Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Sio kirusi tu, ni virusi. Vipo vingi. Chama kifanye uchunguzi huru kuwabaini
 
Hapa kuna watu wawili tu watakuwa wanahisiwa,samahani lakini nadhani ni Dr Slaa na Ben Saanane.

Lets wait and see...
 
Zitto Zuberi Kabwe, you are presidential material! Keep your head up and work towards this role and God will be there for you. Be firm, fare and a follower at the same time and Tanzania will be in safer hands
 
Dr. Slaa amefanya makusudi kutoa siri za barua aliyandikiwa na Zitto.

Dr. Slaa anatakiwa KUWAJIBIKA...
 
Ndugu Zitto anaelekea kumaanisha kwamba kuna mtu ambaye Dr Slaa amempatia nakala ya barua yake,mtu huyo akaifanyia mabadiliko kidogo tu,kisha akaibandika hapa.

Huyo mtu AKA kirusi,ndo anayelalamikiwa na dugu Zitto,so ndo huyo form four leaver2012...

Zitto anasema laindika hiyo barua directly kwa Dr Slaa,so labda aliyemtuma ndo kalikisha,ama aliyepewa(Dr Slaa),ndiyo kafanya hivyo...

Vipi kuhusu hugochavez anapodai kuvujisha video ya lwakatare, je hufikirii anamanisha ni siri ya CDM kitu ambacho ni haramu?
 
Pole sana Zitto kwa yanayokutokea. nadhani sasa umeamini kuwa hata ule mpango wa kutaka kukuwekea sumu ili ufe ulikuwa ni wa kweli. ingawa ulitumia nguvu nyingi sana kuukanusha lakini leo hii unatuthibitisha kuwa kuna wabaya ndani ya chama chako ambao kila kukicha wanakuandama. lengo lao si zuri hata kidogo na usipokuwa makini ujue ndiyo mwisho wako. najua harakati yao hiyo ni kutokana na dhamira yako ya kutaka kugombea urais wa nchi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. aidha hayo yanatokea huku chama kikiwa kinajiandaa kufanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya taifa huku wewe ukitadhamiria kugombea nafasi ya uenyekiti. najua katika uchaguzi huo, mpango umeandaliwa ili wewe na ARFI muondolewe kabisa kwenye safu ya juu ya uongozi. najua nafasi zenu zitachukuliwa na KITILA MKUMBO na PR. ABDALLAH SAFARI. mipango hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uchaguzi huo ufanyike. lengo kuu la mpango huo ni kutaka kukuondoa kabisa kwenye safu ya maamuzi ndani ya chama chako. hatua hiyo ilianza muda mrefu na Dr SLAA ndiyo anayeusimamia. ndiyo maana yeye anapokuwa nje ya nchi kikazi, majukumu yake anamwachia JOHN MNYIKA wakati wewe ndiye uliyekuwa unastahili. hata katika maamuzi mazito kama yale ya kuwafukuza akina MWAMPAMBA na SHONZA, mawazo yako yalipuuzwa.

ZITTO, nakushangaa sana unavyotumia nguvu nyingi na muda mwingi kuwatetea watu wasiokutakia mema. suala la lwakatare lipo bayana kabisa na ilipaswa chama kichukue hatua ili kisipakwe madoa. kitendo cha kukamatwa lwakatare kufuatia kashfa ya video ya kupanga njama za kigaidi ni aibu kubwa si tu kwa lwakatare mwenyewe bali ni kwa chama pia. kumbuka LWAKATARE ni Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama na ninaamini kuwa mipango hiyo kama si maelekezo ya Katibu Mkuu WILBROAD SLAA basi alimshirikisha katika hatua zote. nina hakika hata Mwenyekiti FREEMAN MBOWE mipango hiyo alikuwa haijui na ndiyo maana akakimbilia kusema kuwa kama LWAKATARE amehusika kwa makusudi au uzembe basi anatakiwa awajibishwe. kwa kuwa Dr Slaa anajua nini kinachoendelea katika sakata hilo, amefanikiwa kuwashawishi viongozi wote ili chama kiwe na msimamo mmoja wa kumtetea LWAKATARE kwa gharama zozote zile. tayari kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kwa ajili ya kumhonga JAJI aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo na ndiyo maana kauli imetolewa kuwa CHAMA KINA IMANI NA JAJI HUYO. kama kweli chama kinaona kuwa LWAKATARE ameonewa, iweje watenge kiasi kikubwa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa lengo tu la kuhakikisha ukweli unapindishwa? mikakati yote hiyo inafanyika bila ya wewe Naibu Katibu mkuu kushirikishwa na bila kuijua. ndiyo maana nikatangulia kusema kuwa unajaribu kuwatetea watu wasio na dhamira njema nawe.

ZITTO, hivi unajua ni kwa nini viongozi wenzako wa CHADEMA kupitia Kamati Kuu wameagiza JF kuondoa mijadala yote inayokielemea chama? ni kwamba wamebaini kuwa viongozi wa chama hawapo pamoja na matamshi yao yamekigawa chama. pia unajua ni kwa nini chama hakimtetei LUDOVICK JOSEPH wakati yeye ni mtu wa karibu sana na familia ya Dr Slaa? kama LUDOVICK amesalitiwa, je wewe ambaye ni kama damu ya kunguni kwa dr slaa utapendwa kwa lipi? ndugu yangu, nakupenda sana na najua una safari ndefu katika ukombozi wa taifa hili. wewe ni mzalendo halisi na hawa wengine wapo kwa maslahi yao tu.

zitto, tunakushukuru kwa kututhibitishia kuwa ile video ya LWAKATARE ni halisi kama alivyofanya LISSU. Ninaamini hata ule mjadala wa ama video ile ni halisi au feki umekufa baada ya kupata majawabu sahihi.

pamoja na hayo ZITTO, bado ninakushangaa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Kamati Kuu ya CHADEMA. kama wamekubaliana kuwa msemaji mkuu katika sakata la LWAKATARE ni LISSU, iweje wewe unaongelea jambo hilo katika mitandao ya kijamii? mie ninaamini cha muhimu ujumbe kutolewa. aidha Kwa kuandika au kuongea lakini kote ni kutoa ujumbe. kitendo chako cha kuendelea kuongelea suala la LWAKATARE unashindwa kuficha hisia zako na matokeo yake unakiumbua chama. najua utaniuliza mbona jambo hilo lipo mahakamani na mbona viongozi wa CHADEMA akiwemo lissu anaongelea mara kwa mara ilhali anajua kuwa huko ni kuvunja sheria. jibu ni fupi sana. LISSU anajua kuwa LWAKATARE ana hatia hivyo anajaribu kuongea kwenye public kupotosha mawazo ya watu na kutaka huruma kwa jamii ili ikiamuliwa kuwa LWAKATARE ahukumiwe kifungo warudi mitaani kuandamana kwa madai kuwa CCM wanakidhoofisha shama

namalizia kwa msemo wa kiswahili kuwa NUNGUNUNGU HAKUMBATIWI


Ama akili nyingi huondoa maarifa! Ni bora mngekuwa mmetumia njia nyingine za kuwafanya Chadema ''wamkane'' Rwakatare kwani hii mbinu ya kulazimisha kwenye mtandao imeshindikana. Mtaambulia patupu kama yule fisi aliyekuwa ananyemelea mkono udondoke kwani Chadema kamwe haitafanya kama ninyi mnavyotaka bali kama inavyoona!
 
Zitto uwezo unao na natamani kumuona zitto wa mika ya 2005 kaka. Kila la.kheri
Jay Z alipokuja na album yake mpya kuna verse alisema "If you like ma old shit,buy my old album"
 
mbona jina lako linatisha? Hata hivyo nilivyo ukinitajia jina la mtu kuwa ndiyo hoja badala ya hoja inayohusu suala la kijamii huwa natilia shaka. Kama kuna maovu vyombo vya sheria vinashindwaje kuchukua hatua? Ukweli ukuweke huru

kama chama kinakubaliana kuwatetea wahalifu, hapo vyombo vya dola vitasimama wapi. Jukumu la polisi ni kuwakamata na kuwafikisha mahakamani. Kama chama kinakubaliana kuhonga ili lwakatare aachiwe, hapo vyombo vya dola bado utavilaumu? Dhana ya ulinzi shirikishi itazaa matunda?
 
Ama akili nyingi huondoa maarifa! Ni bora mngekuwa mmetumia njia nyingine za kuwafanya Chadema ''wamkane'' Rwakatare kwani hii mbinu ya kulazimisha kwenye mtandao imeshindikana. Mtaambulia patupu kama yule fisi aliyekuwa ananyemelea mkono udondoke kwani Chadema kamwe haitafanya kama ninyi mnavyotaka bali kama inavyoona!
Mkuu kirusi hicho achana nacho tusonge mbele na M4C
 
Vipi kuhusu hugochavez anapodai kuvujisha video ya lwakatare, je hufikirii anamanisha ni siri ya CDM kitu ambacho ni haramu?
Hapo Zitto kalikoroga kwa nia njema?

BTW barua ya Zitto iliyolikishwa,ni ya hivi majuzi tu wakati wa kikao cha kamati kuu,huyo Ludo wanayemuhusisha na video sidhani kama ndo kirusi kinachozungumziwa hapa.

Siwezi kusema ni haramu kwasababu sijui kama ni kweli hilo la video ya Lwakatare lilikuwa ni siri ya chama cha chadema.
 
ama akili nyingi huondoa maarifa! Ni bora mngekuwa mmetumia njia nyingine za kuwafanya chadema ''wamkane'' rwakatare kwani hii mbinu ya kulazimisha kwenye mtandao imeshindikana. Mtaambulia patupu kama yule fisi aliyekuwa ananyemelea mkono udondoke kwani chadema kamwe haitafanya kama ninyi mnavyotaka bali kama inavyoona!


mbona hueleweki? Chadema ipi unayoizungumzia
 
Ohoup!!!!! Asante zitto nimeshiba wala msikate tamaa kazeni uzi. Ujue kumnyang'anya simba nyama yake hata kama inasumu itamwua ni kazi. Ccm iko madarakani na wana pesa tuwe makini sasa hapana kumwamini mtu watawatumia sasa vijana njaa akijulikana kirusi huyo atajua mungu hii taabu anyotupa. Nimekasirika sana.
 
Nimefurah sn zitto kulitolea hilo suala ufumbuz kwa wakati.ccm wanatumia nguvu nyng sn kukabiliana na cdm,lait wangezielekeza hzo nguvu kutatua matatizo yanao wakabili wananch km taifa tungekuwa mbali.kinacho nifariji ni kuona kiwango cha uelewa miongon mw wananch kikiongezeka kila kukicha.tutasikia na kushuhudia meng kuelekea 2015.Big up zzk, big up cdm.!.
 
Dr. Slaa amefanya makusudi kutoa siri za barua aliyandikiwa na Zitto.

Dr. Slaa anatakiwa KUWAJIBIKA...

tukiweka list ya watu ambao wanatakiwa kuwajibika ccm tutajaza sever bure.......mulogo and the like.bila kumtaja dr.slaa lazima ulale mchongoma eh?basis ya malipo depend how many time umemtaja na kumchafua
 
Sio kirusi tu, ni virusi. Vipo vingi. Chama kifanye uchunguzi huru kuwabaini

HAINA HAJA YA KUFANYA UCHUNGUZI, WANAJULIKANA. NI DR SLAA na Mbowe. hawa wakikaa pembeni chama kitasonga mbele. kwani hao ni akina nani? mbona chama kilikuwepo kabla wao kuwa viongozi?
 
kama chama kinakubaliana kuwatetea wahalifu, hapo vyombo vya dola vitasimama wapi. Jukumu la polisi ni kuwakamata na kuwafikisha mahakamani. Kama chama kinakubaliana kuhonga ili lwakatare aachiwe, hapo vyombo vya dola bado utavilaumu? Dhana ya ulinzi shirikishi itazaa matunda?

Hoja yako ina maana una uhakika chama kinatetea uhalifu bila ushahidi "Narrow mind narrow argument".

Vyombo vyako vya dola havina ushahidi ndiyo maana wanakosa mahali pa kusimama.

Jukumu la polisi ni kusimamia usalama wa raia na mali zake. Polisi wanaosubiri kukamata wahalifu wawfikishe mahakama ni wa CCM peke yao.

Tuhuma za kuhonga bila ushahidi ni mbinu mufilisi za wenye ukomo mfupi sana wa kufikiri.

Dhana ya ulinzi shirikishi itazaa matunda matunda ya ufisadi tu kwa sababu dhana ni shuka ya kujifunika kwa jeshi la polisi kushindwa kwenye majukumu yake hata Waziri Nchimbi analijua hilo.

Kulingana na ujio wako humu jamvini nakushauri uombe review ya assignment yako

Join Date : 28th March 2013
Posts : 63
Rep Power : 314
Likes Received5
Likes Given0​
 
Kwanza kulikuwa na sababu ya kukiandia CHAMA barua in the first place? Ukitaja chama kwa sisi tulio wanachama wa Kawaida unamzungumzia Zitto na viongozi wenzake wakuu, sasa alikuwa anamwandikia nani huko chamani hiyo barua ambayo hatimae eti imevuja? Pili, Zitto aliwahi kutuhumiwa kuwa anahongwa kwenye kamati yake ya POAC, Je Chama au kuna kiongozi aliyeandika barua ya kumshinikiza aachie nafasi zake zote kupisha uchunguzi uliokuwa unaendelea Hata uenyekiti wa kamati hakuachia? Kwanini amekuwa na haraka ya kutaka Lwakatare atelekezwe na Chama wakati yeye hakufanyiwa hivyo na Chama! Tatu, Kama Zitto ambavyo amekiri kuwa maadui wanaitafuta CHADEMA je hajui kuwa Lwakatare pia yuko mstari wa mbele vitani na lolote linaweza kumpata? Je, ni busara kumtelekeza mwanajeshi aliyejeruhiwa vitani! Barua ya Zitto na Maelezo yake yanazua maswali zaidi kuliko majibu! My clock is ticking on Zitto Kabwe!
 
Last edited by a moderator:
Ndugu Zitto anaelekea kumaanisha kwamba kuna mtu ambaye Dr Slaa amempatia nakala ya barua yake,mtu huyo akaifanyia mabadiliko kidogo tu,kisha akaibandika hapa.

Huyo mtu AKA kirusi,ndo anayelalamikiwa na dugu Zitto,so ndo huyo form four leaver2012...

Zitto anasema alindika hiyo barua directly kwa Dr Slaa(barua isiyo public),so labda aliyemtuma ndo kalikisha,ama aliyepewa(Dr Slaa),ndiyo kafanya hivyo...


Ama anayetunza mafaili ya Dr Slaa...ama mtu anayeweza ku access hilo file.., ama ni mtu anayeweza kuaccess mafile kwenye computer ya ZITO iliyotumika kuandika hizo nyaraka, au marafiki wake zito alioshauriana nao kabla hajaandika, au wale aliokwenda kujisifia kwao baada ya kuandika hiyo barua.

Suala la Video ya Rwakatare kuvuja, sijaliona kwenye maelezo ya Zito. Haina hata maana kwa CDM ama chama chochote ama mtu binafsi kutengeneza video ya namna hiyo, iwe kwa matumizi halali ya chama ama kwa visasi. It is absolutely nonsense. Labda kwa matumizi ya uchawi maana huko ndiko kuna mammbo ya tofauti na dunia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom