Barabara ya Mwendokasi kutoka Maktaba hadi Tegeta kuanza kujengwa, Ubungo Kimara kufumuliwa

Kabla ya nyingine ubungo Hadi kimara ,si wange endelea kibaha mpaka mlandizi ,mdogo mdogo mpaka chalinze,kunatisha ajali kila siku,Barabara mbovu magari mengi
Halafu matochi kibao ni kama hawapendi mpite hizo 6 line.
Nauliza tu kauli ya mkandarasi anakuja kipande cha moro chalinze njia mpya ataanza lini.
 
Hiyo ya Ubungo-Kimara njia 8 imekaa vizuri sana

Ina maana hapo itakuwa njia 8 Ubungo mpaka Kibaha

Nashauri serikali wasiishie tu Ubungo wajenge tena njia 8 kutoka Ubungo hadi Kivukoni (Hapo itakuwa ni njia 8 kutoka Kivukoni hadi Kibaha)

Nimeona manufaa ya njia 8 ukipita barabara ya Kimara hadi Kibaha hakuna foreni kabisa siku hizi
 
Bomoa bomoa itakuwa sio ya kitoto

Sent from my itel L5007 using JamiiForums mobile app
 
Barabara za mabasi ya mwendo kasi haziwezi kuwa suluhisho la foleni ya magari dar , ni very short term project na baada ya miaka kadhaa mbele tutakuja kuvunja tena hizi barabara na kujenga kile ambacho first world wanafanya .
Public roads zinatakiwa ziboreshwe na sio ku priotize category fulani ya usafiri kama tunavozipa kipaumbele mwendokasi.
Wenzetu Kenya hili wameliweza .
 
Tuna shindwa nn kutrain watu wetu rather kutegemea nje
 
Kabla ya nyingine ubungo Hadi kimara ,si wange endelea kibaha mpaka mlandizi ,mdogo mdogo mpaka chalinze,kunatisha ajali kila siku,Barabara mbovu magari mengi
kweli kabisa. Kibaha-chalinze ni eneo hatarishi sana.

Pia, kwa mwenendo wa BRT ya sasa, ni bora serikali itafute mwendeshaji binafsi wa BRT, mwekezaji wa ndani kama mwanzoni ilivyokuwa maxcom walipoinstall hata ile mitambo na wakaanzisha malipo ya kadi. Waliopo sasa wamefeli sana, kazi imewashinda. Ikiwa kimara -kivukoni-moroko-gerezani imewashinda hivi. Njia zingine za tegeta, mbagala, gongo la mboto zikianza wataweza?
 
Mama hii miradi yako ni heavy, tuliona hapa bwana yule akitujengea kibarabra cha cha pale Mwenge kwa kuwakamua pesa zao wabunge.

Leo umeamuwa mama. Jioneeni"



Jamani hii ni mi Dirham ya Dubai nini?
Yes ni mambo ya DP, Baada ya kununua bandari wamesema hawataki foleni kabisa kontenna zao zinatakiwa zipite kwa kasi ambayo hata TRA hawataona zimepitia wapi.
 
Hiyo sahau haitakaa iwezekane, hv huoni tuu Barabara ya mwendokasi ilivyopita pale kisutu mpaka kuja kutokea huku Posta ya zamani kwa kuforce, Sasa hizo njia SITA zitapita wap mpaka kivukoni
 
Hakuna mji wenye foleni mbaya kama Nairobi hapa east Africa...wenyew wanatamani hata wawe na mwendokasi....
Kuna muda ukifika pamoja na barabara zao pana cbd ya Nairobi haifikiki kabisa...

BRT ni solution nzr tu....na baadae wanawwza fikiria kuweka trams kwenye hizo njia za mwendokasi....

Nairobi wanaifata marekani ambako miji yake ina foleni hatari...Dar inaifata Europe ambao miji yao ina brt, trams na subways na siku hiz hadi baiskeli kabisa...na actually Europe iko vzr kimaendeleo kuliko us

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Hoja yangu sio kupinga barabara za brt , bali namaanisha barabara hizo sio suluhisho la foleni mjini hapa , Nairobi ina foleni kwa sababu mji wa wenyewe ni mdogo ililinganisha na dar na huwezi kulinganisha infrastructures za Kenha na Tanroad .
Hizi barabara baada ya miaka 10 tutakuja kuvunja tena! amini nakwambia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…