Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Huyu kijana ben wa saa nane ni wakuangalia mara mbili. Huenda ule u-PM7 unaendelezwa kwa utaalamu wa hali ya juu.
 
Usijaribu kutoa tafsiri yako na kuifanya ni ya zitto!

Kwa hiyo Mh. Zitto, unataka kusema hata ile video ilianzia CHADEMA ndo ikaenda mtandaoni kama ilivyotokea kwenye barua yako? Kwa kifupi, namaanisha kuwa hiyo video ya Lwaka ni REAL plot ya CDM?
 
ndugu yangu. Dhana ya kusema kuwa ccm imeingiza kirusi chadema hutumiwa na akina slaa na mbowe ili kuficha maovu yao na kuwakandamiza wanaoenda kinyume na misimamo yao

Mbona jina lako linatisha? Hata hivyo nilivyo ukinitajia jina la mtu kuwa ndiyo hoja badala ya hoja inayohusu suala la kijamii huwa natilia shaka. Kama kuna maovu vyombo vya sheria vinashindwaje kuchukua hatua? Ukweli ukuweke huru
 
Mimi nimependa tu onyo la mwenyekiti kuwa kama Lwakatare ameshiriki mpango huu kwa kujua au kwa kudanganywa au kwa kuingizwa mkenge au kizembe lazima awajibike,...hapo ndio pa kuanzia Hatuwezi kuwa na mkurugenzi wa usalama asiye makini na kazi zake!!Bravo Mbowe!
 
mara zote nimeamini kuwa bila chadema imara, ccm itakuwa kama simba aliyekabidhiwa bustani yenye swala! Itafuja kila kilicho mbele. Chadema ikiwa imara, tanzania itakuwa imara.

ni kweli ndugu,manyerere chadema ikiyumba tanzania itayumba ni muhimu viongozi wa cdm kujizatiti na mipango yote inayopangwa na mafisadi hawa ccm,watanzania wote wapenda haki tupo nyuma yenu,,,msiogope,,,,tutashinda,
 
namalizia kwa msemo wa kiswahili kuwa NUNGUNUNGU HAKUMBATIWI

Nashukuru kukuelewa kuwa ni mchochezi mchonganishi mtu si riziki, unavyoandika utadhani masalia TUNTEMEKE. Ila umenikifu kwa kuegemea hoja uutu kuliko maswala ya maana. Chadema si Zitto au Dr. Slaa. Imekuwaje ubwabwaje na mipango ambayo unaijua halafu unangoja Zitto aandike hapa JF ndipo ushadidie? Kirusi wewe
 
Zitto unanipa wasi wasi sana kwa haya maelezo. Ofcoz maelezo yanaonekana yana lengo la kukisafisha chama dhizi ya propaganda kwamba viongozi hamuelewani lakini, kwa nini haukusema tu barua iliyowekwa hapa haujaiandika wewe yaishe??? Matokeo yake anaanza kumtangazia mtu unaemhisi kuwa mwizi kwamba unajua alipo na unahamasisha wenzio mumkamate. Hili tangazo lako la kukamata mwizi kwa kweli linanipa wasiwasi kama kweli unayo nia ya kuondoa wasaliti kwenye chama. Ingetosha sana kusema barua haujaiandika wewe na haya mengine ya content kufanana ungeenga kujadili ya viongozi wenzako mbaini nani tatizo mumshughulikie. Zitto tangu lilivopita zogo la buzwagi umekuwa unpredictable sana. No wonder umewahi kuwa role model wangu kama mwanasiasa kijana na ofcoz new likuwa nakukubali mpaka chuoni kipindi hicho nikabatizwa jina lako. Zitto uwezo unao na natamani kumuona zitto wa mika ya 2005 kaka. Kila la.kheri
 
mkuu zitto , Asante kwa maelezo Mazuri . Vp kuhusu ludovick ? Mmemtosa au naye bado mpo naye katika kipindi hiki kigumu kinachomkabili ?

NGOZI YA KITIMOTO HAIWAMBWI NGOMA....tafakari!
 
Mohamedi Mtoi na wapiga debe wa chama wengine, sasa baada ya Zitto kukubali kuwa ile barua ni yake mnajisikiaje? Kiherehere muache siku nyingine msubiri mhusika akanushe sio ninyi wapambe.
 
Last edited by a moderator:
Siasa za hapa Tanzania ni zaidi ya siasa za nchi nyingine, hii mikakati ya CCM kuendelea kubaki madarakani japo hawapendwi na wananchi wanajifunzia nchi gani jamani.

Ama kweli hadi ifikapo 2015 kwa watakao kuwepo hai watapata kuyaona na kuyashudia mengi.
 
Leo,Ndugu Zitto Zuberi Kabwe,Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kikuu cha siasa nchini ameweka bandiko humu jamvini akielezea barua yake aliyoiandika kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA,Dr. Wilbrod Peter Slaa kuhusiana na sakata la Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA,Alfred Muganyizi Lwakatare anayekabiliwa na kesi ya ugaidi. Pamoja na Zitto kukiri kuandika barua hiyo,bandiko lake linaibua maswali. Kwanza,Ndugu Zitto amedai kuwa amefanya uchunguzi na kugundua kuwa aliyeweka video ya Lwakatare 'youtube' na aliyeweka barua yake hapa JF,ingawa zimetumika ID tofauti,ni mtu mmoja. Nini kilichomwonesha kuwa hugochavez-wa video ya Lwakatare na @formfourliver2012 aliyeweka barua yake kwa Dr.Slaa ni mtu mmoja? Kwa uchunguzi wake,ni kweli barua yake hakuipata kwake(kwa Zitto) ila Ofisi kuu za chama alikoielekeza? Anataka kusema nini hapa...kwamba Ofisi kuu ina uzembe unaopelekea kuvuja kwa nyaraka za kiofisi? Pili, Zitto anadai kuwa aliyeweka video ya Lwakatare na barua yake ni kirusi kilichopo hapo hapo CHADEMA. Tena Zitto akaongeza kuwa ni mtu mwandamizi chamani au aliyekaribu na vioongozi waandamizi chamani. Yeye anahisi ni nani? Anamaanisha kuwa video ya Lwakatare ilitengenezwa sirini na chama lakini ikavujishwa na hugochavez? This is the most sensitive part of Zitto's thread. Video ya Lwakatare inapingwa vikali kuwa si halali. Sasa kitu kisicho halali kimevujishwaje? Anaamini kuwa video ile imetengenezwa na CHADEMA kweli? Please Z
 
Mkuu kwani CDM hamruhusiwi ku-quote kutoka kitabu chako? Kwa nini uwe mtumwa wa imani za wenzako kisa chama? unafikiri enge-quote Quran usingeeleweka...
Zitto,

Kwa kweli hapo ndipo unapoonyesha umakini ktk siasa. MWAKA JANA niliwahi kukushauri ndugu yangu kuwa WW huna sababu ya kupambana na mtu yeyote ndani ya chama chako muda UTAFIKA na hapo mambo yote yatakuwa mteremko kwako na kwa nchi yetu.

Nukuu bible "JINYENYEKEZE CHINI YA MKONO WA BWANA ULIOHODARI NA YEYE AYEKUNYANYUA KWA WAKATI WAKE" hila hizi za sasa ni hatari sana tena sana ila tutashinda.
 
Mohamedi Mtoi na wapiga debe wa chama wengine, sasa baada ya Zitto kukubali kuwa ile barua ni yake mnajisikiaje? Kiherehere muache siku nyingine msubiri mhusika akanushe sio ninyi wapambe.

Utamuona sasa hivi anakuja na meneno ya twaarabu.
 
Last edited by a moderator:
Usijaribu kutoa tafsiri yako na kuifanya ni ya zitto!

Unafikri Zitto hakuwa na nafasi ya kulalamika kwenye Chama kuhusu barua yake iliyo LEAK ambayo hakutaka iwe public? Badala yake naye ameamua kwenda PUBLIC bila kujua adhari za maneno yake. Kusema mtu aliyeweka hiyo video ndo yuleyule ameweka na barua yake, anataka kumaanisha kuwa mtu huyo YUKO CHADEMA. Kwa hiyo,.....!
 
Hongera sana Kabwe kwa busara na umakini wako. Hakika unafanya critical analysis ya swala hili. Nakuunga mkono kwa yote uliyoyasema kwenye barua pamoja na huu ufafanuzi ulioutoa. Hakika watu wa karibu sana, tena waliopewa majukumu makubwa na chamma kwa kuaminiwa kwao ndio wanaotumiwa na mabamba kukihujumu chama. Kauli zao hizo za kusema CHADEMA itakufa kabla ya 2015 mikakati yake ndo hii inayojitokeza. Binafsi nahisi Lwakatare pia ametumiwa na hawa jamaa. Kwa nini akubali kurekodiwa? Haiingii akilinikabisa.
 
ndugu yangu. Dhana ya kusema kuwa ccm imeingiza kirusi chadema hutumiwa na akina slaa na mbowe ili kuficha maovu yao na kuwakandamiza wanaoenda kinyume na misimamo yao

muvi yote inajulikana na mastalingi ni,,,,,,,,,,,,,,,,na,,,ccm huo ndio hukweli,,,,,kifupi ninyi mnangojea kaburi 2015 siasa za unajim watanzania wamesha amka sasa wanajua blue ni blue nasi njano ndio mnazidi kujikaanga wenyewe,badala ya kutatua shida za watanzania ninyi mnapanga mipango ya kuiua chadema,mnafikiri mkiiua chadema ndio mtasalimika mbele ya watanzania waliopigwa kimaisha na ufisadi wenu,,,,,mnajidanganya sana kwa kweli hamtoki habari yenu kwisha,,,,,
 
Ndugu Zitto anaelekea kumaanisha kwamba kuna mtu ambaye Dr Slaa amempatia nakala ya barua yake,mtu huyo akaifanyia mabadiliko kidogo tu,kisha akaibandika hapa.

Huyo mtu AKA kirusi,ndo anayelalamikiwa na dugu Zitto,so ndo huyo form four leaver2012...

Zitto anasema alindika hiyo barua directly kwa Dr Slaa(barua isiyo public),so labda aliyemtuma ndo kalikisha,ama aliyepewa(Dr Slaa),ndiyo kafanya hivyo...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom