benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,533
- 3,187
Baraza la Biashara la Afrika Mashariki limemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukabidhi ardhi kwa baraza hilo yenye ukubwa wa hekta tatu.
Hati miliki ya ardhi hiyo namba 4/2 iliyopo eneo la Mateves mkoani Arusha, ilipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa EABC, John Bosco Kalisa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bodi, Menejimenti na Uanachama wa EABC, Anjelina Ngalula, ardhi hiyo ina mita za mraba 12,355 na italiwezesha baraza hilo kujenga Makao Makuu yake jijini Arusha, Tanzania ambako pia ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Ngalula alisema hatua hiyo itaiwezesha EABC kutekeleza majukumu yake kama sauti ya sekta binafsi EAC na kuwezesha maono ya Afrika Mashariki isiyo na mipaka kwa biashara na uwekezaji.
"Dhamira ya baraza ni kutetea mazingira mazuri ya biashara na kukuza ukuaji endelevu unaotokana na sekta binafsi katika Kanda ya Afrika Mashariki," alisema. Alisema alichokifan ya Rais Samia ni ushuhuda wa uongozi mkubwa katika kukuza nafasi ya sekta binafsi kama injini ya ukuaji wa kijamii na kiuchumi katika kanda ya EAC.
Alisema EABC inampongeza zaidi Rais Samia kwa dhamira yake ya dhati ya kuongoza ajenda ya ushirikiano wa kikanda ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na kupigania uhusiano wa karibu wa kibiashara kwa kuongeza ustawi kwa Waafrika Mashariki wote.
Ngalula alisema EABC imedhamiria kwa dhati kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha biashara ya ndani ya EAC, viwanda, uwekezaji na utengene zaii wa ajira.