Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki lafanya Uchaguzi wa Rais, Makamu na Katibu Mkuu

Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki lafanya Uchaguzi wa Rais, Makamu na Katibu Mkuu

Wanabodi,

Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania katika mkutano wake Mkuu wa 77 uliofanyika makao makuu Kurasini kuanzia tarehe 21-25 Juni 2021 walifanya uchaguzi wa Viongozi watakaosimamia wa shughuli za baraza katika miaka mitatu ijayo kuanzia 2021 mpaka 2024

  • Baraza limemchagua Mhashamu Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga kuwa Rais wa Baraza kwa awamu ya pili
  • Limemchagua Mhashamu Askofu Flavian Kassala kuwa makamu wa Rais kwa awamu ya Pili
  • Limemteua Katibu Mkuu, Padre Charles Kitima kwa awamu ya pili
  • Limemteua Mheshimiwa Padre Chesco Msaga kuwa naibu mkuu wa Baraza kwa kipindi cha miaka mitatu
CCM! CCM! CCM! Rais huchaguliwa kwa kura ya siri kwa kipindi cha miaka 5, ikiisha anachaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka 5, basi. Rangi zao ni rangi za Yanga. CCM! CCM! CCM!
 
Uaskofu katoliki ukweli sio ule wa kanisa la agano jipya la karne mbili za kwanza. Imekuwa ni taasisi ya kiserikali mtindo.
Kwa ujumla ni mtindo wa kibinadamu zaidi ya uongozi wa roho mtakatifu.
 
Kazi iendelee. Hawa TEC mambo yao yako systematic..huwasikii wakifanya siasa nyingi,wakigombania vyeo. Imenikumbusha wale wa ELCT,ilikuwa ngumi mkononi.. Tujifunze

KKKT Mkuu wa Kanisa anachaguliwa na Maskofu wote Tanzania.

Catholic Askofu anateuliwa na Papa huko Vatican.Tena Papa mwenyewe mzungu sasa sioni cha kujivunia huko Vatican.
 
Chumbani ni Vatican sio huko Buza kwa mpalange.
MAPADRE NI WENGI MNO TZ, NA MAJIMBO NI MACHACHE MNO "every priest is possible candidate " THOSE WITH MERITS

UASKOFU SIO UJI ,AU ASALI KWAMBA KILA MTU AONJE/ARAMBE...[emoji2357][emoji1787][emoji1787][emoji2][emoji2]

By the way mchakato wa kumpata ASKOFU sio rahisi kama unavyofikiri!

Kitima ni Intellectual anapaswa kutumiwa effectively na Kanisa katoliki.

Kumpa uaskofu anakuwa limited!

Mengine ni MAMBO YA CHUMBANI...

we Ishia hapa sebureni PANAKUTOSHA.

Tuachie wenyewe tuliopo KANISANI.
 
hongera kwao, kumbe huwa rais wao wanamchagua nilijua ni mzunguko kwa kila askofu.
 
Kwani wewe baba yako huwezi kumpa heshima ya uheshimiwa?

Wale ni wageshimiwa ndio.
Au mbunge musukuma kwako ndio muheshimiwa?
Mimi mwenyewe ni Mkatoliki, lakin kumuita padri muheshimiwa hapana. Waitwe tu baba. Uheshimiwa tuwaachie wanasiasa.
 
Mimi mwenyewe ni Mkatoliki, lakin kumuita padri muheshimiwa hapana. Waitwe tu baba. Uheshimiwa tuwaachie wanasiasa.
Hivi vyeo vya uheshimiwa ni mbwembwe tu, yaani mtu mwenye PhD amwite kibajaji na msukuma waheshimiwa na elimu yao ya kwenda kuvulia samaki feri.....si bora hiyo title umpe padri maana anayo madini ya kutosha kichwani.
 
Hivi vyeo vya uheshimiwa ni mbwembwe tu, yaani mtu mwenye PhD amwite kibajaji na msukuma waheshimiwa na elimu yao ya kwenda kuvulia samaki feri.....si bora hiyo title umpe padri maana anayo madini ya kutosha kichwani.
Mtumishi wa Mungu unamwita muheshimiwa? Mbona kwenye biblia hatujaona Elisha na Eliya wanaitwa waheshimiwa na wamefanya mambo makubwa sana
 
Back
Top Bottom