Leo wapinga Uislam mpo na Waislam, amma kwa hakika Uislam una nguvu za ajabu.
Huo moto unatokea upande mwingine, baada ya ule wa Escrow. Ccm andaa mchanga na zimamoto.
Hii nchi haina dini jamani. Kila dini/dhehebu likitaka mahakama yake tutafika wapi jamani? Ndugu Waislamu litafakari zaidi hili. Ndio maana hata kufungisha ndoa ni mamlaka ya dini husika na serikali haigharamii shughuli za ufungishaji ndoa za wakristo wala waislamu
Taasisi ipi, jumuiya ya waislam au bakwata?
Kwa kukusaidia bakwata imeasisiwa na nyerere na ndio muhimili mkubwa CCM kwa maswala ya uchaguzi
FF mimi kutokua muislamu haimaanishi siupendi au naupinga uislamu maana katika mfumo wangu wa kuabudu sijawahi kuathiriwa na uwepo wa uislamu.Na maisha yangu naishi na waislamu na ndio marafiki zangu wakubwa.ndio maana nikasema hata ikianzishwa sidhani kama itaathiri imani yangu au mfumo wangu wa kimaisha.So ianze tu kwa sababu kama nyie mtakua Happy kwa uanzishwaji wa mahakama hiyo basi itakua ni neema kwa nchi yote.
Ni lazima Serikali iwaambie waislam ukweli. Lazima tukubali kwenye nchi ambazo zina serikali za ki-secular kama ya kwetu ni ngumu kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu kama za Saudi Arabia au Kuwait.. Hata huko Zanzibar mtu akiiba hawampeleki kwa kadhi ila Jamhuri ndiyo inamfungulia mashtaka....
Lazima tufahamu sheria zimegawanyika katika mafungu mawili makubwa..
(i) Public Law.. Hizi zinalinda maslahi mapana ya umma kwa maana ya Jamhuri, Mfano sheria za jinai nk. Hapa mtu akifanya kosa anashtakiwa na Jamhuri... yule uliyemdhuru anabaki kuwa shahidi tu.. hapa hakuna dini, kabila, utamaduni wala rangi ya mtu.. Kama umefanya kosa lazima utashakiwa kwa kuvunja sheria za nchi na kwa minajili ya kulinda maslahi mapana ya taifa..
(ii) Civil/private Law.. Hizi zinasimamia maslahi ya mtu mmoja mmoja.. Mfano sheria za mikataba, ndoa nk. Hapa ni mtu vs mtu.. na sheria itakayotumika ni ile ambayo kosa limeangukia.. Kama ni mgogoro wa ndoa basi mgogoro utatatuliwa ama kwa kutumia sheria za kimila kama ndoa ni ya kimila, kama ni ya kiislam itabidi utumike utaratibu wa kiislam vivyo hivyo kwa ndoa ya kikristo..
KWANINI MAHAKAMA YA KADHI NI VIGUMU KUFANYA KAZI TANZANIA.??
Mahakama ya Kadhi inaendeshwa kwa kutumia Sharia Law, kwa maana ya kitabu kitakatifu cha Quran, Hadithi za Mtume nk. na lazima utambue kuwa Uislam ni mfumo uliokamilika kwa maana ya taratibu, sharia, mira, desturi, imani/dini vyote vinakwenda kwa pamoja. Sasa ili Mfumo huu uweze kufanya kazi kwa ukamilifu wake unahitaji watu wenye tamaduni, mila, desturi imani/dini moja.. Hivyo Sheria zake zinakuwa rahisi kusimamiwa na Serikali kwa sababu watu wote ni wa Mfumo mmoja..
Lakini kwa nchi kama ya kwetu yenye mchanganyiko wa sio tu dini, bali pia tamaduni, desturi mila na kadharika ni ngumu ku-impliment Sharia Law.. Na kwa sababu tunaishi katika Jamhuri mmoja lazima kuwepo na mfumo ambao utaweza ukawajumuisha watu wenye imani, dini na tamaduni tofauti.. yaan Secular state...
Kwa mchanganyiko wa jamii yetu.. kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu ni ndoto za mchana na lazima Waislam wakubali ukweli huo.. Chukulia Mkristo kaibiwa na Muislam.. au Muislam kaibiwa na Mkristo utatumia Sheria gani hapo ili kutenda haki????
Lazima ukweli ubaki ukweli!! Tatizo limeletwa na CCM kwa kuwapa Waislam matumaini makubwa yasiyotekelezeka ili wajipatie kura..
Niwashauri tu ndugu zangu waislam lazima tujitahidi kujenga Taasisi zetu zenye nguvu, ueledi na fedha ili kuwatumikia waislam kwa yale mambo ya kiimani na kijamii tu. La sivyo hakuna kitu hapo..
Halafu walivyo wabinafsi,ubovu pekee wa Katiba pendekezwa ni kukosekana kwa Mahakama ya Kadhi.
Hapa siitetei CCM. Uislam kwanza kuliko kingine chochote.
Hapa ndipo ninaposhindwa kuwaelewa waislamu.
★kwanza,unawezaje kulinganisha maakama ya kadhi na mahakama ya ardhi au biashara?! Mimi James nikichukua ardhi ya Juma basi Juma atanishtaki mahakama ya ardhi,na mwishowe Juma atapata haki yake! Sasa je Juma akiamua kunipeleka mahakama ya kadhi,mm James nitaridhika vpi kama kuna haki imetendeka?
★Au tufanye Anna ameolewa na Haji then Haji akafariki..na ndugu zake Haji wakataka mirathi igawiwe na mahakama ya Kadhi!unadhani mahakama itawatambua watoto na mama yao kama warithi halali?!
★Pili sifa zakuajiliwa kwenye hiyo mahakama zitakuwa zipi!kitakachotokea ni waislam tu ndio watakao pata ajira huko!sasa hii itawafanya wakristo wakose hizo ajira kabla hata haijatangazwa wakati wao pia huchangia kulipa mishahara ya hao wafanyakazi wa mahakama ya kadhi.
Hao waislam wasaliti waliishabikia katiba ya sita na ya chenge sasa mnamlilia nani
Soma vizuri wewe, wamesema wameitoa rasimu ya warioba na kuweka ya kwao, hapo wamesema hivyo kuepuka kuambiwa wameingilia siasa.
Siipendi CCM, lakini kwa suala la Mahakama ya kadhi, naiunga mkono CCM 100%.
NSSF ni Mini-Kadhi cort.
Mlizoeya mno kuwacheza "SHERE " Waislaamu kwa myaka mingi, na sasa khitami yenyu ndo hini muionayo.
Umoya na Ufahamu wao juu ya hitajio kunako yao "DINI" kumewatosha kuwarejeza pamoya.
Sasa kazi kwenyu "MAKAAFIRI" na zenyu hasada ukomo wake ndo sasa.
Hapa mtajaumia sana.
Msome tu humu utamuelewa.
Kama Nyerere alikuwa kwanza Kanisa halafu ndiyo nchi basi FaizaFoxy kwanza Uislam kabla ya chochote kile.
Huwa hawajitambui watu hawa. Wao wanafuataga upepo tu. Leo wapo huku kesho wapo kule.
Wewe umepotoka au pombe zinakusumbua, hakuna nchi ulimwenguni ambayo ina waislamu hata kwa asilimia 40% kusiwe na Mahkama ya kadhi ambayo inatambuliwa kikatiba ili kuweza kikidhi matatizo na waislamu kupata haki zao. Tanzania Bara peke yake waislamu hawawezi kupungua asilimia 60% si kwambii Zanzibar ambao ni 99% waislamu.
Waislamu tunaelewa ukishakuwa mkiristo basi ata haki unaweza kuikataa na kupinga kupinga tu mana ndivyo ukiristo. Ivi wewe ulitegemea waislamu haki zao zikatatuliwe na mahakama zenu za ki-mission ambazo hawana taaluma juu uislamu?.
Ivi nyinyi Nyerere munamchukuliaje kama nabii ama mtu aliyekuwa na sifa ya kipekee tofauti na mwanadamu wa kawaida kwamba amesema Tanzania haina dini na nyinyi munatii tu.
Dunia inakuwa wakati wa Julius Nyerere sio wakati wa sasa, sasaivi kuna mambo mbali mbali yanahitaji ufumbuzi waislamu wameona kuna haja ya kuwa na Mahkama ya kadhi tena itambuliwe kikatiba ili matatizo yao yaweze kuwa solved kwa mujibu wa dini yao ilivyotaka, Kama ukiristo haukufundisha nyinyi kuwa na mahkama, Uislamu kwa mujibu wa Quran inafahamisha ivyo kwanini munaleta porojo porojo ambazo hamna elimu nazo?.
Waislamu walio Tanzania nao ni Watanzania hawana sehemu nyengine ya kwao ila Tanzania kwanini wanyanyaswe?