Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Kikilacho ki nguoni mwako,walisema wahenga walisema.

Maswali ni je kirusi kimetikana na nini? Kimesababishwa na nini? Je ni CDM wenyewe au ni wapinzani walio nje ya CDM? Je Lwakatare anaweza kununuliwa? Kwa kuwa yeyote ailiyetengeneza hiyo video kama ni ya kweli au uongo amevua "gloves" Je CDM nao wamevuwa "gloves"?

This has gone past a decent political game and if your opposition is dirty,you have got to go dirtier? Je CDM imefanya audit ya phone records za vingozi wao wote walio karibu na vingozi wao?
 
Ni kweli kuna kirusi. Lakini tujiulize maswali rahisi.
1. Mwenendo wa zzk tangu ishu PM7 hadi kutimuliwa shonza et al unaridhisha? 2.Ni kweli zzk hamjui Ben SaaNane? 3.Kwa nini tuamini memo imevuja kupitia ofisi na si kwa zzk mwenyewe?
 
Uko vizuri sana zitto ndio maana niliwahi kukushauri kwamba usiwe na waasiwasi na issue za uraisi hizo zitajipanga zenyewe maana wanachama tunaona nani anabidii na tutampigania vipi ila naomba uwe taratibu mwisha utampata tu aliyeweka huo uzushi hapa JF.
 
"Huu ni wakati wa kuwa na umoja na mshikamano kuliko wakati wowote katka uhai wa chama" ahsante sana zitto tumekuelewa
 
mimi naamini barua imevujia mikononi mwa Zitto, sidhani kama hicho kirusi kingekua jirani na Dr.Slaa kingejihangaisha kufuta saini ya Zitto.!!
 
Nikisoma maelezo ya Zitto halafu nikiunganisha na ule uzi wa Chadema vipande vipande naanza kupata wasiwasi. Wasiwasi wangu unajengwa na mambo yafuatayo:

  • Kwamba kuna kiongozi Mwandamizi wa Chama anakamatwa, halafu kila kiongozi anaongea mambo yake. Ina maana hakuna teamwork hapo.
  • Naibu Katibu Mkuu anamwandika barua Katibu wake mkuu kumshauri mambo ya kufanya (hapa naamini Naibu Katibu Mkuu hakutoa maagizo na masharti kwa katibu - maana kama ni hivyo itakuwa jambo jingine). Hapa maana yake ni kwamba Viongozi hawa hawakai pamoja na wala hawawezi kupigiana simu kama kuna tatizo limetokea. Hadi inafikia Naibu Katibu Mkuu anamwandikia barua Katibu Mkuu maana yake hakuna njia nyingine za mawasiliano zenye kuonyesha rutuba ya uhusiano zaidi ya hii formal process.
  • Ukisoma maelezo ya Zitto kuna kitu kama kutokuaminiana vile ndani ya CDM (yeye kaita kirusi).
Hayo ni mambo yanayonitia wasiwasi na CHADEMA kama kweli mmeamua kufanya kazi ya siasa au mnataka kucheza na akili za Watanzania.

Mimi ningewaambia viongozi wa CHADEMA, kuongoza chama cha siasa siyo favour kwa watanzania. Kwa nini nasema hivyo? Ni kwamba watanzania walikubali mfumo wa vyama vingi ili kutengeneza checks and balances na mfumo huo unaendeshwa kwa kodi zao (ndiyo maana CHADEMA wanapata ruzuku kama vyama vingine vyote vyenye wabunge, akina Mbowe, Zitto na wengine wanalipwa mafao kibao kutoka bungeni na kupewa safari). Sasa kama hawawezi kuongoza mfumo mzuri wa checks and balances na kuanza kuchezea akili za watanzania wajiuzulu.

Yaani ukiangalia hii sinema unapata wasiwasi na viongozi wanaoaminiwa na watu. Hapa nazungumzia wote. Hebu wajifunze kuwa viongozi wenye maadili. Kama kuna suala linasumbua chama kaeni kwenye vikao vyenu mtafute ufumbuzi. Kuja kutafuta ufumbuzi kupitia JF kwa kweli siyo sahihi. Pamoja na kuwa nyie ni wanasiasa lakini mtambue pia ninyi ni mameneja kwa hicho Chama.

Ni hayo tu kwangu yaani wana JF hizo sarakasi za hawa jamaa zinanikera, wanatakiwa kuwa mature sasa.
 

Bila shaka ni hiki
 
Kubenea where are you? Mwanahalisi nadhani lingekuwepo tungepata kumfahamu who is "HUGO CHAVES"
CDM lazma zitumike mbinu thabiti za kukitambua hichi kirusi na kuki scan earlier.
 
Kwa kweli inaudhi sana kwa sasa jinsi chama chetu kinavyoshindwa kudhibiti uvujaji wa siri za ndani. Kama kuna kirusi kinatoa taarifa nje tena zingine zikiwa ni za siri kabisa basi usalama wa chama upo mashakani sana.

BADO NINAAMINI KUWA ADUI YUPO KATIKATI YA VIONGOZI WAKUU WANOTUNZA SIRI ZA CHAMA. Atafutwe kwa kina. Inawezekanaje kitu kimejadiliwa ndani ya chama na ni siri kwa umuhimu wake kikatoka nje wakati huo huo?

Hapa lazima tuaminishwe kuwa ndani ya CDM kuna adui aliyetumwa kufanya kazi yake barabara. Ndio huyu yupo. Kilichopo kwa sasa ni kufanya uchunguzi wa kina na ikibainika hata kama ni mkubwa mwenye cheo lazima afukuzwe kama wengine walivyofukuzwa.
 
Asante mh ZITTO kwa hatua yako ya kukubali kuwa uliandika barua kwa chama na content ndio hizo ambazo nilieleza, kimsingi barua ile ni ya kweli na maelezo yote ni ya kweli japo uzi wenyewe umeshafungwa... KUDOS ZITTO.
 
labda anamaanisha hapa

labda anamaanisha hapa

Mkuu hili pia ni gumu?!

1.Barua imesainiwa (barua ya zk) iliyoopo mtandaoni haija sainiwa. Kimantiki hizi ni barua mbili tofauti, iliyo sainiwa na kuikabidhi na hii isiyo sainiwa ambayo iliwekwa JF.

2. Ni hapo ulipo pigia mstari, Zk mwenyewe anasema imefanana maudhui, (Kitu kikifanana kina kuwa ndio hicho hicho?! Hili lina hitaji shahada ya chuo kikuu mkuu?!) Maudhui yakifanana hayahalalishi kuwa barua moja.

Elewa kuwa tunajadili barua mbili tofauti zinazo fanana maudhui. Moja ikiwekwa na mtu mwenye same I'd location na yule aliye post video ya Lwekatare (kwa mujibu Zk) na nyingine za Zk aliyo ipeleka chamani.
 
watanzania bado ni wajinga sana...yaani Ben Saanane anawasumbua kiasi hiki? dduh hili taifa la ajabu sana...huyu ni undercover wa serikali. sitaki mjadala tena
 
Last edited by a moderator:
The Boss upo hapo?
 
Last edited by a moderator:
Sio tu ID location bali ni ID ILE ILE. Mods wamesha mstukia na kuziunganisha
 
Tatizo mkuu Zitto huwa unaacha uzushi uendelee kusambazwa afu unakuja kuuzawazisha wakati ni too late.

Anyaway tunashukuru kwa kusawazisha mambo.
 
Last edited by a moderator:
Mi nahisi, baada ya mkuu Zito kuona hasikilizwi, aliamua kuweka barua mtandaoni, ili jamii iamua na imuone ameplay his part.

Vinginevyo sikuona sababu ya yeye kuandika barua, wakati vyanzo vingine vya kupashana habari vipo.
 
Mi nahisi, baada ya mkuu Zito kuona hasikilizwi, aliamua kuweka barua mtandaoni, ili jamii iamua na imuone ameplay his part.

Vinginevyo sikuona sababu ya yeye kuandika barua, wakati vyanzo vingine vya kupashana habari vipo.
Ametumia moja ya njia za kuwasiliana. Angetumia sim ungeuliza kwanini hajaandika barua ili rekodi ibaki kua he expressed his view. na his final view ni view ya chama.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…