Bar zilizofungiwa zatakiwa kulipa Faini Milioni Tano 5M kila moja ili ziruhisiwe kufanya biashara

Bar zilizofungiwa zatakiwa kulipa Faini Milioni Tano 5M kila moja ili ziruhisiwe kufanya biashara

Yani kisa mtu unamadaraka unanyanyasa watu na biashara yao wakati unamkuta yeye kiosk hajawahi fungua, huu ni uhuni, ndo maana majitu ya namna hii ,Rais aliyaita mastupidi, nami nasema stupid,

Watu wanapambana tengeneza ajira kama sector binfsi alafu mtu mmoja kisa ni mkurugenzi wa NEMC ,analeta ustupidi hapa , ndo maana maajari yanawatafuna
Waache kupigia kelele waone km hao nemc watawasogelea
 
Kwa uzoefu wangu huyo Mkurugenzi au afisa yoyote aliyepo front lazima atapata anachokitafuta. Kufungia Bar 89 kwa mara moja sio jambo dogo. Kagusa pabaya mno. Wasichokijua biashara nyingi kubwa ni za hawa hawa viongozi wetu ila hawatokei front. NEMC wajitafakari.
Mikwara ya nn chief? Si mfuate sheria?
 
Ndio tatizo wa vijijini wakija kuishi mjini, wanaona ni sawa tu makelele ya muziki
Kuna moja olikuwa karibu na nyumbani miaka ile, ikaanza huu upuuzi, tukamwambia tutachoma baa muda si mrefu, siku moja tukaanza kufanya usafi usiku mtaani na kukusanya takataka kibao karibu ya baa yake tukapiga kiberiti, bonge la bonfire, akapewa taarifa kesho yake na muziki ukayayuka mpaka leo
 
Mkuregenzi WA NEMC amezipa siku Kumi na NNE waliofungiwa bar kulipa Faini ya shillingi milioni tano la sivyo watazifutia lesini.

Mtumishi huyo WA umma ameyasema hayo Leo wakati akitoa taarifa Kwa vyombo vya habari. Hali hii inazidi kuonyesha namna ilivyo ngumu kufanya biashara Tanzania na ilivyo ngumu Kwa sekta binafsi kutoboa.

Wakati akitoa kauli hii hakuna sehemu alipoweza kufafanua
1. Waajiriwa katika bar hizi wataishi vipi?

2. Mapato ya bar husika Kwa mwezi ni kiasi gani?

3. Milioni tano akiambiwa yeye alipe anao uwezo wa kulipa?

4. Anapopanga kuzifutia leseni Kodi inayopotea itapatikana Kwa njia gani

5. Waliolipa Kodi ya biashara kwenye hizo bar mfano wenye leseni ya chakula ndani ya bar hizo ambao NI tofauti na mmiliki WA bar anaathirika vipi?

6. Serikali ikigikishwa mahamani na kudaiwa fidia Kwa hasara alizosababisha atalipa yeye?

7. Wakati wa ufungaji WA bar husika watu wa NEMC awakuweza kukusanya ushahidi WA makosa yaliyotendwa, je serikali ikitakiwa kuthibitisha hayo ataweza kulisaidia Taifa?

8. Nani aliyetoa leseni ya hizi biashara? Nini mtizamo WA taasisi nyingine?

Haya na mengine yalipaswa kutangulia faini lakini Kwa kuwa mfumo uliopo unatamani wanaojitegemea wasifanikiwe na wanaoiba kama walivyotajwa kwenye ripoti ya CAG wafanikiwe basi ..........

Matokeo yake Kwa mambo haya hakuna mchina wala muhindi wala hata mbongo serious ataweka pesa zake Tanzania ; wote watazitorosha kwenda kuzihifadhi nje.

Taifa langu Tanzania mnavyowatesa Watanzania sidhani kama mnaweza kuzitesa biashara za mabeberu hivi.......

Ikivuma Sana inakaribia kupasuka
Sheria za Tanzania zina tungwa na kina Msukuma .. Ambao hata maana ya sheria hawajui..
 
Ungejua ulizozitaja nazo zimefungiwa ndo ungejua kuna husda katika hili lililofanywa na NEMC.

Hawa NEMC ni wajinga na wapumbavu, eti watafungia leseni, kwa mamlaka gani waliyo nayo? Kwani wao ndo waliotoa hizo leseni??

Hivi nikiwafikisha mahakamani kwa madai, si naweza shinda fidia ya maana? Wanaweza vipi kuproduce ushahidi usiotia shaka kwamba wakati wanafika walikuta bar yangu inapiga muziki kwa kelele iliyozidi desibeli inayoruhusiwa? Ushahidi wao ni wa namna gani?(mfano traffic wao hukuonesha picha ya gari lako likioverspeed) Je wao NEMC watanipa audio iliyokuwa inakuwa played na kiwango cha desibeli, watathibitisha vp mziki huo ulikuwa kwangu na sio bar nyingine? Wakili mzuri nione PM tuyajenge PM, nina hisa kwenye Bar moja maarufu hapa DSM wameifungia
Acha mikwara boss
 
Kwa uzoefu wangu huyo Mkurugenzi au afisa yoyote aliyepo front lazima atapata anachokitafuta. Kufungia Bar 89 kwa mara moja sio jambo dogo. Kagusa pabaya mno. Wasichokijua biashara nyingi kubwa ni za hawa hawa viongozi wetu ila hawatokei front. NEMC wajitafakari.
Kwa hiyo viongozi ndio wana haki ya kuvunja sheria na kufanya usumbufu kwa raia wengine?? Akili za hovyo sana hizi.
 
Hapa jirani kuna msikiti unaanza adhana saa kumi za usiku na mwingine saa kumi na moja.
Kuna shehe anapiga adhana halafu anaanza mawaidha usiku, mwingine anaaza vitisho kwa watakaokaidi kuamka, mwingine anaweka Kawaida. Hili nalo liangaliwe kuwe na kanuni ya kuanza adhana na nini kisifanyike ili wengine waendelee kuchapa usingizi.
Sawa ni kweli mkuu hata mi mtaani kwangu ni hivo hivo ila Huwa haidumu dk 20 hizo maneno zote.Sasa mziki Huwa ni kuanzia saa tatu usiku Hadi kunakucha.
 
Kuna viwanda na migodi kibao inachafua mazingira ila wanafungia bar kisa mziki.
Bar zimefungiwa kisa kelele kwa watu wa nje wasiohusika nazo, sio kwa sababu ya muziki.
Viwanda na migodi kufanya uharibifu wa mazingira haihalalishi uchafuzi wa mazingira wa Bar.
 
Hivi utafiti gani huo uliofanyika na kubaini kuwa kupiga mziki kwa sauti kubwa ndio unaovuta wateja? nijuavyo mimi kinyume chake ni sahihi kwa sababu wakati huo muziki unakuwa kama tiba. Unywaji wa pombe na vichangamshi vingine vinapovuka kiwango ndipo watu wanaposhindwa kusikilizana na kudai muziki uongezwe sauti.

Shillingi millioni moja kwa wasumbufu hawa wenye kiburi na dharau kwa wengine wasiopenda makeleie, naona ni ndogo sana. Hiki kinaweza kuwa chanzo kizuri cha mapato ya serikali, Million ishirini ingewafaa sana, waliofungiwa na masharti ya kupata leseni yawe magumu zaidi kwa wote wanaotumia vyombo vya muziki kwenye biashara zao mfano, Makanisa, misikiti, baa, kumbi za harusi, boda boda na magari ya matangazo na promosheni.

1. Ningeshauri NEMC mamlaka yake na utendaji vihamishiwe kwenye ngazi ya Serikali za mitaa, wawe na ofisi zao kwenye halmashauri za miji vijiji na katani.
2. Vibali vitolewe kwa atakayekidhi masharti mapya magumu yanayozuia uzalishaji wa kelele zilizopitiliza hasa kwenye makazi wa watu.
3. Ujenzi wa kumbi za starehe, baa, misikiti makanisa wamiliki wapewe elimu juu ya athali za kelele mtaani, ikibidi walazimishwe kufunga vidhibiti sauti kama hawawezi kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha sauti kinacho kubalika.
4. Kwa kuwa Tatizo la kelele mitaani ni kubwa na wazalishaji wa kelele wanajua hawawezi kuadhibiwa kwa kisingizio cha kulipa kodi au kuajiri wafanyakazi, nashauri vibali vya biashara zote zinazohusiana na uchafuzi wa mazingira, vitolewe kila baada ya miezi sita hadi mwaka na viwango vyake viwe juu zaidi, kitu kama laki tano hadi million moja kwa kila kibali. Anayekiuka masharti alipe millioni 20 au afungiwe kabisa kufanya biashara hiyo.
 
Katika mada kama hizi ndio unapata kipimo sahihi cha unafiki wa waTanzania..... kiukweli ni mtihani mgumu sana kuwasimamia waTanzania.....ndio maana hata viongozi wazalendo walioamua kuthubutu kuhangaika na kero zetu waliamua kuwa wezi.......

Watanzania ni aina ya wananchi wasioeleweka na wasio jielewa.....
 
Mkuregenzi WA NEMC amezipa siku Kumi na NNE waliofungiwa bar kulipa Faini ya shillingi milioni tano la sivyo watazifutia lesini.

Mtumishi huyo WA umma ameyasema hayo Leo wakati akitoa taarifa Kwa vyombo vya habari. Hali hii inazidi kuonyesha namna ilivyo ngumu kufanya biashara Tanzania na ilivyo ngumu Kwa sekta binafsi kutoboa.

Wakati akitoa kauli hii hakuna sehemu alipoweza kufafanua
1. Waajiriwa katika bar hizi wataishi vipi?

2. Mapato ya bar husika Kwa mwezi ni kiasi gani?

3. Milioni tano akiambiwa yeye alipe anao uwezo wa kulipa?

4. Anapopanga kuzifutia leseni Kodi inayopotea itapatikana Kwa njia gani

5. Waliolipa Kodi ya biashara kwenye hizo bar mfano wenye leseni ya chakula ndani ya bar hizo ambao NI tofauti na mmiliki WA bar anaathirika vipi?

6. Serikali ikigikishwa mahamani na kudaiwa fidia Kwa hasara alizosababisha atalipa yeye?

7. Wakati wa ufungaji WA bar husika watu wa NEMC awakuweza kukusanya ushahidi WA makosa yaliyotendwa, je serikali ikitakiwa kuthibitisha hayo ataweza kulisaidia Taifa?

8. Nani aliyetoa leseni ya hizi biashara? Nini mtizamo WA taasisi nyingine?

Haya na mengine yalipaswa kutangulia faini lakini Kwa kuwa mfumo uliopo unatamani wanaojitegemea wasifanikiwe na wanaoiba kama walivyotajwa kwenye ripoti ya CAG wafanikiwe basi ..........

Matokeo yake Kwa mambo haya hakuna mchina wala muhindi wala hata mbongo serious ataweka pesa zake Tanzania ; wote watazitorosha kwenda kuzihifadhi nje.

Taifa langu Tanzania mnavyowatesa Watanzania sidhani kama mnaweza kuzitesa biashara za mabeberu hivi.......

Ikivuma Sana inakaribia kupasuka
Tuliwambia wakati wa Jiwe biashara za watu zinakufa mkasea aaah wapi hao ni wapiga deal.😄😄
 
Back
Top Bottom