Dada halima najua uko poa kabisa
Madhumuni ya barua hii ya wazi ni kutaka kukufikishia ujumbe ufuatao
Kuna taarifa nimezipata chini ya kapeti zikisema kuwa asilimia kubwa ya Wabunge wanaume ambao wamekosa ubunge ndio wanapambana nyie wakina mama msiende viti maalum
Napenda kukwambia kuwa hao wabunge wanasema nyie msiende ni kwa sababu ya ubinafsi wao tu. Hii fursa ingekuwa ya wao wanaume wasingewasikiliza nyie kabisa ingekuwa wameshaenda long time
Wewe ndio kiongozi wa wanawake CHADEMA please acha kusikiliza hao wabinafsi, peleka majina ya akina mama wenzako ili mkatetee Chama
Miaka yote CHADEMA huwa hairidhiki na matokeo ila huwa wanaenda Bungeni hiyo ni kwa sababu wanaume wengi walikuwa wanachaguliwa
Najua una changamoto sana juu ya suala hili but be strong and peleka majina tume. Mwanaume ambae anakwambia msiende bungeni then mwambie avae sketi aende yeye.
Mi-ccm kazi mnayo. Kwamba ni huruma, kuumia, kuchukizwa au ni nini hasa kinachowasukuma kuhangaika na CDM hivi? Hata usingizi mnapata kweli?
Nyie ndiyo leo mmegeuka kuwa washauri wa CDM? Huko kwenu mlishamaliza kazi ya kumshauri jiwe japo akafahamu "#lives_of_others_matter?"
Kwa hiyo unataka apeleke majina ya wabunge wa kuitetea CDM ambayo CDM yenyewe haitaki waende kufanya kazi hiyo? Hizi kweli ni akili au ndiyo matope yenyewe?
Labda ungependekeza tu waende kuwatetea nyie? Bila shaka hapo ndipo angewaelewa vyema?