Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
..well said Zitto.

Nina ushauri muhimu sana sana kwako....kama ambavyo nimekua nikifanya nionapo mambo si mazuri CDM...Katika kufuatilia hali ya mambo CDM(kupitia post zenu humu JF)..nimegundua kuwa wewe mh.Zitto pamoja na mtu anayejiita Ben Saanane hamna uhusiano mzuri....kwa maana ya kutoleana shutuma humu...haswa Ben Saanane.

Pale ambako amekua akikuhusisha wewe na masalia waliotemwa CDM....huku akisahau kuwa naye alikua kundi hili la masalia lakini hakufukuzwa (kama wenzake)...

Inakua inaniuma sana napoona Ben anakuja kukutuhumu humu JF wewe mara kwa mara....wakati alitakiwa akutafte na mkae mmalize tofauti zenu...jambo ambalo mi naona ni jema kwa maslahi ya chama chenu.....

Nasema hivi kwa kuwa mtu aliyetuma maneno ya barua yako humu ni mtu aliye ndani ya CDM...na ni mtu asiyekutakia wewe mema ndani ya CDM....Kwa hiyo ninakushauri fanya hima mtafutane na Ben (kwa uzuri tu)na kwa manufaa ya chama...tafuteni reconciliation...malizeni tofauti zenu ili mkijenge chama...

Mimi binafsi nina imani sana nawe kama kiongozi mahiri wa CDM...na sipendi nione unachafuliwa.....kama ambavyo sipendi nione Dr.Slaa au Mh.Mbowe wakichafuliwa humu JF....

Nakushauri sana..kama bado hamjamaliza tofauti zenu na Ben.....malizeni....kwa manufaa ya CDM....Najua umewahi kusema humjui Ben Saanane...basi ni vizuri umtafute...kupitia wanaomjua...ili mumalize tofauti zenu....huwa nashindwa kuelewa lengo haswa la Ben kutoa shutma kwako humu JF...na kwa maana hiyo mtu wa kwanza kwa wewe kumjua ni huyu....
 
sina imani na Zitto,kwanini adhani barua yake imevuja kutokea ndani ya chadema na si kutoka kwa watu wa karibu yake? Kirusi anachokizingumzia anataka watu warudi nyuma kwa kiboko wa masalia na kumdhania ndiye wakati my sense inasema siye.ni mtazamo wangu tu .
 
mkuu pamoja sana ila nawe usimungunye maneno, Zitto need to play as a team. Yeye anamjua alieleta hio barua. asitufanye kuwa hatunazo. Yani alishindwa kukaaa na Slaa wakajadiliana mpaka barua? email si wanazo? is that too formal? wenye akili wote tunajua jinsi gani Zitto asivyoshirikiana na wenzake.

Selous,
Hapa simung'unyi maneno nilikuwa naangalia hili suala kwa mapana zaidi. Kwa mfano inawezekana Zitto ndiyo tatizo. Sasa kama Zitto ni tatizo wakubwa zake wa CDM wamemchukulia hatua gani? Wanamuogopea nini? Kama wanamuogopa Zitto sasa hivi, je wakichukua nchi akawa Waziri wa Fedha hawezi kufanya kama vile Gordon Brown alivyokuwa anamfanyia Tony Blair? Hiyo ni kwa upande mmoja. Upande mwingine ni Zitto kama anaona viongozi wa CDM hawatoi ushirikiano kwa asijaribu kutafuta huo ushirikiano na akiona hakuna kwa nini aendelee kuwa huko na aonekane kama msaliti, kwa sababu kama watu hawakutaki wewe unaendelea kuwa huko kwa ajili ya nini? Hayo ndiyo maswali niliyokuwa najiuliza
 
4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. ‘Coincidence’ ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa
Kwa hiyo Mh. Zitto, unataka kusema hata ile video ilianzia CHADEMA ndo ikaenda mtandaoni kama ilivyotokea kwenye barua yako? Kwa kifupi, namaanisha kuwa hiyo video ya Lwaka ni REAL plot ya CDM?
 
Mara zote nimeamini kuwa BILA CHADEMA imara, CCM itakuwa kama simba aliyekabidhiwa bustani yenye swala! Itafuja kila kilicho mbele. Chadema ikiwa imara, Tanzania itakuwa imara.

Na agenda kuu ya CCM ni kulinda bustani za watu binafsi. Hawana maono ya kuhakikisha Watanzania kwa ujumla wanahitaji bustani ili iwafae katika maisha yao.
 
Mshahara wa dhambi mara zote ni mauti,kwa hiyo hao wasaliti na CCM yao wasubiri haki yao 2015.
 
mkuu pamoja sana ila nawe usimungunye maneno, Zitto need to play as a team. Yeye anamjua alieleta hio barua. asitufanye kuwa hatunazo. Yani alishindwa kukaaa na Slaa wakajadiliana mpaka barua? email si wanazo? is that too formal? wenye akili wote tunajua jinsi gani Zitto asivyoshirikiana na wenzake.

Ashirikiane nao kwenye nini wakati wanamuwinda wamuue?
 
..well said Zitto. Nina ushauri muhimu sana sana kwako....kama ambavyo nimekua nikifanya nionapo mambo si mazuri CDM...Katika kufuatilia hali ya mambo CDM(kupitia post zenu humu JF)..nimegundua kuwa wewe mh.Zitto pamoja na mtu anayejiita Ben Saanane hamna uhusiano mzuri....kwa maana ya kutoleana shutuma humu...haswa Ben Saanane.Pale ambako amekua akikuhusisha wewe na masalia waliotemwa CDM....huku akisahau kuwa naye alikua kundi hili la masalia lakini hakufukuzwa (kama wenzake)...Inakua inaniuma sana napoona Ben anakuja kukutuhumu humu JF wewe mara kwa mara....wakati alitakiwa akutafte na mkae mmalize tofauti zenu...jambo ambalo mi naona ni jema kwa maslahi ya chama chenu.....Nasema hivi kwa kuwa mtu aliyetuma maneno ya barua yako humu ni mtu aliye ndani ya CDM...na ni mtu asiyekutakia wewe mema ndani ya CDM....Kwa hiyo ninakushauri fanya hima mtafutane na Ben (kwa uzuri tu)na kwa manufaa ya chama...tafuteni reconciliation...malizeni tofauti zenu ili mkijenge chama...Mimi binafsi nina imani sana nawe kama kiongozi mahiri wa CDM...na sipendi nione unachafuliwa.....kama ambavyo sipendi nione Dr.Slaa au Mh.Mbowe wakichafuliwa humu JF....Nakushauri sana..kama bado hamjamaliza tofauti zenu na Ben.....malizeni....kwa manufaa ya CDM....Najua umewahi kusema humjui Ben Saanane...basi ni vizuri umtafute...kupitia wanaomjua...ili mumalize tofauti zenu....huwa nashindwa kuelewa lengo haswa la Ben kutoa shutma kwako humu JF...na kwa maana hiyo mtu wa kwanza kwa wewe kumjua ni huyu....
...huyu Ben simuamini kabisa...kaeni macho viongozi wa CHADEMA huenda kuna mtu amekuja CDM kwa lengo la maangamizi kisha akishamaliza atimue zake...
 
Dawa ya maradhi ni kuyasimulia!!. Hivyo CDM endeleeni kutoa taarifa za wazi kwa kila kile kinachojiri bila kujali ukubwa wala sharubu za ofisi au mhusika na hiyo ndio dawa pekee ya wale wenye mambo yao ya chinichini.
Pia ongezeni juhudi za kuwafikia watanzania wengi iwezekanavyo kwani wananchi wakishajua ukweli hata kama watakamata vinara wa CDM wakawaweka vizurizini halafu wananchi wakawekewa picha siku ya uchaguzi wataichagua. Mfano mzuri tizama hila hizi http://www.mwananchi.co.tz/habari/Siasa/-/1597332/1740870/-/b6xb6cz/-/index.html na hatima yake.
 
Safari bado ndefu sana! Bila shaka hili la kirusi ndio tatizo kubwa kwa CDM kwa sasa! Vijana wasio na ajira wanajifanya wanauchungu na hii nchi kumbe njaa tu! Wakipewa laki nne wapo tayari kufanya lolote!
 
Zitto Kabwe, sasa ni dhahiri umekomaa kisiasa. Hongera sana na maelezo haya. Hawa wenye mbini chafu waache tu, mwisho wa ubaya wao ni aibu kwao.
 
Asante Mheshimiwa Zitto. Naweza kusema kwa ujasiri kabisa kuwa mpaka sasa ndani ya CHADEMA hakuna kiongozi mwingine aliyeonesha ukomavu wa kiwango cha Zitto. Anajiamini na ana msimamo wa kujenga, anaweka maslahi ya chama chake mbele kabisa kabla ya maslahi mengine yoyote. Anaheshimu na kusimama kwenye maelekezo ya chama chake yanayotokana na vikao vyao wenyewe, na siyo kwenye majungu. Nampongeza na kumtakia heri, aendelee kusimamia principle hiyo, tutafika tu.
 
Hapana! ninachosema ni hawa viongozi kutozungumza hata kwenye simu,bar,kahawa nk kushare mambo fulani mapya tena kwa kucheka,kutaniana,kujadili namna na mipango kama hiyo.mfano wewe uko kwenye familia ukiona jambo fulani linalogusa familia unaweza kumjulisha mwenza juu ya jambo na kusudio lako la kuchukua hatua ya awali licha ya kuwa kila mmoa ana uwezo na maoni yake!.

hawa viongozi wako hivyo? au wanakutana kwenye vikao na kuandikiana barua? basi kama ndivyo kuna tatizo kubwa!

Uongozi ni wajibu na ukisha kuwa kiongozi suala la 'haya ni maoni yangu' kwa kiasi kikubwa upungua sana na hakina unanyoweza kujitetea.

zito ni naibu katibu mkuu,coments zake kama hizi haziwezi kukijenga chama chao,bali kuwavuruka tu.

kila mtu anasema lolote,issue eti ni maoni yake?

Mkuu nimekupata vizuri sana.Huwa napata wakati mgumu sana na kijana huyu "Zitto"nimejaribu kuangalia ushauri wake kwa chama ni mzuri mno.Nilikua najiuliza kwa nini aandike barua, wakati hii ni serious issue ambayo angeweza kukaa kitako na katibu wake mkuu na wakaijadili kwa kina kwani ni suala linalohitaji muda wa kutosha?Lakini jambo la pili, je haiwezekani kwamba yeye aliandika hii barua huku akijua italeak then atoe maoni yake na kuonekana yuko vizuri?Kwenye hili napata picha Zitto kuna kitu anakijua hivyo amejiandalia mazingira ya kuja kuonekana ni Mr. clea.Nimejaribu kuangalia tena kirusi anachokizungumzia ,nikapata picha pengine inaweza kuwa hicho kirusi, ndicho kinachotafutwa CDM kwani ,inawezekana kuwa ndio Kikwazo kwa Zitto na kundi lake kutekeleza malengo yao.najaribu pia, kuangalia urafiki wa Zitto na Msacky, pia uhusiano wa Zitto na baadhi ya mafisadi,nahitaji kumjua Zitto vizuri.

Ila yote katika yote,nawapongeza walioratibu mpango mzima wa kuisambaratisha CDM,umepangwa kwa Ustadi wa hali ya juu sana.Ndio maana haikuwawia vigumu CCM kuanza kuzungumza kwenye Press kuwa CDM itasambatratika.Hapa ndipo nataka kuona umahili wa Viongozi wa CDM, wakilivuka hili nina imani CDM itakua imekomaa vilivyo.Huu mtego una vikwazo vingi sana.
 
Pole sana Zitto kwa yanayokutokea. nadhani sasa umeamini kuwa hata ule mpango wa kutaka kukuwekea sumu ili ufe ulikuwa ni wa kweli. ingawa ulitumia nguvu nyingi sana kuukanusha lakini leo hii unatuthibitisha kuwa kuna wabaya ndani ya chama chako ambao kila kukicha wanakuandama. lengo lao si zuri hata kidogo na usipokuwa makini ujue ndiyo mwisho wako. najua harakati yao hiyo ni kutokana na dhamira yako ya kutaka kugombea urais wa nchi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Aidha hayo yanatokea huku chama kikiwa kinajiandaa kufanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya taifa huku wewe ukitadhamiria kugombea nafasi ya uenyekiti. najua katika uchaguzi huo, mpango umeandaliwa ili wewe na ARFI muondolewe kabisa kwenye safu ya juu ya uongozi. najua nafasi zenu zitachukuliwa na KITILA MKUMBO na PR. ABDALLAH SAFARI. mipango hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uchaguzi huo ufanyike. lengo kuu la mpango huo ni kutaka kukuondoa kabisa kwenye safu ya maamuzi ndani ya chama chako. hatua hiyo ilianza muda mrefu na Dr SLAA ndiyo anayeusimamia. ndiyo maana yeye anapokuwa nje ya nchi kikazi, majukumu yake anamwachia JOHN MNYIKA wakati wewe ndiye uliyekuwa unastahili. hata katika maamuzi mazito kama yale ya kuwafukuza akina MWAMPAMBA na SHONZA, mawazo yako yalipuuzwa.

ZITTO, nakushangaa sana unavyotumia nguvu nyingi na muda mwingi kuwatetea watu wasiokutakia mema. suala la lwakatare lipo bayana kabisa na ilipaswa chama kichukue hatua ili kisipakwe madoa. kitendo cha kukamatwa lwakatare kufuatia kashfa ya video ya kupanga njama za kigaidi ni aibu kubwa si tu kwa lwakatare mwenyewe bali ni kwa chama pia. kumbuka LWAKATARE ni Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama na ninaamini kuwa mipango hiyo kama si maelekezo ya Katibu Mkuu WILBROAD SLAA basi alimshirikisha katika hatua zote. nina hakika hata Mwenyekiti FREEMAN MBOWE mipango hiyo alikuwa haijui na ndiyo maana akakimbilia kusema kuwa kama LWAKATARE amehusika kwa makusudi au uzembe basi anatakiwa awajibishwe. kwa kuwa Dr Slaa anajua nini kinachoendelea katika sakata hilo, amefanikiwa kuwashawishi viongozi wote ili chama kiwe na msimamo mmoja wa kumtetea LWAKATARE kwa gharama zozote zile. tayari kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kwa ajili ya kumhonga JAJI aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo na ndiyo maana kauli imetolewa kuwa CHAMA KINA IMANI NA JAJI HUYO. kama kweli chama kinaona kuwa LWAKATARE ameonewa, iweje watenge kiasi kikubwa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa lengo tu la kuhakikisha ukweli unapindishwa? mikakati yote hiyo inafanyika bila ya wewe Naibu Katibu mkuu kushirikishwa na bila kuijua. ndiyo maana nikatangulia kusema kuwa unajaribu kuwatetea watu wasio na dhamira njema nawe.

ZITTO, hivi unajua ni kwa nini viongozi wenzako wa CHADEMA kupitia Kamati Kuu wameagiza JF kuondoa mijadala yote inayokielemea chama? ni kwamba wamebaini kuwa viongozi wa chama hawapo pamoja na matamshi yao yamekigawa chama. pia unajua ni kwa nini chama hakimtetei LUDOVICK JOSEPH wakati yeye ni mtu wa karibu sana na familia ya Dr Slaa? kama LUDOVICK amesalitiwa, je wewe ambaye ni kama damu ya kunguni kwa dr slaa utapendwa kwa lipi? ndugu yangu, nakupenda sana na najua una safari ndefu katika ukombozi wa taifa hili. wewe ni mzalendo halisi na hawa wengine wapo kwa maslahi yao tu.

zitto, tunakushukuru kwa kututhibitishia kuwa ile video ya LWAKATARE ni halisi kama alivyofanya LISSU. Ninaamini hata ule mjadala wa ama video ile ni halisi au feki umekufa baada ya kupata majawabu sahihi.

pamoja na hayo ZITTO, bado ninakushangaa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Kamati Kuu ya CHADEMA. kama wamekubaliana kuwa msemaji mkuu katika sakata la LWAKATARE ni LISSU, iweje wewe unaongelea jambo hilo katika mitandao ya kijamii? mie ninaamini cha muhimu ujumbe kutolewa. aidha Kwa kuandika au kuongea lakini kote ni kutoa ujumbe. kitendo chako cha kuendelea kuongelea suala la LWAKATARE unashindwa kuficha hisia zako na matokeo yake unakiumbua chama. najua utaniuliza mbona jambo hilo lipo mahakamani na mbona viongozi wa CHADEMA akiwemo lissu anaongelea mara kwa mara ilhali anajua kuwa huko ni kuvunja sheria. jibu ni fupi sana. LISSU anajua kuwa LWAKATARE ana hatia hivyo anajaribu kuongea kwenye public kupotosha mawazo ya watu na kutaka huruma kwa jamii ili ikiamuliwa kuwa LWAKATARE ahukumiwe kifungo warudi mitaani kuandamana kwa madai kuwa CCM wanakidhoofisha shama

namalizia kwa msemo wa kiswahili kuwa NUNGUNUNGU HAKUMBATIWI

 
Mh Zitto
Chadema have failed to practice what they preach,
Huwezi kuwashinikiza wengine wajiuzuru kupisha uchunguzi wakati yakitokea kwenu mnawakingia kifua bila kufanya uchunguzi kwanza.
Nani kakwambia uchunguzi aujafanyika???umemsikiliza Lissu??weMarioo vipi wewe
Kwanza ulishaambiwa we mgonjwa
 
Congrats ZZK....unatuonesha nn maana ya kua kiongozi....wewe ni mvumilivu sana ipo siku utashinda aisee......
 
ungekuwa na chembe ya hekima ungeizungumzia ccm na mafanikio yenu ya kuweka virusi. Kwani wewe ulijiuzuru au ulifukuzwa? Ndiyo maana dr. Alex paurine amefanikiwa kutushawishi una magonjwa yanayohitaji immediate attension.


ndugu yangu. Dhana ya kusema kuwa ccm imeingiza kirusi chadema hutumiwa na akina slaa na mbowe ili kuficha maovu yao na kuwakandamiza wanaoenda kinyume na misimamo yao
 
Mkuu nimekupata vizuri sana.Huwa napata wakati mgumu sana na kijana huyu "Zitto"nimejaribu kuangalia ushauri wake kwa chama ni mzuri mno.Nilikua najiuliza kwa nini aandike barua, wakati hii ni serious issue ambayo angeweza kukaa kitako na katibu wake mkuu na wakaijadili kwa kina kwani ni suala linalohitaji muda wa kutosha?Lakini jambo la pili, je haiwezekani kwamba yeye aliandika hii barua huku akijua italeak then atoe maoni yake na kuonekana yuko vizuri?Kwenye hili napata picha Zitto kuna kitu anakijua hivyo amejiandalia mazingira ya kuja kuonekana ni Mr. clea.Nimejaribu kuangalia tena kirusi anachokizungumzia ,nikapata picha pengine inaweza kuwa hicho kirusi, ndicho kinachotafutwa CDM kwani ,inawezekana kuwa ndio Kikwazo kwa Zitto na kundi lake kutekeleza malengo yao.najaribu pia, kuangalia urafiki wa Zitto na Msacky, pia uhusiano wa Zitto na baadhi ya mafisadi,nahitaji kumjua Zitto vizuri.

Ila yote katika yote,nawapongeza walioratibu mpango mzima wa kuisambaratisha CDM,umepangwa kwa Ustadi wa hali ya juu sana.Ndio maana haikuwawia vigumu CCM kuanza kuzungumza kwenye Press kuwa CDM itasambatratika.Hapa ndipo nataka kuona umahili wa Viongozi wa CDM, wakilivuka hili nina imani CDM itakua imekomaa vilivyo.Huu mtego una vikwazo vingi sana.
Watu bana utajuaje kama ndo mpango wa chama kuwasilisha kitu kwa njia ya barua afu ndo kinajadiliwa.....ila sishangai mitanzania ndo tulivyogo na aliyetueoga ashakufa aisee hatuezi kuona mazuri na kusifia na kumpa moyo mtenda mazuri hayo azidi kutenda na kua juu zaidi.... lazima vikasoro muanze.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom