kwa kila kibali. Anayekiuka masharti alipe millioni 20 au afungiwe kabisa kufanya biashara hiyo.
 
Katika mada kama hizi ndio unapata kipimo sahihi cha unafiki wa waTanzania..... kiukweli ni mtihani mgumu sana kuwasimamia waTanzania.....ndio maana hata viongozi wazalendo walioamua kuthubutu kuhangaika na kero zetu waliamua kuwa wezi.......

Watanzania ni aina ya wananchi wasioeleweka na wasio jielewa.....
 
Tuliwambia wakati wa Jiwe biashara za watu zinakufa mkasea aaah wapi hao ni wapiga deal.😄😄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…