1. Mahakama ya kadhi kwa faida ya nani?
2. Mahakama ya kadhi aanzishe nani?
3. Mahakama ya Kadhi kwa ajili ya nini?
4. Mahakama ya kadhi kwa gharama ya nani?
5. Civil court /civil law zimekwenda wapi?
6. Hukumu ya kadhi ikipingwa rufaa itakatwa wapi?
7. Anayepinga hukumu ya m/kadhi atafanywa nini? Kama kukamatwa atakamatwa na nani?
8. Mwislamu akizaa na mkristu,wakigombania mtoto kadhi akaamua mtoto afuate mzazi mwislamu Je mkristo akikataa kwa vile hatambui kadhi itakuwaje?
9. Kanisa katoliki lina mahakama inatumia canon law kwa mambo ya ndani ya kanisa,lakini haijawahi kuomba itambuliwe na serikari/haikuanzishwa na serikari/wala haiombi kuendeshwa na fedha za serikari!
Kwa sasa mahakama ya kadhi si habari,habari ni wizi/ufisadi/huduma mbovu za afya/elimu/ maji.
Lakini pia ,mnaweza kuanzisha mahkama ya kadhi hata kesho alfajiri nyie wenyewe na mkaendesha mtakavyo. Serikari inatambua dini,lakini haina dini.