Hivi utafiti gani huo uliofanyika na kubaini kuwa kupiga mziki kwa sauti kubwa ndio unaovuta wateja? nijuavyo mimi kinyume chake ni sahihi kwa sababu wakati huo muziki unakuwa kama tiba. Unywaji wa pombe na vichangamshi vingine vinapovuka kiwango ndipo watu wanaposhindwa kusikilizana na kudai muziki uongezwe sauti.
Shillingi millioni moja kwa wasumbufu hawa wenye kiburi na dharau kwa wengine wasiopenda makeleie, naona ni ndogo sana. Hiki kinaweza kuwa chanzo kizuri cha mapato ya serikali, Million ishirini ingewafaa sana, waliofungiwa na masharti ya kupata leseni yawe magumu zaidi kwa wote wanaotumia vyombo vya muziki kwenye biashara zao mfano, Makanisa, misikiti, baa, kumbi za harusi, boda boda na magari ya matangazo na promosheni.
1. Ningeshauri NEMC mamlaka yake na utendaji vihamishiwe kwenye ngazi ya Serikali za mitaa, wawe na ofisi zao kwenye halmashauri za miji vijiji na katani.
2. Vibali vitolewe kwa atakayekidhi masharti mapya magumu yanayozuia uzalishaji wa kelele zilizopitiliza hasa kwenye makazi wa watu.
3. Ujenzi wa kumbi za starehe, baa, misikiti makanisa wamiliki wapewe elimu juu ya athali za kelele mtaani, ikibidi walazimishwe kufunga vidhibiti sauti kama hawawezi kuendesha shughuli zao kwa kiwango cha sauti kinacho kubalika.
4. Kwa kuwa Tatizo la kelele mitaani ni kubwa na wazalishaji wa kelele wanajua hawawezi kuadhibiwa kwa kisingizio cha kulipa kodi au kuajiri wafanyakazi, nashauri vibali vya biashara zote zinazohusiana na uchafuzi wa mazingira, vitolewe kila baada ya miezi sita hadi mwaka na viwango vyake viwe juu zaidi, kitu kama laki tano hadi million moja kwa kila kibali. Anayekiuka masharti alipe millioni 20 au afungiwe kabisa kufanya biashara hiyo.