Barabara ya Njia 4 Kibaha - Morogoro itakuwa na Tozo

Dah!

Inabidi nikienda morogoro napitia bagamoyo Road...
 
Ningekuwa Samia ningefuta kibarua cha huyu Naibu Waziri. Kulikuwa na ulazima wowote kusema hilo jambo kwa sasa???? Zaidi ya kuhamakisha hasira za wananchi kuhusu tozo?
 

Hapo mwishoni hapo ndio kwenye uchawi wenyewe sasa. Hata Sasa ingekua tozo zinaelekezwa kuboreshwa huduma za kijamii, hakuna mtu angepiga kelele. Unatoa tozo lakini madawa yapo hispitali, huduma za maji, elimu, usalama, maofisini zinaridhisha unafikiri Kuna mtu atalalamika?

Jamaa hua wanakuja na mawazo mazuuuri, kwenye utekelezaji Sasa.

Walitaka wafanikiwe kwenye Hili la hii barabara, serikali isitie Mkono wake, iiachie kampuni binafsi kuanzia mchakato wa ujenzi Hadi kukusanya mapato, serikali wasubirie ushuru/ Kodi Yao tu wakiwa wamekunja mikono kama wanavyolamba tozo za miamala.

Hapo barabara itajengwa Kwa kiwango Bora, muda mchache na hakutakua na longolongo.
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Ni kweli dictator, mshamba, ni wawili tu nitawakumbuka katika maisha yangu Nyerere kwa high IQ, na mwendazake kuwa wa ajabu kata lugha, maamuzi, uonevu,ubinafsi, matatizo mengi amesababisha kwa muda mfupi!
 
Ni kweli dictator, mshamba, ni wawili tu nitawakumbuka katika maisha yangu Nyerere kwa high IQ, na mwendazake kuwa wa ajabu kata lugha, maamuzi, uonevu,ubinafsi, matatizo mengi amesababisha kwa muda mfupi!
Nyerere alikuwa very very evil tu kama meko.

Nyerere kilichomsaidia ni kwamba mitandao ya kijamii kama ya sasa haikuwepo, lakini nyakati zake watu wengi tu walipotezwa na wengine wengi kukimbia nchi.

Nyerere ndo kachangia sehemu kubwa sana ya matatizo ya Tanzania, hasa hii katiba ya sasa ya kidhalimu.

Nyerere alikuwa mwongeaji mzuri, ila matendo yake yalikuwa opposite na alichokihubiri.
 
Road Tall tax hazina shida, tena itakuwa nzuri sana, duniani barabara nyingi ziko za kulipia tozo ndogo na za free, kikubwa barabara iwe nzuri, kubwa na no traffic jam, yaani ukilipia hapa Dar ni moja kwa moja hadi Morogoro, ila sio uanze uhuni ulipie Dar, ulipie Kibaha, ulipie Mlandizi, ulipie Chalinze, ilipie Mikese, ulipie Moro, huo utakuwa ni uwizi wazi duniani kutokea Tanzania

Na tozo za Road Tall tax huwa sio kubwa kabisa, ni ndogo sana, nchi zote zenye barabara za kulipia ni cheap, natoa angalizo isije hapa kwetu ikawa ni ghali kupita hata nauli ya mabasi, huo utakuwa wizi wa wazi.
 
Nchi yenye madini yenye thamani kubwa kubwa inataka kujenga barabara za kutoza watu...
 
Aliyejenga njia 8 Ubungo - Kibaha yeye hakuona umuhimu wa tozo au nyie ndio mnaijua sana hela?
Fanya reference, Jiwe alikuwa mtu wa kwanza kuwaza kujenga mwendo kasi wa kulipia mpaka chalinze kwa PPP, na alikuwa analihubiri daily. Daraja la kigamboni je? Umesahau mambo ya kupiga mbizi?
Ni mtu mpumbavu tu anayeweza kupinga PPP kwenye miradi ambayo kimsingi serikali haiwezi kuimudu yote.

Kupanga ni kuchagua,utaamua upite kwa speed 2hrs kwenda moro ulipe 10000 au upite kwenye foleni na mashimo masaa 5 kwenda Moro
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Hukupata bahati ya kubondwa risasi ndo maana unasema alikuwa na mapungufu ya kibinadamu
 
Hivi Tz KWa Sasa ina watu wa ina GANI ndani ya serikali, ? au hata serikali haipo ila tuonacho ni kivulu tu, Yani mpaka tozo kwenye barabara, kwani ni lazima kujenga Iyo barabara ,lengo nini KWa Sasa au nikuuza nchi twambizane tujue, maana Sasa yanafanyika Mambo ambayo hata mkoloni hakutufanyia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…