T2015CCM
JF-Expert Member
- Sep 13, 2012
- 7,930
- 991
naona unatafuta ugomvi na slaa weweKazi ya kuvuruga cdm imebaki inafanywa na mjinga mmoja kwa jina la Ben Saa 8
naona unatafuta ugomvi na slaa weweKazi ya kuvuruga cdm imebaki inafanywa na mjinga mmoja kwa jina la Ben Saa 8
Tetesi zilizopo ni kua Josephine Mshumbusi mke wa Dr slaa ana pepesa macho sana kwenye document za Chadema!
Mods wanafanya vizuri kwa sababu taarabu yako melody imechuja wana JF angkupa Ban kabisa,
Mkuu kusema kweli Zitto sio mtu wa kumwamini inawezekana yeye mwenyewe ndio anajiwekea nakala za barua zake humu pia nina wasiwasi mkubwa yeye ndio Bukoba Boy iweje aje haraka hapa na kusema mtu yule yule aliyeweka ile movie kwa youtube ndio huyo huyo aliyeweka barua yake,Hapa mie huyu jamaa namshuku niko na kisa cha ukweli sitakisahau maishani mwangu wakati niko High School ya Boys ambayo ilikuwa bording,tulikuwa tukifunga shule kila mtu anapeleka godoro lake kwa bweni moja hivi na kusaini kwamba kaweka pale tarahe hiyoo nk,sasa basi wakati tunafungua shule kuna jamaa kaingia kachukua godoro lake bila kusaini then later on kaenda ripoti kuwa kaibiwa godoro kaulizwa ulisaini wakati unachukua kasema hapana ila nimecheki kupitia dirishani na kuona halipo pale nilipoweka kaambiwa utawezaje kutambua godoro lako wakati karibu yanafanana na jina liko upande mwingi wa godoro lako.then kambiwa asubiria ili wote wakichukua magodoro yao litakalo baki ni lake lakini watu tukachukua na hakuna lililobaki baada ya uchunguzi kumbe alijiibia mwenyewe so huyu jamaa namfananisha na Mh Zito simwamini hata kidogo japokuwa nilimwambia akaa na wenzake.
kapenge wewe bado mtoto
jmushi1,
Sipendi kuandika sana mambo yanayonigusa moja kwa moja kwenye mtandao.Huwa ninakereka sana na kusingiziwa huku kunakotokana na jitihada za watu ambao wako frustrated.
Sijui ni kwanini mtu anihisi katika hili. jmushi1,sijajua ni kwanini umenihisi.Pengine una vigezo
Naelewa una uwezo mkubwa sana wa kujenga hoja.Na huku JF tumepambana sana pamoja tukiwa na Kichuguu na @Rev.Kishoka.
Wewe si mtu muoga,hebu sema hii conclussion umefikiaje
Kwa wanajamvi:
-Mimi sijahusika kwa lolote
-Mimi ni miongoni mwa watu wanaopinga maswala senstive ya chama kuwekwa public
-Kuna watu ambao hawaoni aibu katika hili.Akina my web , TUNTEMEKE, rais wa tano, Fringe, nice2 MsemajiUkweli , Shonza n.k wanajua huu mchezo wa kuanika vitu ambavyo havipo for public consumption humu.Hawa niliowataja ni ID za kundi fulani mahsusi
-Sijawajahi kupata access ya barua au docoment nyeti za chama changu na hata nikikutana nazo kwa sababu yoyote ile siwezi ku-ziweka public.Nakipenda chama changu,CHADEMA ni mti wenye matunda ambao nimekalia tawi lake.Siwezi kulikata kwa namna yoyote ile,ni bora nife kwa risasi,tindikali n.k kuliko kuvunjika kiungo cha mwili kwa upumbavu wa kukata tawi nililokalia.
Nawaachia wanaocheza michezo hii waicheze.CHADEMA tuendelee kuwa imara
Kwenye ukweli mazingaombwe ukaa kando,,Hapa duniani sisi ni wapita njia yote tunayoyafanya au kufanyiana kimaovu uturudia wenyewe ikiwa kama sio leo kesho
Watu safi watabaki kuwa safi hata wakinyeshewa namvua ya matope
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
Hii kama authentic safi sana. Chadema shikamaneni kana super glue. Nchi hii bila chama makini mbadala tumekwisha.Nimetafutwa na uongozi wa JamiiForums ili kutoa maelezo kuhusu barua iliyowekwa jukwaani inayoonyesha kuwa ndani ya chama kuna kutoelewana kuhusiana na msimamo juu ya kesi inayomkabili mmoja wa viongozi waandamizi wa chama Ndg. Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama.
Maelezo yangu ni kama ifuatavyo:
1. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa chama mnamo tarehe 15 Machi 2013 kutaka chama kifanye uchunguzi wake wa ndani kuhusiana na ukweli wa video iliyowekwa kwenye mitandao inayoonyesha kuwa Kiongozi wetu mwandamizi anapanga mipango ya kumdhuru Mhariri wa moja ya magazeti hapa nchini​. Sikuamini kabisa mambo yale na hivyo kutoa ushauri kwa chama kwamba tufanye uchunguzi wetu wa ndani ili kujiridhisha. Uchunguzi wa ndani ungetufanya kuweka mikakati wa namna bora zaidi ya kulinda chama dhidi ya njama zozote, za ndani au za nje ya chama.
2. Mapendekezo yangu ndani ya chama kamwe hayakulenga kumtosa ndugu Lwakatare wakati huu anakabiliwa na changamoto hii bali yalilenga kuhakikisha kuwa wakati tunamlinda na kumtetea ili haki itendeke, lazima tuhakikishe kuwa chama hakitaathirika na sakata hili kwa namna yeyote ile. Ni jukumu letu kuhakikisha sura (image) ya chama inabakia salama maana hatujui mikakati (game plan) ya maadui zetu kisiasa hasa baada ya kauli zao kwamba chama kitakufa kabla ya 2015 ambayo imerudiwa rudiwa sana. Ni lazima kutilia shaka (doubt) kila linalotokea sasa kwa kulipima kwa jicho la mbele zaidi. Ikumbukwe maneno ya Mwenyekiti wetu "Mwenyekiti Freeman Mbowe anataka ikithibitika kuwa Lwakatare alishiriki kurekodi mkanda huo iwe kwa kurubuniwa, ‘kushikishwa' au kuingizwa mkenge, itamlazimu kuwajibika kwa kosa la kukosa umakini" (Gazeti la Jamhuri).
3. Barua ile ya tarehe 15 Machi 2013 ilikuwa ni ya ndani ya chama, haikuwa ya kiofisi bali ya Zitto Kabwe kwa chama, ilisainiwa na haikukusudiwa kuwa ‘public'. Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Barua imewekwa masaa machache baada ya kikao cha Kamati Kuu kwisha ambapo tuliweka msimamo wa pamoja wa chama juu ya namna bora ya kushughulikia suala la Lwakatare kama chama. Wakati mweka barua anadai kuwa kulikuwa na mgawanyiko katika kikao, ukweli ni kwamba ajenda hiyo haikuwa na mjadala wenye mgawanyiko kabisa na msimamo wa chama ulipatikana kwa mwafaka bila mgawanyiko. Ni dhahiri kuwa maadui zetu walitaraji mgawanyiko na baada ya kushindwa sasa wanatengeneza mgawanyiko huo kwa kusambaza uwongo wenye uzandiki.
4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. ‘Coincidence' ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa ‘kwamba kuna kirusi ndani ya chama kilicho karibu sana na viongozi wa chama chenye kazi moja tu, yani kuonyesha kuwa CHADEMA hapako shwari, kuna migogoro na hatimaye kusambaratisha chama'. Kirusi hiki lazima kina nafasi andamizi au kipo karibu sana na viongozi waandamizi. Inawezekana kabisa kirusi hiki kinahusika na suala zima la Lwakatare katika kupanga, kuendesha na kutekeleza mpango mzima. Maswali kama ‘kwanini Dennis Msacky na Zitto ndani ya Video ya ‘Lwakatare' lazima sasa yaanze kutafutiwa majawabu.
5. Natoa wito tena kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kwamba, huu ni wakati wa kuwa na umoja na mshikamano kuliko wakati wowote ule katika uhai wa chama chetu. Chama cha Mapinduzi kitatumia njia zote kutugawa, kutugombanisha na kupenyeza chuki miongoni mwetu katika juhudi za wao kubakia madarakani. Umakini wa Kiongozi huonekana wakati wa changamoto kama hizi!
6. Msimamo wa chama umetolewa na Kamati Kuu iliyomaliza vikao vyake jana siku ya ijumaa tarehe 5 Aprili 2013. Huo ndio msimamo wangu pia! Kesi ya Lwakatare ipo mahakamani, chama kimeonyesha dhahiri kumwamini Jaji aliyekabidhiwa kesi hii, sasa tuache mahakama ifanye kazi yake na tusubiri hukumu. Msemaji wa chama kuhusu suala hili ni ndugu Tundu Lissu na amekuwa akitoa ufafanuzi kila inapohitajika.
Asanteni
Kazi ya kuvuruga cdm imebaki inafanywa na mjinga mmoja kwa jina la Ben Saa 8
waambiye watoto watu wazima hatudanganyiki, tatizo shilingi 200 anazowatumia mwigulu kwa M-Pesa zimewatia kichaa hamjui hata ya kuandikaTetesi zilizopo ni kua Josephine Mshumbusi mke wa Dr slaa ana pepesa macho sana kwenye document za Chadema!
Ni lini umekua na uchungu na Chadema wewe?Post zako za nyuma zinakuonyesha kuwa adui wa CHADEMA.Ni lini ulianza kukipenda?Najua unaidhika sana ninavyowaharibia mipango miovu dhidi ya Chadema.Na bado ...
Ben Saanane
Today 17:33 #346
JF Senior Expert Member
Array
Join Date : 18th January 2007
Posts : 6,097
Rep Power : 15809
Likes Received
4051
Likes Given
5998
By Bokilo Jr
Mkuu kusema kweli Zitto sio mtu wa kumwamini inawezekana yeye mwenyewe ndio anajiwekea nakala za barua zake humu pia nina wasiwasi mkubwa yeye ndio Bukoba Boy iweje aje haraka hapa na kusema mtu yule yule aliyeweka ile movie kwa youtube ndio huyo huyo aliyeweka barua yake,Hapa mie huyu jamaa namshuku niko na kisa cha ukweli sitakisahau maishani mwangu wakati niko High School ya Boys ambayo ilikuwa bording,tulikuwa tukifunga shule kila mtu anapeleka godoro lake kwa bweni moja hivi na kusaini kwamba kaweka pale tarahe hiyoo nk,sasa basi wakati tunafungua shule kuna jamaa kaingia kachukua godoro lake bila kusaini then later on kaenda ripoti kuwa kaibiwa godoro kaulizwa ulisaini wakati unachukua kasema hapana ila nimecheki kupitia dirishani na kuona halipo pale nilipoweka kaambiwa utawezaje kutambua godoro lako wakati karibu yanafanana na jina liko upande mwingi wa godoro lako.then kambiwa asubiria ili wote wakichukua magodoro yao litakalo baki ni lake lakini watu tukachukua na hakuna lililobaki baada ya uchunguzi kumbe alijiibia mwenyewe so huyu jamaa namfananisha na Mh Zito simwamini hata kidogo japokuwa nilimwambia akaa na wenzake.
Haha ha haaa
mnafiki hajifichi hata kama ajifunike blanketi jeusi.
mwisho wako umekaribia na utaharibikiwa wewe.
Mkuu,
Tafadhali yaache hayo. Yatatuharibia thread. Focus iwe kwenye kumshinikiza dr. Slaa ajiuzuru kwa kushindwa kutekeleza wajibuwake wa kutunza siri za ofisi.
Wewe ndio unaemuona muovu lakini wengine wanamuona mtu safiUnachokisema kinasikika vizuri. Lakini unfortunately dunia haiko hivyo. Mtu anaweza kufanya makosa makubwa na yakaachwa na historia ikaandikwa kuwa mtu huyo ni shujaa. Angalia mfano makosa aliyofanya Bush ya kuvamia Iraq, makosa yale yangefanywa na kiongozi wa nchi nyingine angekuwa kwenye wakati mgumu sana sasa hivi.
Kwahiyo kuamini kuwa ukweli utajileta tu bila kutafutwa sio sahihi.
Dr. Slaa ni muovu. Hatunzi nyaraka za siri za ofisi kama inavyotakiwa.
Ni wakati muafaka wa Dr. Slaa kujiuzuru kwa kushindwa kutunza siri za ofisi.