Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona


kuna watu mna moyo sana wa kutetea kila kitu
 

Hati ya majukumu ya Baraza la Mawaziri haitaji inclusiness, demography, social forces kama vigezo vya kuteuliwa....



 
Hoja yako hii ya kutaka kuzingatia elimu, weledi, uzoefu na utayari peke yake kama vigezo vya kuendesha nchi ina imply kuwa kwako wewe binafsi huoni tatizo kuwa na baraza la mawaziri ambalo let say asilimia 50 ni watu wa familia moja, maana kwetu sisi hapa Tanzania rais ana mamlaka ya kuteua ndugu zake 10 na kuwapa ubunge na kisha kuwateua kuwa mawaziri!, Raisi anazopower kabisa za kufanya hivyo na akajustify kuwa anafanya kwa best interest ya nchi!

Sasa basi, kwa muktadha wa hoja yako ambayo umeeleza kuwa vigezo pekee vya kuzingatiwa ni weledi, elimu, uzoefu na utayari wa kufanya kazi, basi hii unaimply kuwa kwako siyo tatizo kabisa iwapo rais akateua mke wake, watoto wake watano, kaka yake na dada yake kuwa mawaziri maadam wana elimu nzuri, ni weledi sana, wako wana uzoefu na wana utayari.

Kiufupi ni kuwa hauna Tatizo hata na serikali ya kifamilia as long as inadeliver na kwa muktadha huo hauna tatizo na serikali ya kifalme Tsnzania.

Uongozi wa kitaifa una vigezo vingi na kama ni kiongozi mwenye hekima basi mizania yako inakuwa na vigezo vingi vya kuzingatia unapounda serikali. Nimekupa mfano mmoja wa namba hoja yako inavyoweza kutofaa kwenye uongozi, kuwa hata kama ndugu zako wa karibu wana vigezo kama ulivyovitaja kwa kiasi gani, kuwateua na kuwafanya wawe asilimia 50 ya baraza ka mawaziri.

Hoja ya pili katika hili suala ni je ina maana hivyo vigezo ulivyovitaja vya elimu, weledi, uzoefu utayari wa kufanya kazi vinapatikana kwenye kundi moja tu la demografia?, Watu 23 siyo wengi, na ni dhahiri watu wa vigezo unavyovitaka wamo wa kutosha tu katika society(nafasi zile 10 za rais), na wengine wa kutosha wamo ndani ya bunge (Wazanzibar kwa wabara) . Kwa nini watu wa imani moja wawe ni wengi katika hiyo selection wakati vigezo havuchagui imani ya mtu, jama unavyo unavyo tu

Kwa hiyo kwa muktadha huu, naona uteuzi uliofanyika kuwa sampling iliyofanywa kimakusudi(na imekuwa based kwenye dini ukuachilia mbali vigezo vingine(purposeful sampling blocked on religion as a selection criteria), ndiyo maana laiti wangewekwa mawaziri wazanzibar kuna high chance wangekuwa waislamu na hivyo kuraise number ya waislamu kwenye cabinet. Sasa kwa kuwa blocking inafanyika kwa mrengo wa kidini, basi wateuaji wakaona hata Wazanzibar wasiwemo kwenye hilo baraza potelea mbali maana uwemo wao utaharibu mahesabu yao ambayo katika sampuli yao, blocking imebase kwenye dini (Si unajua wazanzibar more than 99% waliomo bungeni ni waislamu) .

Huhitaji kuwa ni Genius kuliona hilo kuwa kuna udini wa aibu katika teuzi hii
 
Kwa hiyo kwa muktadha huu naiona sampling iliyofanywa kimakusudi(na imekuwa based kwenye dini ukuachilia mbali vigezo vingine(purposeful sampling blocked on religion as a selection criteria) !

Mawili,

  1. Kadiri hoja yangu inayoanzia kwenye meritocracy, inavyohusika, ndugu wa familia moja wanaweza kuingizwa katika Baraza la Mawaziri na likatekeleza majukumu yake, isipokuwa pale kwenye mgongano wa kimaslahi unaokwamisha ufanisi.
  2. Kwenye utafiti, focused sampling, as opposed to randome sampling, inaruhusiwa pia, ilimradi kuwepo na justification.

Mengine yanajadilika.
 
Waislamu bwana shida tupu.Ungejua hata kwamba Rais hakuwa na mawazo ya udini wala unzanzibari alipokuwa ana-zoom kutafuta mawaziri! I believe he was more interested in professionalism.Be positive,mawazo hasi hayatawafikisha popote,mtajiletea visukari na pressure bure wakati mwenzenu hata hayuko huko.
 
Huku kwetu wanasema, mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama... Ukiona wa kuja kapata nyama na wewe uliyemswaga ng'ombe toka maporini umekosa, basi ujue mwenzio ana kisu kikali kukuzidi.. Usinune.. Ndio kanuni ya mchezo.. Kanuni ya mchezo ni mwenye kisu kilali, ale...
Badala ya kununa, badili mahesabu... Ukiwa na kisu butu, usimswage ng'ombe na rungu, mpige bapa moja uambulie hata nundu.. By the time ng'ombe anafika machinjioni, tayari we ushabeba shea yako.
Mahesabu yakigoma kabisa, tumia kanuni ya pili ya mchezo: Hii inaitwa, tukose wote.. Ukiona kisu chako butu na uhakika wa kula nyama ni mdogo, usimswage ng'ombe kwenda machinjioni.. Mswage atumbukie kwenye kisima, MKOSE WOTE!
 
Kwani ni lazima kuteua waziri toka huko wapi katiba imesema hivyo mbona wao hawateui toka bara!
Muungano ufe tu kila mmoja akae kwake maana hata Zanzibar sasa wameanza kuzinduka hawataki mambo mabaya ya BOT kuwapora watu pesa zao pindi zikitumwa tokea nje, sasa kwa Zanzibar wao ni ruksa pesa zozote kutumwa Zanzibar hawataki usumbufu kwa pesa inayoingia huko wanataka pesa ziingie zilete maendeleo
 
Bakwata ni Tawi la CCM wataendelea kupata ruzuku tokea CCM hawaoni tabu waislam kupungua kwenye baraza la mawaziri ambalo 11 wanatoka kanda ya ziwa
 
Sasa ile si serikali ya Zanzibar hii ya magufuli ni serikali ya muungani kati ya Zanzibar na Tanganyika
Zanzibar huwa na Serikali yake baraza la wakilishi hata bunge lao hakuna mbunge tokea Tanganyika, bora kila upande uende kivyake ili Zanzibar ianze kufanya maendeleo yake bila kubugudhiwa na Tanganyika
 
Bila checks and balances kwa mteuaji na kwa aina ya katiba tuliyonayo hiyo unayosema "bila ya mgongano wa kimaslahi" haiexist, maana hata mgongano wa kimaslahi ukiwepo atakwambia haupo na hata ukiwa na proof kuwa upo bado ana loophole nyingi tu za kuendelea na akitakacho yeye!

By the way Nepotism haijawahi kukubalika kama positive action ya namna ya kuongoza au kutawala!
 
Mtajua wenyewe na muungano wenu!
 
% ya Wakristo Zanzibar ni ndogo kuliko ya Baniani huku bara, ushawahi kusikia mtu anajadili kwanini Baniani hawapati fursa za kiutumishi serikalini bara?
Zanzibar hawatambui ukiristo wao ni waislam 100/%
 
Waislam wapewe wizara ya Ulinzi na wizara ya fedha ili waone kama wanathaminiwa washike pesa na pia washike mabunduki yote
 
Kama tumefika hatua ya kuanza kuuliza waislamu, wakristo na wapagani ni wangapi kwenye taasisi basi tumefirisika sana kimtizamo.
Bakwata ni Tawi la CCM ndiyo maana wapo busy kuulizia waislam wenzao
 
Mawili tena,
  1. Ukaguzi wa kuangalia uzingatiwaji wa taratibu (compliance audit) unaanzia kwenye kigezo kilichotamkwa kama mwongozo wa tabia kabla ya zoezi la kufanya ukaguzi. Kwa hiyo, naona tunachanganya mtiririko wa kimantiki. Tuweke vigezo vya uteuzi kwanza, halafu tupime uzingatiwaje wake, na sio kinyume chake.
  2. Kuhusu nepotism: kila kiongozi analo kabila, dini, mbari, etc, lakini hilo halimaanishi kwamba ni mkabila, mdini, mbaguzi wa rangi, n.k. Lakini, hilo halituzuii kuweka vigingi vya kuzuia ukabila, undugunaizesheni, udini, urangi, nk. Wanadamu sio wakamilifu.

Mengine yanajadilika.
 
Rais Mkristo
Makamu wa Rais Muislam
Waziri mkuu Muislam
Jaji Mkuu anaemuapisha Rais Muislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…