Barabara nne Dar kufungwa kuimarisha Usalama mkutano wa SADC na EAC kujadili mzozo wa DRC na M23

Chanzo cha mgogoro ni Kagame na Mseveni kutafuta Raw materials DRC kwa njia ya hila.
Siyo kweli hata kidogo, inavyoonekana wewe hauna taarifa za kutosha na za uhakika kuhusiana na Mgogoro huo wa huko DRC (Zaire). Fanya utafiti wako wa kina kabisa kuhusu suala hili kabla ya kutoa maoni yako humu mtandaoni
 
Exactly 💯

Ova
 
Siyo kweli hata kidogo, inavyoonekana wewe hauna taarifa za kutosha na za uhakika kuhusiana na Mgogoro huo wa huko DRC (Zaire). Fanya utafiti wako wa kina kabisa kuhusu suala hili kabla ya kutoa maoni yako humu mtandaoni
Maoni ya kisomi na maoni halisi ni vitu viwili tofauti.Maoni ya kisomi yanapenda sana kuamini katika uongo na mifano ambayo haina tija.Lakin maoni halisi yanaenda stright kwenye point.Kwanza sababu kubwa ni UBINAFSI,pia rasilimali zilizoko eneo la Beni ni chanzo cha mgogoro huo,pia Marais hawa wawili Kagame na Mseveni wamekuwa kichocheo kikubwa kwa misingi ya UKABILA.
 
Acha ujinga wako mumzomee kwa sababu gani? Hujui historia ya mgogoro Ndio maana unazungumza ujinga huu!
Leo hii Mkiamua kuwapa kipigo wamasai wa Tanzania unadhani wamasai wa Kenya wataacha kuja kuwasaidia ndugu zao? Ndio Kagame anachofanya DRC.
Kuvuka mpaka ni kosa. Ukielewa hilo umeelewa pakubwa sana
 
Narudia tena kusema kwamba 'Root Causes' za huo Mgogoro wa huko DRC (Zaire) siyo Rais Paul Kagame wa Rwanda wala siyo Rais Yoweri Museven wa Uganda. Kamwe Watu hao siyo sababu wala siyo kiini na chanzo cha kuibuka kwa Mgogoro huo.

Je, wakati wa mauaji ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Bw. Patrice Lumumba miaka ya 1960 huyo Kagame na Museven walikuwa maRais kwenye hizo nchi zao wanazotawala hivi Sasa?

Rudi ukafanye tena utafiti wako upya kabla ya kujadili suala hili. "No research no right to speak:" (By Mao Zedong).

Mgogoro huo una historia ndefu.
 
Umzomee,amefanya nini?
Kwa sababu anawasapoti M23?
Wa Emirati wanaiunga mkono RSF wanaleta unnecessary complication katika kuimaliza vita ya Sudan,mbona hatujasikia mtu yoyote anawazomea?
Ya kwenu yameisha hadi unahangaika na jirani?
 
Kuvuka mpaka ni kosa. Ukielewa hilo umeelewa pakubwa sana

"Injustice somewhere is the threat to Justice everywhere."
Martin Luther King Jr.

Usifikiri kwamba Watu wataogopa kuvuka mipaka ya nchi yoyote ile ili kwenda kutoa msaada kwa Watu wengine ambao wanaamini wazi kabisa kwamba hawatendewi HAKI.
Utawala wa nchi au Serikali ya Nchi yoyote ile hapa duniani inapofanya DHULUMA dhidi ya Watu fulani fulani katika nchi husika basi Utawala huo unapaswa utambue ya kwamba kwa kufanya hivyo itakuwa inawaalika kwa LAZIMA Watu Wapenda HAKI kuweza kuingia kwa nguvu kwenye hiyo nchi ili kuwasaidia wale Watu wanaodhulumiwa Haki zao.

DHULUMA huwa Ina kawaida ya kuwakusanya na kuwaunganisha pamoja wale Watu ambao wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya DHULUMA.
 
Umzomee,amefanya nini?
Kwa sababu anawasapoti M23?
Wa Emirati wanaiunga mkono RSF wanaleta unnecessary complication katika kuimaliza vita ya Sudan,mbona hatujasikia mtu yoyote anawazomea?
Kuna tafauti kubwa kati ya athari za matatizo ya Sudani na matatizo DRC!.
Rwanda na DRC ni majirani zetu! Na matatizo ya majirani zetu ni matatizo yetu! Nchi jirani zinapokuwa vitani husababisha uwepo wa wakimbizi wanaokimbilia kwenye nchi yetu!
Na ushahidi unaonyesha kuwa Paul Kagame ndio mzizi wa vita vinavyoendelea mashariki mwa DRC.
Kwahiyo Kagame sio kuzomewa tu bali yatakiwa pawepo mipango thabiti ya kumng'oa madarakani ili kurudisha amani ya kudumu katika nchi za maziwa makuu.
 
Chuma nakielewa sana iki mwili mdogo vitu vikubwa
 

Attachments

  • FB_IMG_1737997769908.jpg
    50.6 KB · Views: 1
Wewe na nani?
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Unajidanganya Sana.

Amani ya Kudumu kamwe haiwezi kuwepo endapo kama HAKI haipo.

Guarantee ya uhakika ya kuwepo kwa Amani hutokana na kuwepo kwa HAKI.

Amani ni tunda la HAKI.

If there is no Justice then there will be no Peace!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…