Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
MwanaFalsafa1

Labda tu uwoga wa hao wana chadema,kwani CCM imefanya maovu mangapi na iko madarakani?

CCM imehusishwa na Kolimba, KOMBE, ULIMBOKA, MWANGOSI, KADHIA ZA AJALI KUBWA ZA MELI NA TRENI, HALI NGUMU YA MAISHA NA UPUUZI MWINGI SANA WA RUSHWA NA KUTOROSHA NYARA ZA SERIKALI,TENA VIONGOZ WAKE WAANDAMIZI WANAHUSIKA, KUNA ANNABEN,KUNA DOWANS, RICHMOND SASA LEO CHADEMA WANAOGOPA SUALA DOGO KAMA HILI, SI UZUZU HUO?

Mkuu wanasiasa wote ni sawa na lengo lao ni moja nayo ni kushika madaraka. Vyama vya siasa nk ni a means to an end. Huo ndiyo ukweli na ndiyo maana watu wakisha anza kumuona mwanasiasa fulani au chama fulani ndiyo mkombozi mwisho wake ni maumivu. Watu wanatumika na wao kama kondoo wana timiza azma ya wanasiasa kwa niaba yao.

Ukitaka kupima hili angalia hapa hapa barani Afrika na uniambie ni nchi ngapi zilibadilika baada ya upinzani kuingia? Lipi haswa lililo badilika? Angalia Kenya, angalia Malawi pia waweza angalia na Zambia. Ukitaka angalia hata Marekani. 2008 kwenye kampeni zake alivyo gusa hisia za watu na watu wakamuona "Messiah", kaingia madarakani kipi kikubwa kimebadilika?

Sisemi watu waendelee kukipigia kura CCM kwa sababu vyama vyote ni sawa, la hasha ila nataka tu watu wajue kubadilisha vyama madarakani huwa hakuleti mabadiliko kama watu wanavyo dhani.
 
Asante sana mh Zitto kwa ufafanuzi bila shaka hicho kirusi kitajulikana tuu!
Asante kwa majibu matamu! Nilisema tangu jana hapa kuwa pengine barua hii ilikuwa na maudhui aliyo yaandika lakini siyo aliyo iandika! Walitegemea chadema igawanyike lakini wameishia kuiba maudhui a barua tuu!

Alaf kwa taarifa tuu hii barua ililetwa na id ya formfourleaver2012 na ikwa merged na kuwa hugochavez!

Wajipange upya sana na huu ni mkakati hule hule wa kuwachonganisha wanachadema!

tumshukuru pia ametuthibitishia ukweli wa ile barua yake..hicho mnachokiita kirusi ni mtoa habari anayewapenda watanzania na hapendi mauaji na mateso ya waandishi na wanaharakati
 
Last edited by a moderator:
chadema bwana.slaa kaita waandishi wa habar ktk siku za mwanzo,mbowe katoa tamko,lisu kila siku ndio kazi yake,makene jana,zitto jana na leo kuhusu rwakatale swali.kama hamkuhusika presha zote hizi za nn .hapa kuna jambo limejificha
 
Mtatapatapa sana mwaka huu mwishowe "kusney!!!"chezea chama dola nyinyi?.
 
Bila shaka hujui kusoma yani umeshindwa kuelewa kuwa zitto kaikana hile barua japo amaesema kuna maudhui yana fanana na barua alio andika?

Hii barua ni ya kwenu na mmeonesha msivyojua qulity za barua!

Acha kujifanya juha bana, sasa hapa Zitto amekuja kuimba bongo flava.
 
Nyie chekeni na watu wanaotoa barua za chama nje ya chama,huyo mtu aliyeitoa barua hiyo na kuiweka JF sio mtu wa kucheka nae kabisa,kwa maana hiyo anaelewa nini kinaendelea ndani ya chadema na ipo siku atafanya lolote lile baya juu ya chama chenu,ni wakati sasa wa kupambana na hivyo vimelea la sivyo itakuwa ni story ya kumpa nyani alinde mahindi yako
kuna kirusi ndani ya chadema,ni lazima dawa itafutwe kukiangamiza
 
imefika wakati chadema inatakiwa iangalie outside the box na isiwe inakurupuka kwa kutmuia ushabiki na moyo tu

Kwa heshima na taadhima NDIYO MAANA CHADEMA NI CHADEMA NA CCM NI CCM. Unanichefua kwa kauli za kishenzi kama "isiwe inakurupuka kwa kutmuia ushabiki na moyo tu" Wewe ni nani kuhumu watu kwa maneno kama haya. Tunazungumzia hoja ya zito upuuzi wa kukurupuka unatoka wapi?

Mbaya zaidi unaamua kuwa "imimefika wakati" basi na iwe hivyo umefika wakati wa Chadema kusimamia wanachokiamini.
 
wanasubiri upepo uende vipi lol

sasa kama Zitto hana uhakika na ukweli wa video ya Rwakatare
hadi aombe uchunguzi
why tena aseme haamini kuna watu wanataka muua?
what if uchunguzi ukisema video ni kweli?

Kwani kwenye hiyo video wanazungumzia mauaji??
Na wanapanga kumuua Zitto??
Acha kuchanganya mambo....kama hujui kitu cheza karata....
 
chadema bwana.slaa kaita waandishi wa habar ktk siku za mwanzo,mbowe katoa tamko,lisu kila siku ndio kazi yake,makene jana,zitto jana na leo kuhusu rwakatale swali.kama hamkuhusika presha zote hizi za nn .hapa kuna jambo limejificha

Mbona na wewe hubanduki humu presha yako nini?
 
Tafadhali weka kumbukumbu zako sahihi juzi tuu hapa katajwa Mwakyembe kutaka kutumia TPA kufanya biashara na CCM sukita, Nape katoa waraka unadhani si kusimama na kiongozi wao huko.

Kikwete aliambiwa ameanzisha udini na kwamba anendekeza ugaidi wa kidini, Nape huyo amesimama mara ngapi kumgombea mwenyekiti wake.

Kinana Meli zake zimeonyesha kuwa zinasafirisha meno ya tembo yaliyopatikana kwa njia ya ugaidi na ujangiri, Mpaka makamu mwenyekiti wa CCM amesimama kutetea japo vyote hivyo ni kweli lakini bado wametetea na kujaribu kutunga uongo kuwaokoa watu wao ,kwa hiyo weka rekodi zako sawa

Kwa hiyo CDM imeona ni sawa ianze kutumia mbinu za CCM kwa kujitetea instead of kutegemea mahakama? As chama cha demokrasia lazima wa-walk the talk na waheshim mahakama. Au mkuu sijui unaonaje? maybe sijakuelewa
 
:rockon:Nenda tena shule! Hapo kwenye RED aliyekwambia kwamba muhalifu hatetewi na nani? na eti mtakiweka katika hali gani chama?. kwani nyie chama chenu mkiweka kwenye hali gali mbona kina waalifu wa kumwaga na bado kinatawala na kuendelea kuclaim kuwa bado kitaendelea kutawala milele.

Mkuu sikulaumu kwa sababu najua unaongea kwa hisia kwa hiyo nitakujibu kipole pole. Mtuhumiwa yoyote ana haki ya legal representation unanielewa hapo? Chama hakitakiwi kuonekana kuside na upande wowote. Walicho takiwa kufanya ni kusema tunamsupport mwanachama wetu mpaka hukumu itakapo tolea. Ila haya matamka ya kudai kuwa na uhakika wa mtu kuwa "innocent au guilty" inaweza ikacost chama. Naomba usome academica articles on public relations/spin etc.

Kuhusu mimi kwenda shule tena mkuu hilo wala siwezi kubishana na wewe. Kwa maana wewe hujui kisomo changu na wala mimi sijui kisomo chako na hiyo elimu ulionayo wewe kama ilelisaidia taifa kwa lolote.
 
Hivi ben saanane ( cobra ) si ndio anatabia ya kurekodi watu ? Yeye ndio atakuwa amefanya hii kazi kwa kutumia ile saa yake ya ajabu .Atakuwa ni kirusi kibaya sana ndani ya chama .

Fitina, fitina hadi mfumaniwe. Unataka kusema hata Ben ni mtu wenu? Poa lakini huyo huyo atawachojoa mbaki uchi
 
mbona mnasema film iliwekwa na ludo. hicho kirus au virus ni uongozi mzima hapo juu hamko pamoja.japo zitto ni kijana wa nyumbani kigoma nawasiwasi na zitto waha hatuko hivyo. yaani umeweza kujua walioficha pesa uswizi umeshindwa mambo ya ndani cdm

Mbona unachachawa....Zitto ni mwanasiasa makini hawezi kuishi katika assumption kama wewe na ku-publicize kile ulichochagua kuona.....whether kipo au hakipo!
 
Utaifakwanza, Zemakopo(wazee wa kulipwa) siwaoni kwenye hii au inakuwaje hapa. Hamna mmojawapo aliyeweka hii barua hapa???
 
Roulette,

Mimi nitakuambia kwa nini kwa sasa Chadema wana deny authenticity ya hiyo video. Ukweli ni kwamba kama video itagundulika kuwa authentic na vyombo husika basi itakua ni big blow kwa Chadema especially wakati huu wa kuelekea 2015 na nitaeleza kwa nini.


Lwakatare ni mkurugenzi wa Usalama wa Chadema pia ni kiongozi mwandamizi. Watajielezaje kwamba mkurugenzi wao wa usalama alikua ana panga njama ya kuteka? Swali la pili ni kwamba kama kweli video ni authentic basi itabidi wajiulize Lwakatare alipanga hizo njama kwa niaba ya nani (chama au baadi ya viongozi wa chama)? Ana mgogoro gani binafsi na huyo aliepanga kumteka? Kama hamna mgogoro binafsi ina maana ana fanya hiyo kazi kwa niamba ya fulani au watu fulani je ni wakina nani?

Mimi ningekua mshauri wa Chadema ningewashauri yafuatayo:
1. Acheni kudai video siyo authentic mpaka pale hilo litakapo sibitishwa maana laa sivyo mtaonekana mnaedeshwa na hisia na siyo logic.

2. Tundu Lisu asingekua msemaji kwenye kesi hii. Lwakatare ana timu ya wanasheria kadhaa, mwanasheria yoyote angetakiwa kuwa spokesperson kwa maana Lisu ni mwanasiasa ukiacha kwamba ni mwanasheria. Je Lwakatare akigundulika na hatia chama mtakiweka katika hali gani kama mlikua mnamtetea mhalifu?

3. Waache kupoliticize hii ishu maana kwa sasa hali ilivyo ni win-lose situation kwao. Kama kesi ikienda ndivyo sivyo itareflect vibaya kwa chama.

Hata kama video ni ya kweli (kitu ambacho naamini mimi) bado huwezi kufanya conclusion kuwa Rwakatare alikuwa anapanga kuteka. Ni lazima ujue kwa upana, uefu na kina kuhusu yale mazungumzo yaliyorekodiwa. Mtu anaweza kukuuliza maswali ya mtego na akakurikodi ikawa kabisa kama ulikuwa unapanga mpango fulani kumbe sivyo.

Tufanye wewe mwanajeshi na rafiki yangu kabisa, tunaaminiana na na tanapenda kupiga soga pamoja, naweza kuja na swali la mtego kama hili kwako:

''Wewe MwanaFalsafa1 si unajifanya unajua mbinu za medani? Hebu tujifanye leo hii, mimi ni tajiri mmoja mfanya magendo na katili sana, nataka kukukodisha ukamuue askari polisi mmoja mnoko anayezuia biashara zangu, utatumia mbinu gani? Nielezee, ikiwezekana uandike kila hatua kwenye hili daftari hapa mezani''.

Wakati unaanza kueleza nikikurekodi halafu nikaifanyia ile video editing mbona utaonekana kama kweli ulikuwa unapanga njama?
 
Gud move zk...ur a leader with stable facts..i usually take care in my life with double agents and now u prove me right..JACK BAUER did what he thout waz right..u a also doing it.congrats
 
Mbona unachachawa....Zitto ni mwanasiasa makini hawezi kuishi katika assumption kama wewe na ku-publicize kile ulichochagua kuona.....whether kipo au hakipo!

mbona anabwabwaja tu et id mbili za aliye post
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom