Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Usisahau 2015
uchaguzi matokeo ni kama hivi
CCM 52%
CUF 26%
CDM 14%0
The rest watagawana wapinzani, najua mods wameikata na kuifadhi.
Aibu kwenu Cdm.

Tanga kunani paleeee eeee Tanga shame on you Tanga peoples kumbuka Maccm ya leo hii ukiacha ile ya Mwalimu ndio wameichakachua Tanga hadi leo hii imekuwa nyuma kimaendeleo kipindi hicho tukiwa watoto miaka ya 90 wakati huo nasoma darasa la tatu kama sikosei ilkuwa Tanga atleast jinsi miaka inavyosonga Lol kila kitu chaenda mfu bana kwetu Tanga pia sema nina siku mingi jo sijatia maguu.mwisho ilikuwa mwaka ule 2002 wakati nimepitia pale Amboni Caves Lol Tanga yangu so kama umeamua kuwapa kura yako Maccm mkuu kumbuka kwetu ndio kutakufa kabisaaaaaaaaaaa.
 
Nimefuatilia Kwa makini kimbunga Cha Siasa Zetu Na Kama kawaida napenda kukusanya mlolongo wote wa matukio Na kutengeneza tafsiri Moja..

Tokea mchezo huu Wa kuwadhuru binaadam sisi watanzania wenzao, Na kuunganisha unyama huu Na mambo ya kisiasa uanze, kuna kila dalili ya fukuto hili kuzidi kutiwa chumvi Na kuvuma pasipo Sababu yoyote ya msingi ndani ya CDM.

Barua iliyomwagwa mtandaoni isiyosainiwa Kwamba Mhe Zitto alimwandikia Katibu Mkuu wa CDM juu ya clarification kadhaa zinazopaswa kuchukuliwa juu ya suala la ...Rwakatale Na Chadema Kwa Ujumla, wimbi la Baadhi ya wanachama wa CDM kuhongwa Na MIMTU ILIYOLAANIWA NA KULAANIKA, Kwamba watoe ushahidi wa dhulma juu ya Kesi ya Rwakatale, Clarification Za. mhe Zitto Juu ya Barua ile hapa mtandaoni na kuonyesha hofu yake Kwamba Ndani kabisa ya CDM kuna "nyokas" au VIRUSI wanaovujisha taarifa ni mwendelezo wa fukuto ambalo Lazima tushauri kama raia WA Nchi yetu tunaopenda mageuzi ya HAKI..

HAKUNA haja ya kumsaka "KIRUSI AU VIRUSI AKA NYOKAS" Ndani au NJE ya CDM, kuwekeza nguvu kuwasaka nyoka Wala hamtawamaliza, wapo, walikuwepo Na watakuwepo, vichaa huwezi kuwaondoa mjini ukawamaliza wote. Shambani tunajifunza mengi, unapolima Na kupanda mbegu zako Na magugu yanatend kuota sambamba Na mmea kusudio, ukipambana Na magugu Kwenye hali ya uchanga unahatarisha maZao mema, wacha mmea ukue, time will tell, gugu utaliadentify easily Na kuliondoa..

Chama chote kujikita kuongelea Rwakatale all days ni matumizi makubwa ya nguvu Za watu makini zisizo Na Sababu, JUKUMU Hilo analo Mhe jembe la Ukweli Tundu Lissu, aachiwe Yeye, Uwezo wa Tundu unatosha kabisa kuwakabili TISS, Polisi, Mahakama, Na CCM yote wakijumlisha Uwezo wao wanafit kidole tu Cha hili Jembe..

Ni Muda Muafaka sasa wa VIONGOZI kuiamsha serikali si mnajua serikali ya sasa inasubiri CHADEMA aseme jambo ndio watende?, sasa endeleeni kutema vitu, ni Muda Muafaka sasa wa kulichukua JIMBO LA IGUNGA, si mnajua serikali imeagiza zaidi ya kampuni moja wafanye Kazi usiku Na mchana kuhakikisha daraja la Mbutu linakamilika ndipo watangaze tarehe ya uchaguzi huo?.. Daraja wanakamilisha Na jimbo linaenda CDM.. Hivi nani ulimwengu we Leo ataichagua CCM honestly tell me..

Kuna kampeni zimeshaanza huku mitaani Za uongozi Wa serikali Za mitaa, 2014 imekaribia sana,, kuna move inayoendelea ya kusimika uongozi Wa kikanda, kuna M 4 C nk.

Yule ambaye Kwenye movement Na shamrashamra hizi Za kichama, hatajitokeza kuwa mstari wa Mbele mjue direct ndio KIRUSI mwenyewe Na ahukumiwe Kwa matendo yake ..
Adios..
 
Hii single ya kirusi haiuzi kwangu labda kwa wengine. Anataka CHADEMA waanze kumtafuta kirusi wakati ni yeye mwenyewe ZZK aliyelikisha barua
Said it well......my foot! ZZK now wants us to get busy trying to find out who is leaking CHADEMA information(which is not true) He is actually fanning the spark into a great fire
 
mnafiki tu wewe huna lolote, unapenda sana kutajataja majina ya watu humu...haya unayafanya kwa maslahi yako kama kibaraka wa mtu wako wala sio kwa maslahi ya chadema..usifikiri haujulikani....

rais wa tano umesahau ulipokua CHADEMA nilikua nakukataza kupeleka habaribza uongo gazeti la Afrika leo na gazeti la HOJA ?

Wewe unaandika hapa kwa maslahi ya nani.Subiri JF members wafuatilie ID yako kuona kama post zako zinaonyesha nia njema kwa Chadema kama si maslahi binafsi

Nakutakia ziara njema mkoani kilimanjaro.Ila waeleze pia uliwabatiza jina la kibaguzi na kuwaita 'WAGAZZA'.Hata katibu wako mpya wa itikadi na uenezi anastahili kuomba radhi huko maana alishatoa kauli za kibaguzi.Kama huu ni unafiki nimeuendeleza na siachi.Jioni njema,
 
Last edited by a moderator:
asante sana ZITTO,

Ndio maana hadi sasa MAGAMBA hayajasema lolote kwenye hii clarification,inaonyesha namna gani yanavyoumbuka, ila hiki kirusi lazima tufanye kazi ya ziada kukibaini,hiki kirus kitaumbuka sana.
 
Ungekuwa mtu safi ungeshiriki kwenye harakati za kuhimiza kuwa ni wakati muafaka wa Dr. Slaa kujiuzuru kwa kushindwa kutunza siri za ofisi.

Bila kufanya hivyo unakuwa responsible kwa mchezo anaocheza.

This is digital politics, you either have one or zero. No portions...

ZeMarcopolo the hater....!

Nitaufanyia kazi ushauri wako
 
Last edited by a moderator:
Ok....

Hongera sana mkuu kwa kuja kusawazisha mambo mapema...

Niliwahi kusema mapema kuwa the central point ya mikakati ya CCM kuivuruga CDM ni kwa kumtenganisha Zitto na Chama... Nashukuru Zitto bando yupo Imara ingawa ni majaribu magumu sana...

Niliwahi kusema tena kama inavyonenwa kuwa "Sio kila anayesema Bwana Bwana ataurithi ufalme wa mbinguni" basi pia "Sio kila anayesema Slaa, Slaa ni mwenzetu katika CDM"... Na leo naongeza usemi kuwa kama ilivyoandikwa "Watakuja wengi kwa jina langu, lakini muwe makini maana ni waongo"... Wafuasi wa CDM tujue kuwa "Watakuja wengi kwa jina la Slaa, lakini, kahika wao ni wana wa yule ibilisi, CCM"

Walijitokeza watu hapa wakajifanya kuwa karibu sana na Dr Slaa, na kumshambulia Zitto kwa nguvu nyingi sana. Wanachadema wengi 'walizolewa' nao kwa bahati mbaya, lakini wachache tulioziona nyufa nyembamba kwao, tulisimama imara kuitetea CDM, bila kumtenga Zitto,.. tulitukanwa sana na hadi sasa kuna watu wananiona mimi kama msaliti.

Barua ya Zitto iliyowekwa hapa, na maelezo yake haya yanathibitisha umuhimu wa wanachadema tusimuamini kila mtu anayekuja hapa akijifanya kuwa yeye yuko karibu sana na Slaa, huku akiponda viongozi wengine wa chama. Hiki ni kielelezo kuwa ndani ya CDM, kuna watu bado wanahakikisha kuwa wanakigawa chama kwa kumchonganisha Zitto... Kama Zitto anasema kuwa barua aliyomwandikia Slaa ilikuwa imesainiwa, lakini barua hiyo tumewekewa hapa ikiwa haijasainiwa, ina maana kuwa kuna mtu alimsomea mtu kwa simu kilichokuwa humo ndani, na huyo aliyesomewa akaandika barua hiyo...

Kama mtu aliyeweka video ya Lwakatare ndiye aliyeweka barua ya Zitto... Kama barua ya Zitto imewekwa wka lengo la kuonyesha Zitto haungi mkono chama, ina maana kuwa lengo ni kumchonganisha Zitto na chama na wanachama. Ukiangalia video ya Lwakatare, utaona lengo ni kuonyesha kuwa CDM inamchukia Msaky kwa sababu yuko karibu na Zitto. Matendo yote haya mawili yana lengo moja... kuhakikisha Zitto anatenganishwa na CDM...

Namchukuru sana Zitto kwa kuendelea kuwa imara ndani ya chama, nawashukuru wanachadema wanaoamini kuwa Slaa ndiye chaguo la wengi katika kuiongoza CDM kuwatetea wanyonge, lakini viongozi wengine pia akiwemo Zitto ni muhimu sana katika kuhakikisha uimara na umoja wa CDM unadumishwa na nawaomba CDM wajue kuwa TISS wapo pale makao makuu Kinondoni pia, wanaitana Kamanda, wanasalimiana Peoples power, wanashiriki M4C, wanajifanya kuwa wanamuunga mkono Slaa na CDM kwa ujumla... lakini tusipokuwa makini kuna siku tukishakusambaratika, tutainua macho tuwaone wale "Wenzetu" wakiwa wananeemeka katika utawala wa Ibilisi...

Wake up people.... CCM hawatakubali kuachia madaraka so easily kama tunavyodhani...
Wana cdm ungeni mkono cdm sio mtu, mkiunga mkono mtu mtasambaratishwa kirahisi. Shukuruni Zitto ni kijana mzalendo na mwenye hekima sana ama sivyo ndoana mia au zaidi za ccm zingeshamtoa baharini, lakini namsifu bado anaogelea salama..
 
CHADEMA si chama cha kusambaratisha kwa vigezo vya propaganda mtupu wala utitiri wa kesi za kuchonga kila kukicha; ewe Mkuu Alibaba acha woga wako huo.

Siku zote uimara wa mti kuhimili mitikiso na vimbunga vya kila aina hutegemea sana aina ya mizizi yake na jinsi gani mizizi hiyo ilivyotanda mita kadhaa kila upande huku shina kuu la mti huo likifanya mawasiliano ya moja kwa moja bwawa kuu la maji mita kadhaa chini ya ardhi.

Ni vema tukakumbuka ya kwamba siku zote hakuna nafasi ya mtu au taasisi kama CDM kujikuta tu ndani ya RAHA bila kwanza kujikuta likihangaishwa vilivyo na utitiri wa KARAHA na KADHIA lukuki katika safari yake. Hivyo napenda nikuhakikishie ya kwamba haya mahangaiko ya CCM kujibidisha kila siku KUKIPITISHA CHADEMA kwenye tanuri la kesi za kuchonga na propaganda kibao yote kwa pamoja ni 'A NECESSARY TEST OF RESILIENCE TOLERANCE in our tomorrow leaders before we ultimately take them to Magogoni come 2015.



Zitto nakukubali sana kaka kwa jinsi unavyoendesha siasa zako na chadema kwa ujumla.

lakini mkuu nakusihi kuwa mwangalifu sana na maCCM. haya majamaa yatakutumia sana

kuisambatisha chadema kwa kuwa kwa sasa ni wewe tu unayeweza kutumika kuisambaratisha

chadema. Jitahidi sana kuwa Straight katika matamshi yako na mwepesi wa kujibu yanayokukabili.

Nakubaliana kabisa na wewe kuwa kwa sasa tunahitaji kuwa wamoja kuliko wakati wowote na

hakika mtihani huu utakijenga chama zaidi tofauti na mategemeo ya wategaji wetu lakini hili

litawezekana tu kama tutajiona na kujikuta tuko kichadema zaidi kuliko mtu mmoja mmoja.

Chadema ni chuma cha pua lazima kipitie mateso makali na hali ngumu ili kujiandaa kazi ngumu

na maalumu kuinua taifa linaloendelea kupolomoka.
 
With no offense, imani yangu na niko sahihi kabisa ni kwamba KITU KITAKACHO IMALIZA CHADEMA NI JOSEPHINE MUSHUMBUSI either
kwa michezo kama hii, au mingine atakayo iamua.

NB: Ni mtazamo tu, msinitoe meno na kucha zangu please.

Kila kitu kinawezekana aisee, umenikumbusha 24 series jinsi Jack Bauer alivosalitiwa na hawara yake Nina...mtu anafanya kazi undercover either kwa kuharibu chama au kwa kutaka kuua reputation ya Zitto ili aonekane msaliti.
 
Tanga kunani paleeee eeee Tanga shame on you Tanga peoples kumbuka Maccm ya leo hii ukiacha ile ya Mwalimu ndio wameichakachua Tanga hadi leo hii imekuwa nyuma kimaendeleo kipindi hicho tukiwa watoto miaka ya 90 wakati huo nasoma darasa la tatu kama sikosei ilkuwa Tanga atleast jinsi miaka inavyosonga Lol kila kitu chaenda mfu bana kwetu Tanga pia sema nina siku mingi jo sijatia maguu.mwisho ilikuwa mwaka ule 2002 wakati nimepitia pale Amboni Caves Lol Tanga yangu so kama umeamua kuwapa kura yako Maccm mkuu kumbuka kwetu ndio kutakufa kabisaaaaaaaaaaa.

Wee achana na Tanga kabisaaa, na kama haumini aje Slaa kama atarudi swalama.
 
Ni lini umekua na uchungu na Chadema wewe?Post zako za nyuma zinakuonyesha kuwa adui wa CHADEMA.Ni lini ulianza kukipenda?Najua unaudhika sana ninavyowaharibia mipango miovu dhidi ya Chadema.Na bado ...

Kama ningekuwa mie Ben wa Saanane kamwe nisingejibizana na hawa Wafu kabisaaa kama ujuavyo Ukibishana na mgonjwa wa akili wakati unafahamu fika jamaa ni mgonjwa wa akili na hata watu wengine wanafahamu so wewe utaonekana ndio mgonjwa zaidi Kamanda Ben Wa Saanane acha wafu wazikane wenyewe jenga Chama kama sio wewe tungefahamu vipi mikakati ya Kina Shonza Juliana,Mwampamba na Mchange.Hawa wote ni wivu wao wanaona umekuwa mwiba kwa masalia ndio maana vidomodomo vinatoa harufu kama ya panya alokufa
 
Mkuu,

Tafadhali yaache hayo. Yatatuharibia thread. Focus iwe kwenye kumshinikiza dr. Slaa ajiuzuru kwa kushindwa kutekeleza wajibuwake wa kutunza siri za ofisi.

Mimi nadhani pamoja na kushindwa kutunza siri, babu anaonesha mapungufu sana kwenye uongozi, ni yeye pekee aliyetoka wazi kusema ile video ni feki baada kupata ushauri wa IT specialist mama Junior anayeongoza chama tokea kitandani.
 
Hapa hata wakiwekeza Vipi Chama kimezeeka,hakiwezi kuchukua nchi 2015,labda wamsimamishe mzee wa mvi hapo wanaweza wakafurukuta,wakimtosa wameula wa chuya.
Na hilo la kutopendwa ndio linalo wasumbua CCM maana wanachofanya wao ni Kuichafua CHADEMA, lakini hawaonyeshi ni nani Mbadala wa CHADEMA, yeyote mwenye akili awezi kushabikia CHADEMA na akarudi kushabikia CCM na hawezi kwenda CUF, NCCR, TLP, UDP kwani hawa wote ni zilipendwa kuanzia viongozi wao mpaka vyama vyenyewe.Kwavyovyote wakitaka kufanikiwa lazima walete chama kipya chenye watu wapya na fikra mpya na hapo wanaweza wakafanikiwa kuwateka vijana wengi ambao ni mashabiki wa CHADEMA kwa sasa.
 
rais wa tano umesahau ulipokua CHADEMA nilikua nakukataza kupeleka habaribza uongo gazeti la Afrika leo na gazeti la HOJA ?

Wewe unaandika hapa kwa maslahi ya nani.Subiri JF members wafuatilie ID yako kuona kama post zako zinaonyesha nia njema kwa Chadema kama si maslahi binafsi

Nakutakia ziara njema mkoani kilimanjaro.Ila waeleze pia uliwabatiza jina la kibaguzi na kuwaita 'WAGAZZA'.Hata katibu wako mpya wa itikadi na uenezi anastahili kuomba radhi huko maana alishatoa kauli za kibaguzi.Kama huu ni unafiki nimeuendeleza na siachi.Jioni njema,
Ha ha ha ha ha Ben!
 
Last edited by a moderator:
Nimegundua kuwa kuna mbinu zimepangwa mapema kabla ya BANDIKO hili!.
Nazo ni nani wa kulaumiwa juu ya kusambazwa kwa barua ya Mh. Zitto ngoja niendelee kusoma naweza na mimi kugundua [MENTION]hugochavez[/MENTION] na [MENTION]formfourliver[/MENTION] ni nani.
 
Last edited by a moderator:
Nimetafutwa na uongozi wa JamiiForums ili kutoa maelezo kuhusu barua iliyowekwa jukwaani inayoonyesha kuwa ndani ya chama kuna kutoelewana kuhusiana na msimamo juu ya kesi inayomkabili mmoja wa viongozi waandamizi wa chama Ndg. Wilfred Lwakatare, Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa chama.

Maelezo yangu ni kama ifuatavyo:

1. Niliandika barua kwa Katibu Mkuu wa chama mnamo tarehe 15 Machi 2013 kutaka chama kifanye uchunguzi wake wa ndani kuhusiana na ukweli wa video iliyowekwa kwenye mitandao inayoonyesha kuwa Kiongozi wetu mwandamizi anapanga mipango ya kumdhuru Mhariri wa moja ya magazeti hapa nchini​. Sikuamini kabisa mambo yale na hivyo kutoa ushauri kwa chama kwamba tufanye uchunguzi wetu wa ndani ili kujiridhisha. Uchunguzi wa ndani ungetufanya kuweka mikakati wa namna bora zaidi ya kulinda chama dhidi ya njama zozote, za ndani au za nje ya chama.

2. Mapendekezo yangu ndani ya chama kamwe hayakulenga kumtosa ndugu Lwakatare wakati huu anakabiliwa na changamoto hii bali yalilenga kuhakikisha kuwa wakati tunamlinda na kumtetea ili haki itendeke, lazima tuhakikishe kuwa chama hakitaathirika na sakata hili kwa namna yeyote ile. Ni jukumu letu kuhakikisha sura (image) ya chama inabakia salama maana hatujui mikakati (game plan) ya maadui zetu kisiasa hasa baada ya kauli zao kwamba chama kitakufa kabla ya 2015 ambayo imerudiwa rudiwa sana. Ni lazima kutilia shaka (doubt) kila linalotokea sasa kwa kulipima kwa jicho la mbele zaidi. Ikumbukwe maneno ya Mwenyekiti wetu “Mwenyekiti Freeman Mbowe anataka ikithibitika kuwa Lwakatare alishiriki kurekodi mkanda huo iwe kwa kurubuniwa, ‘kushikishwa’ au kuingizwa mkenge, itamlazimu kuwajibika kwa kosa la kukosa umakini” (Gazeti la Jamhuri).

3. Barua ile ya tarehe 15 Machi 2013 ilikuwa ni ya ndani ya chama, haikuwa ya kiofisi bali ya Zitto Kabwe kwa chama, ilisainiwa na haikukusudiwa kuwa ‘public’. Nimeshangazwa sana kusikia na baadaye kuona barua yenye maudhui kama yale yale ya barua yangu kwa Katibu Mkuu imewekwa mtandaoni. Barua imewekwa masaa machache baada ya kikao cha Kamati Kuu kwisha ambapo tuliweka msimamo wa pamoja wa chama juu ya namna bora ya kushughulikia suala la Lwakatare kama chama. Wakati mweka barua anadai kuwa kulikuwa na mgawanyiko katika kikao, ukweli ni kwamba ajenda hiyo haikuwa na mjadala wenye mgawanyiko kabisa na msimamo wa chama ulipatikana kwa mwafaka bila mgawanyiko. Ni dhahiri kuwa maadui zetu walitaraji mgawanyiko na baada ya kushindwa sasa wanatengeneza mgawanyiko huo kwa kusambaza uwongo wenye uzandiki.

4. Baada ya kufanya uchunguzi mdogo nimegundua kuwa ID iliyoweka video ya Lwakatare mtandaoni na ID iliyoweka barua hii mtandaoni ni IDs za mtu mmoja. ‘Coincidence’ ya namna hii inashangaza na kushtusha, lakini inatuambia jambo moja kubwa ‘kwamba kuna kirusi ndani ya chama kilicho karibu sana na viongozi wa chama chenye kazi moja tu, yani kuonyesha kuwa CHADEMA hapako shwari, kuna migogoro na hatimaye kusambaratisha chama’. Kirusi hiki lazima kina nafasi andamizi au kipo karibu sana na viongozi waandamizi. Inawezekana kabisa kirusi hiki kinahusika na suala zima la Lwakatare katika kupanga, kuendesha na kutekeleza mpango mzima. Maswali kama ‘kwanini Dennis Msacky na Zitto ndani ya Video ya ‘Lwakatare’ lazima sasa yaanze kutafutiwa majawabu.

5. Natoa wito tena kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA kwamba, huu ni wakati wa kuwa na umoja na mshikamano kuliko wakati wowote ule katika uhai wa chama chetu. Chama cha Mapinduzi kitatumia njia zote kutugawa, kutugombanisha na kupenyeza chuki miongoni mwetu katika juhudi za wao kubakia madarakani. Umakini wa Kiongozi huonekana wakati wa changamoto kama hizi!

6. Msimamo wa chama umetolewa na Kamati Kuu iliyomaliza vikao vyake jana siku ya ijumaa tarehe 5 Aprili 2013. Huo ndio msimamo wangu pia! Kesi ya Lwakatare ipo mahakamani, chama kimeonyesha dhahiri kumwamini Jaji aliyekabidhiwa kesi hii, sasa tuache mahakama ifanye kazi yake na tusubiri hukumu. Msemaji wa chama kuhusu suala hili ni ndugu Tundu Lissu na amekuwa akitoa ufafanuzi kila inapohitajika.

Asanteni

Mimi nashauri kama Chadema wamegundua kuna "kirusi" au virusi vinavyochota mambo yao na kuyapika upya ili chama kionekane kimekosa mwelekeo, kitu kimoja tu kitawaokoa. Hakikisheni mnachosema ni kweli kabisa bila chembe ya nyongeza au punguzo. Maana yake ni kwamba kama viongozi wa Chadema wataendelea kusema ukweli na kutenda haki hawataweza kushindwa jambo, lakini ikitokea mkajichanganya, mjue umaarufu wenu utakwisha na mtaipa nafasi CCM kubaki madarakani au chama kingine mbadala kuibuka na "to take over." Watanzania wanataka ukombozi wa kweli hatwataki maneno au porojo porojo.
 
Mimi nadhani pamoja na kushindwa kutunza siri, babu anaonesha mapungufu sana kwenye uongozi, ni yeye pekee aliyetoka wazi kusema ile video ni feki baada kupata ushauri wa IT specialist mama Junior anayeongoza chama tokea kitandani.

Kuna kila sababu ya kumtaka Dr. Slaa ajiuzuru kuonyesha mfano wa uwajibikaji. La sivyo ataendelea kushusha credibility ya chadema kama chama. Next time chadema ikishinikiza kiongozi kama Kawambwa awajibike wataulizwa kwanini Dr. Slaa bado yupo madarakani?
 
Nimegundua kuwa kuna mbinu zimepangwa mapema kabla ya BANDIKO hili!.
Nazo ni nani wa kulaumiwa juu ya kusambazwa kwa barua ya Mh. Zitto ngoja niendelee kusoma naweza na mimi kugundua [MENTION]hugochavez[/MENTION] na [MENTION]formfourliver[/MENTION] ni nani.

Mbinu za kum-attack Dr. Slaa. Sasa ni dhahiri CCM wanamgwaya Dr. Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom