Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Mkuu mimi nina
maswali kadhaa. Umeandika kwamba uliandika barua kwa katibu mkuu wa
chama kukisihi chama kifanye uchunguzi wa ndani kuhusu swala la
Lwakatare. Je:

1. Ombi la kufanya uchunguzi ulikubaliwa?

2. Kama Ombi la uchunguzi lilikubaliwa je uchunguzi wa ndani
umethibitisha nini?

3. Inaelekea unaamini kabisa kuwa kuna ki/virusi (spies) ndani ya chama.
Je mmefanya uchunguzi wa kuwagundua ni wakina nani?

Kukurupuka ni kubaya sana, maswali yako umekurupuka. Mf. swali la 3, Zitto kasema kwa kuitoa ile barua hapa jf amegundua kuna kirusi, leo hii wewe unaulisa swali la 3, sasa huo uchunguzi umefanyika lini? Acha KUKURUPUKA.
 
Naamini na ntaendelea kuamini kuwa aliye post ile video Zitto anamfahamu na naamini pia yeye ndo aliye mpa hii barua aje kuipost hapa.
 
Mungu anisamehe bure, sijui ni kwa nini Nawachukia wewe na Pasco Mayala, am so sorry, mna rangi nyingi zaidi ya kinyonga.

I hate this person like hell

PINDA-MAYALA
 
Hata kama video ni ya kweli (kitu ambacho naamini mimi) bado huwezi kufanya conclusion kuwa Rwakatare alikuwa anapanga kuteka. Ni lazima ujue kwa upana, uefu na kina kuhusu yale mazungumzo yaliyorekodiwa. Mtu anaweza kukuuliza maswali ya mtego na akakurikodi ikawa kabisa kama ulikuwa unapanga mpango fulani kumbe sivyo.

Tufanye wewe mwanajeshi na rafiki yangu kabisa, tunaaminiana na na tanapenda kupiga soga pamoja, naweza kuja na swali la mtego kama hili kwako:

''Wewe MwanaFalsafa1 si unajifanya unajua mbinu za medani? Hebu tujifanye leo hii, mimi ni tajiri mmoja mfanya magendo na katili sana, nataka kukukodisha ukamuue askari polisi mmoja mnoko anayezuia biashara zangu, utatumia mbinu gani? Nielezee, ikiwezekana uandike kila hatua kwenye hili daftari hapa mezani''.

Wakati unaanza kueleza nikikurekodi halafu nikaifanyia ile video editing mbona utaonekana kama kweli ulikuwa unapanga njama?

Ndiyo maana nikasema mkuu uchunguzi uta thibitisha yote.
 
Mh Zitto
Chadema have failed to practice what they preach,
Huwezi kuwashinikiza wengine wajiuzuru kupisha uchunguzi wakati yakitokea kwenu mnawakingia kifua bila kufanya uchunguzi kwanza.
 
Mungu anisamehe bure, sijui ni kwa nini Nawachukia wewe na Pasco Mayala, am so sorry, mna rangi nyingi zaidi ya kinyonga.

Bora useme ukweli wako watu vibahasha vya kaki vimewavua utu
 
Yaani ukiangalia hii sinema unapata wasiwasi na viongozi wanaoaminiwa na watu. Hapa nazungumzia wote. Hebu wajifunze kuwa viongozi wenye maadili. Kama kuna suala linasumbua chama kaeni kwenye vikao vyenu mtafute ufumbuzi. Kuja kutafuta ufumbuzi kupitia JF kwa kweli siyo sahihi. Pamoja na kuwa nyie ni wanasiasa lakini mtambue pia ninyi ni mameneja kwa hicho Chama.

Ni hayo tu kwangu yaani wana JF hizo sarakasi za hawa jamaa zinanikera, wanatakiwa kuwa mature sasa.

mkuu pamoja sana ila nawe usimungunye maneno, Zitto need to play as a team. Yeye anamjua alieleta hio barua. asitufanye kuwa hatunazo. Yani alishindwa kukaaa na Slaa wakajadiliana mpaka barua? email si wanazo? is that too formal? wenye akili wote tunajua jinsi gani Zitto asivyoshirikiana na wenzake.
 
Hapa hakuna ukweli kabisa na kama unaweza thibitisha! Na ingekuwa ana wajua wala asinge sema kama alivyosema!

Naamini na ntaendelea kuamini kuwa aliye post ile video Zitto anamfahamu na naamini pia yeye ndo aliye mpa hii barua aje kuipost hapa.
 
Je uchunguzi wako wa ku identify id za kirusi hiko haujakutajia id zingine za kirusi hiko hap JF au email zake?

Mh Zitto
Chadema have failed to practice what they preach,
Huwezi kuwashinikiza wengine wajiuzuru kupisha uchunguzi wakati yakitokea kwenu mnawakingia kifua bila kufanya uchunguzi kwanza.

Mzee wa magamba ccm wameweza kupractise MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?
 
naipenda chadema hata kwa mabaya yake thanks zito nipe id hiyo ni trace that people
 
Binafsi naamini kabisa kua the video is authentic and I am surprised that CDM efforts are focusing on blaming the recorder and not the recorded. Ni sawa na mtu akamatwe na CCTV then defense yake iblame the CCTV for recording the crime (maana kupanga walichokua wanapanga is a crime already).
But what I wanted to say in that post ni kua viongozi wa CDM hawawezi kusema sasa hivi kua video ni authentic or not as that is part of what the court has to pronounce. Issuing a final statement on the authenticity of the video now would be a contempt of the court ("Kesi iko mahakamani, hairuhusiwi kujadiliwa" type of argument).

Mko wengi sana kwa sababu zenu nzuri mnauelewa unaowafaa nyinyi kwa hali ilivyo. Uelewa ni majaliwa ya mwenyezi Mungu. Na mimi binafsi naishukuru sana JF kwa fursa ya sisi wote kuweka mawazo yetu hapa.

Kitu cha kusikikitisha ni jitihada za kutaka mtu anavyoelewa na wengine waelewi hivyo hivyo. Kama vile mwenyezi Mungu alivoficha wanadamu fikra zao za kweli zisibainike hadharani zikaonekana na kila mtu. Hapa kuna wanaotumia hulka hiyo kuchokonoa na kuchota mawazo ya wengine KWA NIA NA MATUMIZI MABAYA kiasi cha kujiuliza fursa yote ya JF ni mchezo usio na mwelekeo yaani Komede Orijino. Hii haitushangazi baadhi yetu kulingana na uhalisia wa "survival".

Kwa watu wazima wanajua kabisa kama unajaliwa hekima tu na Mwenyezi Mungu kuelewa kuwa kuna binadamu simba, wengine fisi, popo, nyoka na malaika wamo humo humo kati ya wanadamu.

Kwa nijuavyo mimi na watu wengine wengi, hili sakata ni mchezo wa kitoto unaochezwa na CCM kwa lengo la kutaka wafe na mtu maana hatima yao wameibaini. Ila kuna msemo cheza na nyoka mkiani usije ukamkunja ukaona uso wake wakati unatafuta miguu yake. Kwa bahati nzuri mchezo upo kwenye hadhara lazima kuna atayekosea na kumtafuta nyoka miguu
 
Nimemaliza kazi ilio nipeleka kua moderator, na sasa naenddelea na kazi zingine. So yes, tunaweza kusema kwa JF nimestaafu.
To me kuwa Moderator naona kunakubana kushiriki mijadala kwa uhuru, huoni sasa utamu wake unavyojimwaga jukwaa la siasa? maana mwanzoni ulikuwa unaishia MMU tu.
 
Mh Zitto
Chadema have failed to practice what they preach,
Huwezi kuwashinikiza wengine wajiuzuru kupisha uchunguzi wakati yakitokea kwenu mnawakingia kifua bila kufanya uchunguzi kwanza.

Ungekuwa na chembe ya hekima ungeizungumzia CCM na mafanikio yenu ya kuweka virusi. Kwani wewe ulijiuzuru au ulifukuzwa? Ndiyo maana Dr. Alex Paurine amefanikiwa kutushawishi una magonjwa yanayohitaji immediate attension.
 
Mh Zitto
Chadema have failed to practice what they preach,
Huwezi kuwashinikiza wengine wajiuzuru kupisha uchunguzi wakati yakitokea kwenu mnawakingia kifua bila kufanya uchunguzi kwanza.
Umeshamaliza dose? pls Dr Pauline hebu njoo umchukuwe huyu mgonjwa wako Chris Mkosi.
 
Umeongea vizuri sana na kwa ushupavu mkubwa bila kujikanyaga...inaonesha dhahiri kuwa hukuwa na nia ovu katika barua yako...hongera sana kiongozi wetu na Mungu utuzidishie mshikamano zaidi na atulinde dhidi ya adui zetu ili wakija kwa pamoja tuwatawanye katika njia 7 tofautitofauti...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom