Ni lazima Serikali iwaambie waislam ukweli. Lazima tukubali kwenye nchi ambazo zina serikali za ki-secular kama ya kwetu ni ngumu kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu kama za Saudi Arabia au Kuwait.. Hata huko Zanzibar mtu akiiba hawampeleki kwa kadhi ila Jamhuri ndiyo inamfungulia mashtaka....
Lazima tufahamu sheria zimegawanyika katika mafungu mawili makubwa..
(i) Public Law.. Hizi zinalinda maslahi mapana ya umma kwa maana ya Jamhuri, Mfano sheria za jinai nk. Hapa mtu akifanya kosa anashtakiwa na Jamhuri... yule uliyemdhuru anabaki kuwa shahidi tu.. hapa hakuna dini, kabila, utamaduni wala rangi ya mtu.. Kama umefanya kosa lazima utashakiwa kwa kuvunja sheria za nchi na kwa minajili ya kulinda maslahi mapana ya taifa..
(ii) Civil/private Law.. Hizi zinasimamia maslahi ya mtu mmoja mmoja.. Mfano sheria za mikataba, ndoa nk. Hapa ni mtu vs mtu.. na sheria itakayotumika ni ile ambayo kosa limeangukia.. Kama ni mgogoro wa ndoa basi mgogoro utatatuliwa ama kwa kutumia sheria za kimila kama ndoa ni ya kimila, kama ni ya kiislam itabidi utumike utaratibu wa kiislam vivyo hivyo kwa ndoa ya kikristo..
KWANINI MAHAKAMA YA KADHI NI VIGUMU KUFANYA KAZI TANZANIA.??
Mahakama ya Kadhi inaendeshwa kwa kutumia Sharia Law, kwa maana ya kitabu kitakatifu cha Quran, Hadithi za Mtume nk. na lazima utambue kuwa Uislam ni mfumo uliokamilika kwa maana ya taratibu, sharia, mira, desturi, imani/dini vyote vinakwenda kwa pamoja. Sasa ili Mfumo huu uweze kufanya kazi kwa ukamilifu wake unahitaji watu wenye tamaduni, mila, desturi imani/dini moja.. Hivyo Sheria zake zinakuwa rahisi kusimamiwa na Serikali kwa sababu watu wote ni wa Mfumo mmoja..
Lakini kwa nchi kama ya kwetu yenye mchanganyiko wa sio tu dini, bali pia tamaduni, desturi mila na kadharika ni ngumu ku-impliment Sharia Law.. Na kwa sababu tunaishi katika Jamhuri mmoja lazima kuwepo na mfumo ambao utaweza ukawajumuisha watu wenye imani, dini na tamaduni tofauti.. yaan Secular state...
Kwa mchanganyiko wa jamii yetu.. kuwa na Mahakama ya Kadhi yenye nguvu ni ndoto za mchana na lazima Waislam wakubali ukweli huo.. Chukulia Mkristo kaibiwa na Muislam.. au Muislam kaibiwa na Mkristo utatumia Sheria gani hapo ili kutenda haki????
Lazima ukweli ubaki ukweli!! Tatizo limeletwa na CCM kwa kuwapa Waislam matumaini makubwa yasiyotekelezeka ili wajipatie kura..
Niwashauri tu ndugu zangu waislam lazima tujitahidi kujenga Taasisi zetu zenye nguvu, ueledi na fedha ili kuwatumikia waislam kwa yale mambo ya kiimani na kijamii tu. La sivyo hakuna kitu hapo..