Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Baraza Jipya la Mawaziri 2020: Hizi ndizo kasoro kuu 3 ninazoziona

Wewe una chuki ya muda mrefu dhidi ya Rais Magufuli, suala la baraza la mawaziri umelitumia kama nyenzo ya kumshambulia.
Mbona unazungumzia mawaziri tu lakini manaibu mawaziri huzungumzii? Au hivyo sio vyeo? Mbona huhoji kuhusu dini zingine kama budha, hindu, sikh na wapagani? Kwani nchi hii ina dini mbili tu? Baraza la mawaziri Zanzibar lina mkristo hata mmoja? Mbona huko huchambui?

Unadai wanawake ni wachache umeangalia na manaibu mawaziri? Baraza la mawaziri sio chombo cha uwakilishi bali ni chombo cha utendaji hivyo kinachoangaliwa ni ufanisi katika kutekeleza ilani na utendaji.

Hata kama wangeteuliwa watu wa hiyo dini na jinsia unayotaka bado mwingine angelalamika kuwa nchi ina makabila 120 hivyo theluthi mbili za makabila hawamo hivyo haiakisi demography ya nchi. Haya mambo yakiendekezwa ndiyo yanasababisha mlipa kodi kutwishwa mzigo mkubwa wa kodi ili kugharimia baraza kubwa la mawaziri ambalo limesheheni makabila yote. Rejea baraza la Sudani kusini kwa mfano, nchi ndogo masikini inakuwa na baraza kubwa sababu ya kuendekeza upuuzi wa ukabila, dini au jinsia.

Badala ya kukosoa tu hebu eleza mazuri ya JPM au kwa uelewa wako hajawahi kufanya zuri hata moja?

kuna watu mna moyo sana wa kutetea kila kitu
 
Umewahi kusomea kozi yoyte ya uongozi au utawala?
Kuna kitu kinaitwa
1.Inclusiveness
2.Demography
3. Social forces

Hivyo vitu lazima uvizingatie kwenye kuunda timu za kiutawala, las sivyo unaweza kuishia kuunda serikali iliyojaa watu wa kijiji chako peke yake kisha ukajitetea kuwa "lakini ni watendaji wazuri"-Je hakuna watendaji wazuri kutoka sehemu nyingine za nchi?

Hati ya majukumu ya Baraza la Mawaziri haitaji inclusiness, demography, social forces kama vigezo vya kuteuliwa....

1607194631801.png


1607194724711.png
 
Nimesoma bandika la "Misile of the Nation", aka Kombora la Taifa, na kuelewa hoja yake. Lakini sikubaliani na hoja hiyo. Nitaifupisha na kuihakiki hapa chini, tena kwa ufupi kabisa. Mleta bandika amejenga hoja ifuatayo:

  1. Kwa ajili ya kuimarisha umoja wa kitaifa, Baraza la Mawaziri linapaswa kubalansi nguvu za kijamii katika Taifa kwa kutengeneza uwiano mwafaka wa kidemografia katika Taifa;
  2. Baraza la Mawazi lililotangazwa na Rais Magufuli jana halina uwiano mwafaka wa kidemografia katika Taifa kwa sababu uwiano wa Wakristo kwa Waislamu ni 87:13; uwiano wa Wabara na Wazanzibari ni 1:0; na uwiano wa wanawake kwa wanaume sio 50:50.
  3. Kwa hiyo, Baraza la Mawazi lililotangazwa na Rais Magufuli jana haliwezi kuimarisha umoja wa kitaifa.
Hoja hii inabutulika kwa sababu madokezo mawili ya kwanga ni porojo zisizo na ukweli wowote. Hebu tuone porojo hizo.

Uwongo katika dokezo la kwanza: Majukumu ya Baraza la Mawaziri yaliyotajwa kwenye Katiba hayasemi kuwa jukumu mojawapo la Baraza la hilo ni kubalansi nguvu za kijamii katika Taifa, kama anavyosema mleta hoja. Hilo ni wazo lake na anapaswa kulijengea hoja kabla ya kulihitimisha.

Kuna njia 101 za kujenga umoja wa kitaifa. Mfano, kuna JKT, shule za mabweni na vyuo vinazounganisha makabila tofauti, kufundisha lugha ya taifa, kuwa na mtaala mmoja wa elimu katika Taifa, kuwa na mitaala ya uraia inayofundisha utaifa, michezo, sanaa, vyombo vya habari, masomo ya falsafa juu ya ubinadamu, kutandawazisha maisha ya jamii za jirani, n.k

Hivyo, yafaa atwambie kwa nini anafikiri kutengeneza mseto wa kidemografia kwenye Baraza la Mawaziri ni jambo muhimu na lazima kufanyika kama likilinganishwa na njia bali. Kwa hiyo, dokezo la kwanza limeokotwa barabarani na kuletwa hapa kabla ya juhudu za utafiti kufanyika.

Uwongo katika dokezo la pili: Dhana ya uwiano wa kidemografia katika nchi inamaanisha kwamba, Baraza ligawanywe katika sekta kadhaa kwa kutumia vigezo tofauti vya kidemografia. Vigezo hivyo vya kidemografia ni pamoja na jinsia, dini, umri, jiografia, kabila, mbari, nk. Kuna matatizo mawili hapa.

Mosi, vibadilka (variables) vingi kati ya hivi vilivyotajwa vinabeba thamani zaidi ya mbili. Mfano, kibadilika cha jinsi kinaweza kuwa ME au KE, na hapo hakuna shida, kwani, inangia akilini kuongelea uwiano wa nusu kwa nusu. Lakini, vibadilika baki vinabeba thamani zaidi ya mbili, kama ifuatavyo: dini (ukatoliki, ulutheri, usabato, uislamu, uhindu, ubuda, n.k); umri (watoto, vijana, wazee, n.k.); jiografia (mikoa 25, kanda 10, wilaya 200, n.k); kabila (yapo 122); mbari (wabantu, waarabu, wahindi, wanilo, n.k); n.k.

Tatizo la pili ni kwamba, uwaziri ni ofisi yenye majukumu maalum yaliyotajwa kwenye hati ya majukumu. Hakuna hati ya majukumu ya Waziri inayotaka sifa za kidemografia kama kigezo ya uteuzi.

Kwa hiyo, dokezo la pili ni longo longo za vijiweni tu. Halina umakini wowote.

Kwa sababu madokezo mawili ya kwanza yamebutuliwa, basi inafuata kimantiki kwamba hitimisho pia halikubaliki.

Kwa maoni yangu vigezo muhimu katika uteuzi wa Mawaziri sio sifa za kidegorafia, bali weledi, elimu, uzoefu na utayari wa kufanya kazi. Mengine yote ni ziada tu!

Kwa hiyo, inawezekana kabisa tukawa na Mawaziri 23 wanatoka mkoa mmoja, dini moja, kabila moja, mbari moja, jinsi moja, na bado Baraza la Mawaziri likatekeleza majukumu yake kwa kasi na ufanisi.

Nashauri tuelekeze nguvu zetu katika haya:


  1. Jinsi Ilani itakavyotafsiriwa katika mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25
  2. JInsi mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25, utakavyotafsiriwa kwenye mipango mikakati ya kisekta (wizara),
  3. Jinsi, mpango mkakati wa Taifa wawa miaka mitano, 2020/25, utakavyounganishwa na mipango mikakati ya LGAs.
  4. Vigezo vya kuwapata watekelezaji wa mpango mkakati wa Taifa wa miaka mitano, 2020/25, pamoja na mipango mikakati ya LGAs.
  5. Ukusanyaji wa rasilimali kwa ajili ya kutekeleza mipango hii.

Karibu Sumbawanga!
Hoja yako hii ya kutaka kuzingatia elimu, weledi, uzoefu na utayari peke yake kama vigezo vya kuendesha nchi ina imply kuwa kwako wewe binafsi huoni tatizo kuwa na baraza la mawaziri ambalo let say asilimia 50 ni watu wa familia moja, maana kwetu sisi hapa Tanzania rais ana mamlaka ya kuteua ndugu zake 10 na kuwapa ubunge na kisha kuwateua kuwa mawaziri!, Raisi anazopower kabisa za kufanya hivyo na akajustify kuwa anafanya kwa best interest ya nchi!

Sasa basi, kwa muktadha wa hoja yako ambayo umeeleza kuwa vigezo pekee vya kuzingatiwa ni weledi, elimu, uzoefu na utayari wa kufanya kazi, basi hii unaimply kuwa kwako siyo tatizo kabisa iwapo rais akateua mke wake, watoto wake watano, kaka yake na dada yake kuwa mawaziri maadam wana elimu nzuri, ni weledi sana, wako wana uzoefu na wana utayari.

Kiufupi ni kuwa hauna Tatizo hata na serikali ya kifamilia as long as inadeliver na kwa muktadha huo hauna tatizo na serikali ya kifalme Tsnzania.

Uongozi wa kitaifa una vigezo vingi na kama ni kiongozi mwenye hekima basi mizania yako inakuwa na vigezo vingi vya kuzingatia unapounda serikali. Nimekupa mfano mmoja wa namba hoja yako inavyoweza kutofaa kwenye uongozi, kuwa hata kama ndugu zako wa karibu wana vigezo kama ulivyovitaja kwa kiasi gani, kuwateua na kuwafanya wawe asilimia 50 ya baraza ka mawaziri.

Hoja ya pili katika hili suala ni je ina maana hivyo vigezo ulivyovitaja vya elimu, weledi, uzoefu utayari wa kufanya kazi vinapatikana kwenye kundi moja tu la demografia?, Watu 23 siyo wengi, na ni dhahiri watu wa vigezo unavyovitaka wamo wa kutosha tu katika society(nafasi zile 10 za rais), na wengine wa kutosha wamo ndani ya bunge (Wazanzibar kwa wabara) . Kwa nini watu wa imani moja wawe ni wengi katika hiyo selection wakati vigezo havuchagui imani ya mtu, jama unavyo unavyo tu

Kwa hiyo kwa muktadha huu, naona uteuzi uliofanyika kuwa sampling iliyofanywa kimakusudi(na imekuwa based kwenye dini ukuachilia mbali vigezo vingine(purposeful sampling blocked on religion as a selection criteria), ndiyo maana laiti wangewekwa mawaziri wazanzibar kuna high chance wangekuwa waislamu na hivyo kuraise number ya waislamu kwenye cabinet. Sasa kwa kuwa blocking inafanyika kwa mrengo wa kidini, basi wateuaji wakaona hata Wazanzibar wasiwemo kwenye hilo baraza potelea mbali maana uwemo wao utaharibu mahesabu yao ambayo katika sampuli yao, blocking imebase kwenye dini (Si unajua wazanzibar more than 99% waliomo bungeni ni waislamu) .

Huhitaji kuwa ni Genius kuliona hilo kuwa kuna udini wa aibu katika teuzi hii
 
Kwa hiyo kwa muktadha huu naiona sampling iliyofanywa kimakusudi(na imekuwa based kwenye dini ukuachilia mbali vigezo vingine(purposeful sampling blocked on religion as a selection criteria) !

Mawili,

  1. Kadiri hoja yangu inayoanzia kwenye meritocracy, inavyohusika, ndugu wa familia moja wanaweza kuingizwa katika Baraza la Mawaziri na likatekeleza majukumu yake, isipokuwa pale kwenye mgongano wa kimaslahi unaokwamisha ufanisi.
  2. Kwenye utafiti, focused sampling, as opposed to randome sampling, inaruhusiwa pia, ilimradi kuwepo na justification.

Mengine yanajadilika.
 
Nikiangalia hili baraza la mawaziri, by all standards haliakisi sura ya Taifa na kwa hiyo halisaidii kwa namna yoyote kuimarisha umoja wa Kitaifa.

1. Hivi inawezekana vipi uje na baraza la Mawaziri la watu 23 lakini lenye Waislamu 3 tu?

Takwimu hizi ni 87% Wakiristo, na 13% Waislamu. Je, hii maana yake ni kwamba asilimia kubwa ya watu wanaoweza kufanya kazi ya kuendesha serikali yetu katika nchi yetu more than 80% ni watu wa dini moja? Hili linaacha maswali mengi. Lakini haya sishangai, inaonyesha tu kuhusu ujeuri wa mamlaka za uteuzi, Waislamu hili suala wamelilamikia sana, Mwaka 2016 Sheikh Khalifa alilisemea, Kisha mwaka huu kwenye Waraka wa shura ya maimamu Sheikh Ponda alilisema.

Binafsi sioni kama ni weledi wa kiungozi kutoheshimu demography za nchi yako katika kuunda timu ya kufanya nayo kazi. Naiona kama ni udini wa dhahiri tu ambao unashuhudiwa na aina ya teuzi zilizofanyika toka muhula wa kwanza wa serikali hii!. Je, Waislamu wanapenda haya? - La hasha, lakini pamoja na hayo Wa kulaumiwa pia ni viongozi wao, hawajitambui, hawajielewi, wanapigana mishale wao kwa wao badala ya kusimama kwa sauti moja ya kuangalia maslahi ya watu wao. Angalau Sheikh Ponda anajitambua, aliliona hili.

2. Baraza la Mawaziri halina Waziri hata mmoja kutoka Zanzibar
Zipo wizara za muungano, hakuna waziri hata mmoja wa wizara hizo ambaye ni Mzanzibar. Ni yaleyale niliyoyasema kwenye nukta ya juu. Huwezi kuunda timu ya mambo ya nchi isiyozingatia demography za kitaifa. Kwa mfano Huwezi mathalani ukachukua watu kutoka Kanda moja ukaunda baraza la mawaziri halafu ukasema eti hawa vigezo vyao vinatosha, Well hata kama vinatosha je wao peke yao ndo wenye vigezo? . Lakini katika hili Wazanzibar wa CCM nao wajilaumu wenyewe, Wameamua kuitoa nchi yao kwa Tanganyika "iwasimamie" basi wacha nchi yao igeuzwe mkoa, yaani hata mawaziri kutoka kwao ni hiyari tena kama ilivyo mawaziri kutoka Mtwara, Mwanza au Tanga

3. Idadi ya Wanawake ni ndogo katika baraza zima la Mawaziri

Sijajua kama ilikuwa ni vision ya kitaifa au ni maono ya kiuongozi tu wa serikali za awamu ya tatu na nne. Lakini kuna kipindi tumewahi kuwaza 50/50. Japo kwa maoni yangu hiyo siyo hoja, lakini kwangu hoja ya msingi ilikuwa ni kuwa lazima katika vyombo vya mamlaka na maamuzi jinsia zote zionekane vizuri siyo kuwa na mfumo uliolalia upande mmoja kupita kiasi (mfumo dume), Sasa wanawake wa kutosha wapo, kwa nini baraza la mawaziri liwe na wanawake kiduchu sana kwenye hili baraza?

Kwa hiyo ukiniuliza kuhusu hili baraza nitakwambia kuwa:
a)
Hili baraza linanuka udini, ni as if Magufuli katuletea parokia ya Mtakatifu Joseph, haliakisi demography ya kitaifa ya kwamba nchi hii ina watu wengi wa imani zote hizi mbili. Nilitegemea kuona baraza lenye sura ya kitaifa, lakini naona baraza lenye sura ya Tanzania ya Kikristo zaidi

b) Hili ni baraza la Tanganyika, yawezekana vipi usiwe na baraza lenye waziri kamili hata mmoja Mzanzibar?

4) Ni baraza la Mfumo dume - Ratio ya akina mama katika baraza hilo siyo wakilishi, sioni ni kwa namna gani baraza hilo linasaidia kuondoa mfumo dume

Namshauri Magufuli atengue hilo baraza kabla ya kuliapisha. La sivyo litampa tabu kwenye kubalance force za kijamii za kitaifa.

Katika kipindi hiki ambapo jumuia ya kimataifa inamnyooshea kidole juu ya aina ya utawala wake, ingekuwa busara kujaribu kubalance force za ndani, ingemsaidia sana.

Ila akizidi kukataliwa ndani ya nchi na nje ya nchi, basi ajiandae kutumia miguvu zaidi kutawala katika kipindi hiki cha miaka mitano, kwa sababu kutakuwa na silent rejection ya utawala wake ndani ya nchi na hii itamsumbua sana!
Waislamu bwana shida tupu.Ungejua hata kwamba Rais hakuwa na mawazo ya udini wala unzanzibari alipokuwa ana-zoom kutafuta mawaziri! I believe he was more interested in professionalism.Be positive,mawazo hasi hayatawafikisha popote,mtajiletea visukari na pressure bure wakati mwenzenu hata hayuko huko.
 
Moja: Balaza la Mawazili ni pamoja na manaibu, je manaibu wale hujawaona?!?

Mbili: Balaza la Mawazili ni pamoja na Makamu wa Raisi, Waziri Mkuu, Raisi wa Zanzibar, hawa nao ni makafiri?!? ewe uliyedini ya 'kweli'

Tatu: Nafasi za uongozi si zawadi, kwa dini, makabila, mikoa; hadi liwe ni swala la kufa na kupona, kwamba ni lazima dini, kabila, mkoa upate
Huku kwetu wanasema, mwenye kisu kikali ndiye anayekula nyama... Ukiona wa kuja kapata nyama na wewe uliyemswaga ng'ombe toka maporini umekosa, basi ujue mwenzio ana kisu kikali kukuzidi.. Usinune.. Ndio kanuni ya mchezo.. Kanuni ya mchezo ni mwenye kisu kilali, ale...
Badala ya kununa, badili mahesabu... Ukiwa na kisu butu, usimswage ng'ombe na rungu, mpige bapa moja uambulie hata nundu.. By the time ng'ombe anafika machinjioni, tayari we ushabeba shea yako.
Mahesabu yakigoma kabisa, tumia kanuni ya pili ya mchezo: Hii inaitwa, tukose wote.. Ukiona kisu chako butu na uhakika wa kula nyama ni mdogo, usimswage ng'ombe kwenda machinjioni.. Mswage atumbukie kwenye kisima, MKOSE WOTE!
 
Kwani ni lazima kuteua waziri toka huko wapi katiba imesema hivyo mbona wao hawateui toka bara!
Muungano ufe tu kila mmoja akae kwake maana hata Zanzibar sasa wameanza kuzinduka hawataki mambo mabaya ya BOT kuwapora watu pesa zao pindi zikitumwa tokea nje, sasa kwa Zanzibar wao ni ruksa pesa zozote kutumwa Zanzibar hawataki usumbufu kwa pesa inayoingia huko wanataka pesa ziingie zilete maendeleo
 
Rais angekuwa ni muislamu na akateua waislamu wakutosha (kama nusu tu ya baraza zima), leo jumapili makanisani zingesomwa nyaraka za maaskofu kuipinga serikali, mahubiri na maombi yangekuwa ni kuipinga serikali, wakristo wangeambiwa wafunge siku kadhaa dhidi ya uislamu kushamiri hapa Tz nk.

Viongozi wa kikristo nawajua vizuri.
Bakwata ni Tawi la CCM wataendelea kupata ruzuku tokea CCM hawaoni tabu waislam kupungua kwenye baraza la mawaziri ambalo 11 wanatoka kanda ya ziwa
 
Sasa ile si serikali ya Zanzibar hii ya magufuli ni serikali ya muungani kati ya Zanzibar na Tanganyika
Zanzibar huwa na Serikali yake baraza la wakilishi hata bunge lao hakuna mbunge tokea Tanganyika, bora kila upande uende kivyake ili Zanzibar ianze kufanya maendeleo yake bila kubugudhiwa na Tanganyika
 
Mawili,

  1. Kadiri hoja yangu inayoanzia kwenye meritocracy, inavyohusika, ndugu wa familia moja wanaweza kuingizwa katika Baraza la Mawaziri na likatekeleza majukumu yake, isipokuwa pale kwenye mgongano wa kimaslahi unaokwamisha ufanisi.
  2. Kwenye utafiti, focused sampling, as opposed to randome sampling, inaruhusiwa pia, ilimradi kuwepo na justification.

Mengine yanajadilika.
Bila checks and balances kwa mteuaji na kwa aina ya katiba tuliyonayo hiyo unayosema "bila ya mgongano wa kimaslahi" haiexist, maana hata mgongano wa kimaslahi ukiwepo atakwambia haupo na hata ukiwa na proof kuwa upo bado ana loophole nyingi tu za kuendelea na akitakacho yeye!

By the way Nepotism haijawahi kukubalika kama positive action ya namna ya kuongoza au kutawala!
 
Muungano ufe tu kila mmoja akae kwake maana hata Zanzibar sasa wameanza kuzinduka hawataki mambo mabaya ya BOT kuwapora watu pesa zao pindi zikitumwa tokea nje, sasa kwa Zanzibar wao ni ruksa pesa zozote kutumwa Zanzibar hawataki usumbufu kwa pesa inayoingia huko wanataka pesa ziingie zilete maendeleo
Mtajua wenyewe na muungano wenu!
 
% ya Wakristo Zanzibar ni ndogo kuliko ya Baniani huku bara, ushawahi kusikia mtu anajadili kwanini Baniani hawapati fursa za kiutumishi serikalini bara?
Zanzibar hawatambui ukiristo wao ni waislam 100/%
 
Ndugu zangu Waislam bara na visiwani msiwe mashaka. Mwenyezi Mungu yupo na atayajibu. Ila niwakumbushe mnawatu imara Sana pale juu kuanzia Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Mam Samia. Msimsahau waziri Jafo Ila Jaji Mkuu embu ndugu wa Islam msimsahau huyu Mh ktk Salah zenu mwekeni mbele za Mungu Jaji Mkuu wa Taifa. Hili. Amin
Waislam wapewe wizara ya Ulinzi na wizara ya fedha ili waone kama wanathaminiwa washike pesa na pia washike mabunduki yote
 
Kama tumefika hatua ya kuanza kuuliza waislamu, wakristo na wapagani ni wangapi kwenye taasisi basi tumefirisika sana kimtizamo.
Bakwata ni Tawi la CCM ndiyo maana wapo busy kuulizia waislam wenzao
 
Bila checks and balances kwa mteuaji na kwa aina ya katiba tuliyonayo hiyo unayosema "bila ya mgongano wa kimaslahi" haiexist, maana hata mgongano wa kimaslahi ukiwepo atakwambia haupo na hata ukiwa na proof kuwa upo bado ana loophole nyingi tu za kuendelea na akitakacho yeye!

By the way Nepotism haijawahi kukubalika kama positive action ya namna ya kuongoza au kutawala!
Mawili tena,
  1. Ukaguzi wa kuangalia uzingatiwaji wa taratibu (compliance audit) unaanzia kwenye kigezo kilichotamkwa kama mwongozo wa tabia kabla ya zoezi la kufanya ukaguzi. Kwa hiyo, naona tunachanganya mtiririko wa kimantiki. Tuweke vigezo vya uteuzi kwanza, halafu tupime uzingatiwaje wake, na sio kinyume chake.
  2. Kuhusu nepotism: kila kiongozi analo kabila, dini, mbari, etc, lakini hilo halimaanishi kwamba ni mkabila, mdini, mbaguzi wa rangi, n.k. Lakini, hilo halituzuii kuweka vigingi vya kuzuia ukabila, undugunaizesheni, udini, urangi, nk. Wanadamu sio wakamilifu.

Mengine yanajadilika.
 
Rais Mkristo
Makamu wa Rais Muislam
Waziri mkuu Muislam
Jaji Mkuu anaemuapisha Rais Muislam
 
Back
Top Bottom