Ok....
Hongera sana mkuu kwa kuja kusawazisha mambo mapema...
Niliwahi kusema mapema kuwa the central point ya mikakati ya CCM kuivuruga CDM ni kwa kumtenganisha Zitto na Chama... Nashukuru Zitto bando yupo Imara ingawa ni majaribu magumu sana...
Niliwahi kusema tena kama inavyonenwa kuwa "Sio kila anayesema Bwana Bwana ataurithi ufalme wa mbinguni" basi pia
"Sio kila anayesema Slaa, Slaa ni mwenzetu katika CDM"... Na leo naongeza usemi kuwa kama ilivyoandikwa "Watakuja wengi kwa jina langu, lakini muwe makini maana ni waongo"... Wafuasi wa CDM tujue kuwa "Watakuja wengi kwa jina la Slaa, lakini, kahika wao ni wana wa yule ibilisi, CCM"
Walijitokeza watu hapa wakajifanya kuwa karibu sana na Dr Slaa, na kumshambulia
Zitto kwa nguvu nyingi sana. Wanachadema wengi 'walizolewa' nao kwa bahati mbaya, lakini wachache tulioziona nyufa nyembamba kwao, tulisimama imara kuitetea CDM, bila kumtenga Zitto,.. tulitukanwa sana na hadi sasa kuna watu wananiona mimi kama msaliti.
Barua ya Zitto iliyowekwa hapa, na maelezo yake haya yanathibitisha umuhimu wa wanachadema tusimuamini kila mtu anayekuja hapa akijifanya kuwa yeye yuko karibu sana na Slaa, huku akiponda viongozi wengine wa chama. Hiki ni kielelezo kuwa ndani ya CDM, kuna watu bado wanahakikisha kuwa wanakigawa chama kwa kumchonganisha Zitto... Kama Zitto anasema kuwa barua aliyomwandikia Slaa ilikuwa imesainiwa, lakini barua hiyo tumewekewa hapa ikiwa haijasainiwa, ina maana kuwa kuna mtu alimsomea mtu kwa simu kilichokuwa humo ndani, na huyo aliyesomewa akaandika barua hiyo...
Kama mtu aliyeweka video ya Lwakatare ndiye aliyeweka barua ya Zitto... Kama barua ya Zitto imewekwa wka lengo la kuonyesha Zitto haungi mkono chama, ina maana kuwa lengo ni kumchonganisha Zitto na chama na wanachama. Ukiangalia video ya Lwakatare, utaona lengo ni kuonyesha kuwa CDM inamchukia Msaky kwa sababu yuko karibu na Zitto. Matendo yote haya mawili yana lengo moja... kuhakikisha Zitto anatenganishwa na CDM...
Namchukuru sana Zitto kwa kuendelea kuwa imara ndani ya chama, nawashukuru wanachadema wanaoamini kuwa Slaa ndiye chaguo la wengi katika kuiongoza CDM kuwatetea wanyonge, lakini viongozi wengine pia akiwemo Zitto ni muhimu sana katika kuhakikisha uimara na umoja wa CDM unadumishwa na nawaomba CDM wajue kuwa TISS wapo pale makao makuu Kinondoni pia, wanaitana Kamanda, wanasalimiana Peoples power, wanashiriki M4C, wanajifanya kuwa wanamuunga mkono Slaa na CDM kwa ujumla... lakini tusipokuwa makini kuna siku tukishakusambaratika, tutainua macho tuwaone wale "Wenzetu" wakiwa wananeemeka katika utawala wa Ibilisi...
Wake up people.... CCM hawatakubali kuachia madaraka so easily kama tunavyodhani...