Ahahahahah shaba moja kwa mojaYani nikipewa madaraka nitakuwa Magufuli x 10 yake sicheki na boya. Kazi tu!
Maadui zangu ni wajinga wajinga wezi na mafisadi ndio ntawanyoosha. Hukumu ni shaba tu hamna kingine. Ukikutwa umedokoa hela na ushahidi ukapatikana jua ni shaba moja kwa moja.
Extrovert,Yani kulikoni huyo mzabuni bora serikali ichukue tozo yenyewe. Sababu gharama ya kusafiria barabara kwa hizo kilometre inaweza kuwa ndefu kichizi. Ila bora ilimradi isiwe na matrafiki tu ambao ni kero namba 1
Kwa tabia zetu watanzania na wapinzani,hizo barabara zitajengwa, na itakapofikia kipindi Sasa serikali inaanza kuchukua Tozo kwenye hizo barabara hili kurudisha ghalama alizotumia mkandarasi,utasikia wananchi watakuja kuanza kulalama mitandaoni kuwa tozo ziondolewe na blablaa kibao,na wapinzani nao watavalia njuga, na anaweza tokea miaka hiyo Rais mpenda Sifa za kisiasa akaondoa hizo tozo na mkandarasi akapata hasara au serikali,Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance
Kazikwe pembeni yake,kwani alijenga kwa fedha zake huyo mungu wenuAliyejenga njia 8 Ubungo - Kibaha yeye hakuona umuhimu wa tozo au nyie ndio mnaijua sana hela?
kazikwe pembeni yakeNdiyo yatakuwa yaleyale ya DART...
Yani hiyo barabara mpaka waje wairudishe ni mpaka pale hiyo barabara ichakae kwanza.
Hawataikabidhi kwa muda kwa visingizio vya hapa na pale hasa "Bado Hatujarudisha Chetu"..
Na hapo tenda ndiyo utakuta kuna mkono wa mkubwa mmoja.
Yani inshort ni kwamba hapa tayari kuna mkubwa kashaichukua hii tenda.
RIP JPM, ULISEMA TUTAKUKUMBUKA KWA MAZURI NA KWELI YANATIMIA.
Kazikwe pembeni yake nawewe huende peponi mkuu, yaani serikali isifanye Jambo kisa huyo mungu wenu,,kubarini serikali inaongozwa na walio hai sio waliokufaSi mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Kwenye miradi yoyote mikubwa ya umma, ni lazima public iwe engaged properly lasivyo hakutakuwa na sustainability.Kwa tabia zetu watanzania na wapinzani,hizo barabara zitajengwa, na itakapofikia kipindi Sasa serikali inaanza kuchukua Tozo kwenye hizo barabara hili kurudisha ghalama alizotumia mkandarasi,utasikia wananchi watakuja kuanza kulalama mitandaoni kuwa tozo ziondolewe na blablaa kibao,na wapinzani nao watavalia njuga, na anaweza tokea miaka hiyo Rais mpenda Sifa za kisiasa akaondoa hizo tozo na mkandarasi akapata hasara au serikali,
Japo lengo Ni zuri Sana, kwamba tujenge kwa fedha zetu,japo tujaribu
Mhe. Silvester Koka, mmoja wa wabunge makini kabisa. Hii ni product ya Tambaza alikuwa mbele yangu akiwa na Dr. Mwinyi, Dr. Seche, na wengine wengi.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).
Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).
Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.
=====================
SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).
Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.
“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.
Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).
Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.
Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.
Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”
Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.
Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.
Chanzo: HABARI LEO
Vp mkuu unaona hii project itawezekana kweli au Siasa tuuMhe. Silvester Koka, mmoja wa wabunge makini kabisa. Hii ni product ya Tambaza alikuwa mbele yangu akiwa na Dr. Mwinyi, Dr. Seche, na wengine wengi.
P
Njoo na hoja yakoUzi umejaa watu wajinga hata wanachojadili hawakijui
Wewe unaona Kati ya wote waliojadili hapo kuna mwenye akili?
Maandalizi gani hayo wakati ndio kwanza tender inatangazwa?Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May
Watajenga mpya ndio watatoza hela, ya zamani inabaki vile vile ya bure.Barabara yetu, iliyojengwa kwa kodi zetu, anapewa Mwekezaji aipanue halafu atulipishe tozo? Hao wawekezaji kwanini wasijenge mahighway yao wakaweka hizo tozo? Hizi zilizopo ni Interstate roads zetu, haiingii akilini kuwagawia wawekezaji
JW, TISS, PCCB, POLICE, PRISON, NEC, MSAJIRI Wa VyamaCCM haitegemei kura kubaki madarakani
Watakapojenga pia wataboresha ya zamaniWatajenga mpya ndio watatoza hela, ya zamani inabaki vile vile ya bure.
Hii inatofauti gani na Ule ujenzi wa bandari Bagamoyo? Kweli viongozi wetu mnavhemka na badala ya kuwasaidia wananchi mnawakatisha Tamaa.Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).
Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).
Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.
=====================
SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).
Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.
“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.
Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).
Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.
Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.
Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”
Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.
Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.
Chanzo: HABARI LEO
Hadithi za alinachaMambo ya kufikirika